Historia isiyofahamika na wana Ngara wengi kuhusu wabunge waliowahi kuliongoza Jimbo la Ngara toka uhuru mpaka sasa

josias

Member
Jan 7, 2014
47
34
HISTORIA ISIYOFAHAMIKA NA WANA NGARA WENGI KUHUSU WABUNGE WALIOWAHI KULIONGOZA JIMBO LA NGARA TOKA UHURU MPAKA SASA.

Mara kadhaa kumekuwa na ubishani kuhusu Wabunge waliowahi kuongoza Jimbo la Ngara toka Uhuru mpaka sasa. Pia kumekuwa na upotoshaji kuwa Jimbo la Ngara halijawahi kuongozwa na Mbunge yeyote kwa Awamu Mbili Mfululizo.

Utangulizi:-
Historia ya Bunge la Tanzania inaanzia Mwaka 1926 wakati huo likiitwa Bunge la Tanganyika (Bunge la Mkoloni). Bunge hili liliundwa na Wabunge 20 waliokuwa wanateuliwa na Gavana ambaye ni Muingereza.

Mwaka 1957 kulitokea marekebisho ya madogo ya Sheria yaliyotaka Bunge liwe na uwakilishi wa Wabunge wa kupigiwa kura. Mnamo mwaka 1958 uchaguzi wa kwanza ulifanyika na hapo ndipo Bunge la Tanganyika likaitwa Tanganyika Legislative Council (LEGCO). Kupitia mabadiliko hayo ndipo Sir George Kahama alichaguliwa kuwakilisha Jimbo la West Lake ambalo lilikuwa linajumuisha maeneo yote ya Bukoba hadi Ngara. Baada ya Serikali kutangaza Mikoa eneo la Jimbo la West Lake liliitwa Mkoa wa Ziwa Magharibi na baadae mwaka 1980 Mkoa wa Ziwa Magharibi ulibadilishwa jina na Kuitwa Mkoa wa Kagera hadi sasa.

Kwa Msaada wa maarifa toka kwa baadhi ya wana Ngara nimekuandalia List nzima ya Wabunge waliowahi kuliongoza Jimbo la Ngara kwa nyakati tofauti tofauti:-

Sir. George Kahama(1958-1960)
Huyu aliongoza eneo la Ngara katika Kipindi cha Bunge la ukoloni Tanganyika (Tanganyika Legislative Council -LEGCO). Sir.Gorge Kahama aliiongoza Ngara kati ya Mwaka 1958-1960 katika Kipindi ambacho Ngara, Biharamuro na Karagwe ilitambuliwa kuwa ni Jimbo moja lililoitwa Jimbo la West Lake. Mbunge George Kahama alikuwa mwenyeji wa Karagwe.

Edward Barongo (1960-1965)
Mnamo Mwaka 1960 Bunge lilifanyiwa mabadaliko tena. Mabadiliko haya yalipelekea kuchaguliwa kwa Wabunge ikiwa ni maandalizi ya Tanganyika kupata Uhuru. Kupitia mabadiliko haya ndipo Edward Barongo akawa Mbunge wa Jimbo la Ngara hadi Mwaka 1965 ilipoanzishwa Bunge la kwanza la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika Kipindi hicho ndipo Ngara ikatambuliwa rasmi kama Jimbo la Uchaguzi. Uchaguzi wa Mwaka 1965 ndipo kwa mara ya kwanza Ngara ikapata Mbunge wa Jimbo la Ngara ambaye alikuwa Ndugu. Edwin Nyamubi.

Edwin Nyamubi (1965-1970)
Huyu alikuwa Mbunge wa Kwanza wa Jimbo la Ngara baada ya Tanganyika kupata Uhuru. Aliwakilisha Jimbo la Ngara katika Bunge la Kwanza la Tanzania kuanzia mwaka 1965- 1970. Katika Kipindi hiki Karagwe na Biharamuro zilitenganishwa na Ngara na kila Wilaya ikawa na Mbunge wake. Edwin Nyamubi alikuwa mwenyeji wa Murugwanza Ngara.

