Mjue gwiji wa sheria nchini Dkt. Lamwai

Abby Uladu

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
2,031
4,236
IMG_8918.jpeg


Nenda, pita pote, mji kwa mji, kijiji kwa kijiji. Uliza nani mwamba wa sheria, Tena usisahau kupita kwa Wanazuoni wa kizazi cha 21 *uliza hilo swali, Pita *Udom, Udsm, Mzumbe, Saut, Tudarco mpaka,Ruco kwa wakatoliki. Wote watakujibu Gwiji wa sheria ni Kibatala na Tundu lissu, wakienda mbali watamtaja Mnyakusa wakili Mwabukusi wa Mwanjelwa.

Sasa acha hao wote, kuna huyu mwamba ambaye kawapiku wote, Rekodi yake haijawahi kuvunjwa na wote hao. Ubaya ni kuwa Hakufanya kazi zake kipindi Watoto wa Mkapa na JK tunazaliwa.

Huyu Mwamba alizitesa mahakama za Taifa hili Mpaka zikakubali, Hayati Jaji kisanga na Nyalali waliukubali mtikiso wa Mwamba huyu haijawahi kutokea.

Huyu Ndiyo Dr Masumbuko Mahunga Selasini Lamwai. almarufu Dr Lamwai, mzaliwa wa mkoa adhimu wa kilimajaro aliyezikataa zile mbichi na kuiheshimisha tasnia ya uwakili nchini.

Kwanza ni Genius vibaya mno, Alipoenda kusoma Chuo kikuu Cha Oxford- Uingereza aliwapiga na kitu kizito wazungu, aliwaambia yeye anao uwezo wa kusoma miaka miwili kozi ya miaka minne. Wakamjaribu, Mwamba akagraduate na kuwaacha wazungu wakomae na miaka minne.

Alihitimu PhD ya Criminal & Procedural law kwa miaka miwili tu badala ya minne. huu utaratibu ulikuwepo pale chuoni.

Mpaka sasa anatajwa kuwa ndiye Mwanafunzi pekee kutoka afrika aliyewahi kuhitimu hiyo fani kwa Miaka miwili.

Dr Lamwai alikuwa wakili matata Sana. Aliingia Bungeni kama Mbunge wa jimbo la ubungo mwaka 1995. Akiwa Bungeni aligoma kuapa kiapo cha utii kwa Rais. Akatoa hoja kuwa Bunge ni muhimili unaojitegemea, hivyo, sio Sawa mbunge kuapa kiapo cha utii kwa Rais, mwamba akamfundisha Spika dhana ya Separation of power, akampa vifungu konki Spika Pius Msekwa.

Spika Msekwa, akaamuru sheria ya kiapo cha utii irekebishwe na kufuta kipengele cha wabunge kuapa utii kwa Rais, wabunge wote walirudia kuapa upya mwaka huo na mpaka sasa wabunge hawaapi kiapo cha utii kwa Rais kwasababu ya ufundi wa Dr lamwai.

Dr Lamwai aliwahi kumshikisha adabu waziri mmoja aliye kuwa mwanamama. Alimpiga cross examination ya kichokozi kinoma, alimuuliza; "Inaonekana wewe ni Malaya Sana?", waziri akachukia, akaanza kutukana hovyo hovyo mahakamani.

Mwamba akatoa picha za Watoto wanne wa yule waziri akamuuliza; "Hawa ni wanao?", Waziri akakubali. Wakili lamwai akatoa picha za wanaume wanne akamwambia; iambie mahakama Hawa ni Akina nani?. Waziri akainamisha kichwa kwa aibu. Basi umalaya ukathibitishwa na wakili lamwai, kwani kila mtoto alikuwa na Baba yake kwenye zile picha. Yaani waziri alizaa na wanamume wanne tofauti. Huu ni utundu wa Dr lamwai.

Dr lamwai aliwahi Kusimamia kesi maarufu ya kupinga ushindi wa ubunge jimbo la temeke mwaka 1996 Ambapo alishinda na kumng'oa kitini mh Ramadhan kihiyo kwa tuhuma za kudanganya elimu yake.

Dr lamwai alikuwa kivutio kikubwa kwa vijana enzi za miaka ya 90. Inasemekana watu walilala kwenye stesheni za treni kumsubili lamwai.

Lamwai alikuwa mbunge wa kwanza wa chama cha upinzani NCCR-mageuzi katika jimbo la ubungo, aliitumia Taaluma ya sheria kushinikiza mambo nyeti na muhimu Bungeni.

Baada ya kuitesa serikali kwa muda mrefu, kisasi kikamfikia. Dr lamwai alifukuzwa kazi pale Udsm alipokuwa akifundisha sheria, akafanyiwa figisu akapoteza ubunge, akaporwa leseni ya uwakili, Mali zake zikataifishwa. akabaki yeye na nguo zake tu. Akaishi kwa dhiki muda mrefu hadi alipoamua kujiunga na chama tawala-CCM ndipo akarudishiwa leseni ya uwakili na mali zake.

Dr lamwai ametoa vipanga wa sheria nchini. Mfano mzuri ni wakili Msomi John Malya. Hiki kichwa kiliandaliwa na Dr lamwai pale chuo kikuu Cha Tumaini - dar es salaam.

Dr lamwai alifariki mwaka 2020 kwa maradhi.
 
Ukiona msomi yeyote kaingia kwenye siasa, elewa kuwa huyo kasoma lakini hajaelimika.

Msomi kuingia kwenye siass iwe kwenye miaka yake ya kustaafu, ndipo kweli bado ana nia ya kuitumikia jamii.

Tazama kina Dr. Janabi, na fursa zote walizonazo na usomi wao lakini wamekataa kabisa kuingia kwenye siasa, Janabi alikataa mpaka uwaziri, anasema anataka kuitendea haki elimu yake. Hao ndiyo wasomi walioelimika.
 
Huku Dr Masumbuko Lamwai, Kule Joseph Selasini, pemben Mabere Marando katikati Lyatonga

winga akiwa Dr Walid Aman Walid Kabourou

nyuma yupo Dr Mihogo, bila ya kumsahau Prof nguli wa Uchumi

1995 ilikuwa ngumu sana kumwambia hata msomi kuwa hawa wote walikuwa 'watoto wa Baba mmoja ' ila baadae sana hatukutumia nguvu sana watu kuamini

next 20 years kuna Makamanda watu watakuwa hawataki hata kuwasikia japo sasa hivi huwaambi kitu

Kikosi cha Wabunge walioingia kwa tiketi ya vyama vingine ilikuwa hatare sana aisee

Igizo lilikuwa kama Hollywood hadi kina Prof Simon Mbilinyi wakang'oka mapema sana kwa ma kashfa kashfa

kuna Mwana Mama aliitwa Fatma Maghimbi ndio aligoma kuapishwa ilipofika zamu yake akiwa ndio Kiongozi wa kwanza wa Kambi ya Upinzani Bungeni

Heka heka za Dr Masumboko Lamwai ndio lilizalisha neno maarufu la Kihiyo kwny kesi ya Ubunge Jimbo la Temeke akimtetea Tambwe hiza

woooote hawa Wamerejea kwa Mola wao wakiwa wamesharudi CCM
 
Back
Top Bottom