Nyerere 1995 Mjini Iringa: Rais mchagueni Mhe. Mkapa lakini Mbunge chagua Mgombea atakayewafaa Jimboni

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,959
141,956
Sabato ya leo nimejikuta najikumbusha kizungumkuti cha Uchaguzi Mkuu wa 1995 katika jimbo la Iringa Mjini.

Wagombea wetu walikuwa Ben Mkapa ( CCM) vs Lyatonga Mrema ( NCCR mageuzi) kwa urais.

Mwalimu wa Kemia Mfalamagoha Kibassa ( NCCR mageuzi) vs Kachero mbobezi Dr Hassy Kitine ( CCM) kwa ubunge

Kwenye mkutano wa kampeni wa CCM katika uwanja wa Samora baba wa taifa mwalimu Nyerere alisema " watu wa Iringa nawaombeni sana mumvhague Mkapa kama Rais wa JMT ili nvhi ikapate maendeleo ya kweli kwa watanzania wote na kwa upande wa ubunge ni haki yenu kumchagua mgombea yoyote mnayemuona ana uwezo wa kulisaidia jimbo " mwisho wa kunukuu.

Na matokeo yakawa Mkapa Rais na mkemia Kibassa Mbunge.

Nawatakia sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
1596890405651.png

Ni Yeye Tundu Lissu
 
Nyerere ndiye aliyeijenga hii nchi na pia aliiharibu
Likatiba aloacha ndio tatizo
Ccm wote wanafanana
Hadi Nyerere naye alikuwa walewale tu,..
Nyerere alikuwa anaogopa ushindani hadi alifuta vyama vya upinzani..
Mwisho wa siku aliikimbia ikulu kwa kibano cha kiuchumi cha wazungu..
 
Sabato ya leo nimejikuta najikumbusha kizungumkuti cha Uchaguzi Mkuu wa 1995 katika jimbo la Iringa mjini.

Wagombea wetu walikuwa Ben Mkapa ( CCM) vs Lyatonga Mrema ( NCCR mageuzi) kwa urais.

Mwalimu wa Kemia Mfalamagoha Kibassa ( NCCR mageuzi) vs Kachero mbobezi Dr Hassy Kitine ( CCM) kwa ubunge

Kwenye mkutano wa kampeni wa CCM katika uwanja wa Samora baba wa taifa mwalimu Nyerere alisema " watu wa Iringa nawaombeni sana mumvhague Mkapa kama Rais wa JMT ili nvhi ikapate maendeleo ya kweli kwa watanzania wote na kwa upande wa ubunge ni haki yenu kumchagua mgombea yoyote mnayemuona ana uwezo wa kulisaidia jimbo " mwisho wa kunukuu.

Na matokeo yakawa Mkapa Rais na mkemia Kibassa mbunge.

Nawatakia sabato yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
Kura yangu na familia yangu na kura za wafanyakazi wenzangu na familia zao tumeshakubaliana kumpa LISSU kwa sababu NI YEYE!!!
 
Back
Top Bottom