Filimon Niboye Biholabikenyeye (1970-1975)
Hakuna taarifa nyingi kuhusu Mbunge huyu zilizofanikiwa kukusanywa. F. N. Biholabikenyeye ni Mzaliwa wa Muruvyagira Wilayani Ngara.

Angus Gwasa Sebabili (1975-1990) na 1980-1985.
Huyu alikuwa Gwiji kweli kweli wa Siasa za Ngara. Alikuwa Mbunge wa kwanza kuongoza Ngara kwa Vipindi viwili Mfululizo na pia Mbunge wa Kwanza kuiongoza Ngara kwa Awamu tatu kwani aliiongoza Ngara tena mwaka 2000-2005. Angus Gwasa Sebabili alishika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Waziri wa Afya. Angus Gwasa Sebabili alikuwa mzaliwa wa Kata ya Kanazi.

Jeremiah Jared John Gachocha (1985-1990 na 1990-1995)
Mbunge huyu alikuwa Mbunge wa Pili kuiongoza Ngara kwa Awamu Mbili Mfululizo. Mbunge Gachocha anakumbukwa Sana kwa Harakati zake ndani ya Bunge kwani alikuwa sehemu ya Wakundi 55 waliokuwa wakiunda Kundi la G55 ambalo lilikuwa likidai Uwepo wa Serikali ya Tanganyika ili kuwa na Serikali Tatu.
waliosimama Bunge wakiongoza na Njelu Kasaka kudai Tanganyika na mageuzi ya Katiba. Kipindi kile akiwa Bungeni, japo lilikuwa Bunge la chama kimoja, lakini Gachocha alipata umaarufu mkubwa wa kuwa mtetezi wa hoja nzito za kuibana Serikali.
Kundi la akina Gachocha lilitaka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utizamwe upya kwani ulizaliwa bila kupata baraka za wananchi wengine na hivyo kuwa na mapungufu. Walifikiria kwamba kwa wakati huo Muungano ulizaliwa kwa makubaliano tu kati ya TANU na Afro-Shiraz Party (ASP), lakini bila ridhaa ya wananchi.
Kwa muda mrefu Jared Gachocha ameishi Mkoani Mwanza na Mwaka 2010 aligombea ubunge Ilemela na kushindwa kura za maoni.
Gachocha alikuwa mzaliwa wa Kata ya Kanazi Wilayani Ngara.

Pius Ngeze (1995-2000)
Pius Ngeze alianza safari yake ya Siasa kama Mwenyekiti wa kwanza wa
TANU tawi la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Iringa
Mnano mwaka 1974 mpaka mwaka 1975 na
mjumbe wa kamati ya siasa ya Tawi la Ofisi ya
Waziri Mkuu na Makamu wa pili wa Rais
Dodoma toka mwaka 1975 mpaka mwaka
1977. Baada ya TANU kubadili Jina na Kuitwa Chama cha Mapinduzi (CCM),Pius Ngeze alishika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera.
Mwaka 1995 mpaka mwaka 2000, alikuwa
Mbunge wa jimbo la Ngara ambapo aliongoza Jimbo la Ngara kwa awamu moja pekee. Pius Ngeze ni Mzaliwa wa Tarafa ya Murusagamba lakini akiwa na Makazi Tarafa ya Rulenge Wilayani Ngara pamoja na Wilaya ya Bukoba Mjini.

Angus Gwasa Sebabili (2000-2005)
Ndugu Angus Gwasa Sebabili aliongoza Jimbo la Ngara kwa awamu nyingine kati ya mwaka 2000-2005 baada ya kuongoza Jimbo hilo katika awamu mbili kati ya 1975-1980 na 1980-1985).

Prof. Feetham Philipo Banyikwa (2005-2010)
Huyu ni Msomi wa Ngazi za Juu katika Masuala ya Mimea akiwa amesoma katika vyuo Vikuu mbalimbali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Syracuse University kutoka Marekan na pia Muhadhiri wa Vyuo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Aliiingoza Ngara kama Mbunge kati ya Mwaka 2005-2010. Profesa Banyikwa anaingia pia katika kundi la Wabunge walioiongoza Ngara kwa awamu moja. Professor Banyikwa ni Mzaliwa wa Mabawe Wilayani Ngara.

Deogratias Ntukamazina. (2010-2015)
Moja ya Wabunge wanye wasifu Mkubwa katika Utumishi wa Umma nchini Tanzania. Alihudumu kama Mbunge wa Jimbo ka Ngara kati ya Mwaka 2010-2015 kwa awamu moja. Deogratias Ntukamazina ndiye Mbunge pekee aliyestaafu Ubunge kwa Hiyari yake tofauti na wengine ambao waliangushwa kupitia Kura za Maoni. Deogratias Ntukamazina ni Mzaliwa wa Tarafa ya Rulenge Wilayani Ngara.

Alex Raphael Gashaza. (2015-2020)
Alex Gashaza ni mwanasiasa ambaye alipambana bila kuchoka kutetea nafasi ya Kuliongoza Jimbo la Ngara toka zilipoanza Siasa za Vyama vingi Mwaka 1995. Mara zote alizoshiriki uchaguzi iliaminika kuwa ameshinda kutokana na ushawishi aliokuwa nao. Alex Gashaza alikuwa mwanachama machachali wa NCCR- Mageuzi na aligombea Ubunge wa Jimbo la Ngara mwaka 2000 akiwa NCCR- Mageuzi dhidi ya Angus Sebabili Alex Gashaza alikuwa kijana mwenye hoja za ushawishi, alivutia wengi na kupata umaarufu, mkubwa kupitia NCCR Mageuzi. Mnamo mwaka 2005 alihamia CCM. Alitangaza Kugombea Ubunge Kupitia CCM mnamo mwaka 2005 na 2010 japo hakufanikiwa kwenye Kura za maoni. Alitangaza nia ya kugombea tena Ubunge mwaka 2015 na alifanikiwa kuteuliwa kuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ngara kupitia CCM. Alex Gashaza alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara kwa awamu moja pia. Alex Gashaza ni Mzaliwa wa Mulukurazo na Mkazi wa Kata ya Ngara Mjini.

Ndaisaba George Ruhoro (2020- Mpaka sasa)
Mbunge Kijana, Msomi wa Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Aliingia Madarakani Mwaka 2020. Ndaisaba George Ruhoro ni Mzaliwa wa Kanazi Wilayani Ngara.

Hitimisho: Wabunge waliofanikiwa Kuliongoza Jimbo la Ngara kwa zaidi ya Awamu moja ni wawili pekee ambao ni, Gwasa Sebabili 1975-80, 1980-85 na Mwaka 2000-2005, Mbunge wa Pili kuliongoza Jimbo la Ngara kwa zaidi ya awamu moja ni Ndugu Jared John Gachocha 1985-90, na 1990-95. Je Mbunge wa sasa Ndugu Ndaisaba George Ruhoro atafanikiwa Kuweka Record ya Kuwa Mbunge wa Tatu kuongoza Jimbo la Ngara kwa zaidi ya awamu moja?

(Unaweza kuboresha andiko hili kwa kuongeza taarifa za Kweli na za Uhakika Pekee).

©By Josias Charles
Credit : Sam Ruhuza
Images Sir George Kahama and Ndaisaba George Ruhoro
imgonline-com-ua-twotoone-Zi6HR9PzClB (1).jpg
 
Mara kadhaa kumekuwa na ubishani kuhusu Wabunge waliowahi kuongoza Jimbo la Ngara toka Uhuru mpaka sasa. Pia kumekuwa na upotoshaji kuwa Jimbo la Ngara halijawahi kuongozwa na Mbunge yeyote kwa Awamu Mbili Mfululizo. Kwa Msaada wa maarifa toka kwa baadhi ya wana Ngara nimekuandalia List nzima ya Wabunge waliowahi kuliongoza Jimbo la Ngara kwa nyakati tofauti tofauti:-

Sir. George Kahama
Huyu aliongoza eneo la Ngara katika Kipindi cha Bunge la ukoloni Tanganyika na miaka michache baada ya Uhuru. Kipindi hicho Ngara, Biharamuro na Karagwe ilitambuliwa kuwa ni Jimbo moja. Mbunge George Kahama alikuwa mwenyeji wa Karagwe.

Edwin Nyamubi
Huyu alikuwa Mbunge wa Kwanza wa Jimbo la Ngara baada ya Tanganyika kupata Uhuru. Aliwakilisha Jimbo la Ngara katika Bunge la Kwanza la Tanzania kuanzia mwaka 1965- 1970. Katika Kipindi hiki Karagwe na Biharamuro zilitenganishwa na Ngara na kila Wilaya ikawa na Mbunge wake. Edwin Nyamubi alikuwa mwenyeji wa Murugwanza Ngara.

Filimon Niboye Biholabikenyeye (1970-1975)
Hakuna taarifa nyingi kuhusu Mbunge huyu zilizofanikiwa kukusanywa. F. N. Biholabikenyeye ni Mzaliwa wa Muruvyagira Wilayani Ngara.

Angus Gwasa Sebabili (1975-1990) na 1980-1985
Huyu alikuwa Gwiji kweli kweli wa Siasa za Ngara. Alikuwa Mbunge wa kwanza kuongoza Ngara kwa Vipindi viwili Mfululizo na pia Mbunge wa Kwanza kuiongoza Ngara kwa Awamu tatu kwani aliiongoza Ngara tena mwaka 2000-2005. Angus Gwasa Sebabili alishika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Waziri wa Afya. Angus Gwasa Sebabili alikuwa mzaliwa wa Kata ya Kanazi.

Jeremiah Jared John Gachocha (1985-1990 na 1990-1995)
Mbunge huyu alikuwa Mbunge wa Pili kuiongoza Ngara kwa Awamu Mbili Mfululizo. Mbunge Gachocha anakumbukwa Sana kwa Harakati zake ndani ya Bunge kwani alikuwa sehemu ya Wakundi 65 waliokuwa wakiunda Kundi la G55 ambalo lilikuwa likidai Uwepo wa Serikali ya Tanganyika ili kuwa na Serikali Tatu.

Kundi la akina Gachocha lilitaka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utizamwe upya kwani ulizaliwa bila kupata baraka za wananchi wengine na hivyo kuwa na mapungufu. Walifikiria kwamba kwa wakati huo Muungano ulizaliwa kwa makubaliano tu kati ya TANU na Afro-Shiraz Party (ASP), lakini bila ridhaa ya wananchi.

Kwa muda mrefu Jared Gachocha ameishi Mkoani Mwanza na Mwaka 2010 aligombea ubunge Ilemela na kushindwa kura za maoni.
Gachocha alikuwa mzaliwa wa Kata ya Kanazi Wilayani Ngara.

Pius Ngeze (1995-2000)
Pius Ngeze alianza safari yake ya Siasa kama Mwenyekiti wa kwanza wa
TANU tawi la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Iringa
Mnano mwaka 1974 mpaka mwaka 1975 na
mjumbe wa kamati ya siasa ya Tawi la Ofisi ya
Waziri Mkuu na Makamu wa pili wa Rais
Dodoma toka mwaka 1975 mpaka mwaka
1977.

Baada ya TANU kubadili Jina na Kuitwa Chama cha Mapinduzi (CCM),Pius Ngeze alishika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera.
Mwaka 1995 mpaka mwaka 2000, alikuwa
Mbunge wa jimbo la Ngara ambapo aliongoza Jimbo la Ngara kwa awamu moja pekee. Pius Ngeze ni Mzaliwa wa Tarafa ya Murusagamba lakini akiwa na Makazi Tarafa ya Rulenge Wilayani Ngara pamoja na Wilaya ya Bukoba Mjini.

Angus Gwasa Sebabili (2000-2005)
Ndugu Angus Gwasa Sebabili aliongoza Jimbo la Ngara kwa awamu nyingine kati ya mwaka 2000-2005 baada ya kuongoza Jimbo hilo katika awamu mbili kati ya 1975-1980 na 1980-1985).

Prof. Feetham Philipo Banyikwa (2005-2010)
Huyu ni Msomi wa Ngazi za Juu katika Masuala ya Mimea akiwa amesoma katika vyuo Vikuu mbalimbali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Syracuse University kutoka Marekan na pia Muhadhiri wa Vyuo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Aliiingoza Ngara kama Mbunge kati ya Mwaka 2005-2010. Profesa Banyikwa anaingia pia katika kundi la Wabunge walioiongoza Ngara kwa awamu moja. Professor Banyikwa ni Mzaliwa wa Mabawe Wilayani Ngara.

Deogratias Ntukamazina. (2010-2015)
Moja ya Wabunge wanye wasifu Mkubwa katika Utumishi wa Umma nchini Tanzania. Alihudumu kama Mbunge wa Jimbo ka Ngara kati ya Mwaka 2010-2015 kwa awamu moja. Deogratias Ntukamazina ndiye Mbunge pekee aliyestaafu Ubunge kwa Hiyari yake tofauti na wengine ambao waliangushwa kupitia Kura za Maoni. Deogratias Ntukamazina ni Mzaliwa wa Tarafa ya Rulenge Wilayani Ngara.

Alex Raphael Gashaza. (2015-2020)
Alex Gashaza ni mwanasiasa ambaye alipambana bila kuchoka kutetea nafasi ya Kuliongoza Jimbo la Ngara toka zilipoanza Siasa za Vyama vingi Mwaka 1995. Mara zote alizoshiriki uchaguzi iliaminika kuwa ameshinda kutokana na ushawishi aliokuwa nao. Hali hiyo ilimlazimu kuhama Mara kadhaa kutoka CCM kwenda NCCR Mageuzi hadi pale alipoteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) Kugombea nafasi ya Ubunge Mwaka 2015 ambapo aliibuka na ushindi Mkubwa. Alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara kwa awamu moja pia. Alex Gashaza ni Mkazi wa Ngara Mjini.

Ndaisaba George Ruhoro (2025- Mpaka sasa)
Mbunge Kijana, Msomi wa Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Aliingia Madarakani Mwaka 2020. Ndaisaba George Ruhoro ni Mzaliwa wa Kanazi Wilayani Ngara.

Hitimisho: Wabunge waliofanikiwa Kuliongoza Jimbo la Ngara kwa zaidi ya Awamu moja ni wawili pekee ambao ni, Gwasa Sebabili 1975-80, 1980-85 na Mwaka 2000-2005, Mbunge wa Pili kuliongoza Jimbo la Ngara kwa zaidi ya awamu moja ni Ndugu Jeremiah Jared John Gachocha 1985-90, na 1990-95. Je Mbunge wa sasa Ndugu Ndaisaba George Ruhoro atafanikiwa Kuweka Record ya Kuwa Mbunge wa Tatu kuongoza Jimbo la Ngara kwa zaidi ya awamu moja?

(Unaweza kuboresha andiko hili kwa kuongeza taarifa za Kweli na za Uhakika Pekee).

©By Josias Charles
Credit : Sam Ruhuza
Waliongoza au waliwakilisha?
 
HISTORIA ISIYOFAHAMIKA NA WANA NGARA WENGI KUHUSU WABUNGE WALIOWAHI KULIONGOZA JIMBO LA NGARA TOKA UHURU MPAKA SASA.

Mara kadhaa kumekuwa na ubishani kuhusu Wabunge waliowahi kuongoza Jimbo la Ngara toka Uhuru mpaka sasa. Pia kumekuwa na upotoshaji kuwa Jimbo la Ngara halijawahi kuongozwa na Mbunge yeyote kwa Awamu Mbili Mfululizo.

Utangulizi:-
Historia ya Bunge la Tanzania inaanzia Mwaka 1926 wakati huo likiitwa Bunge la Tanganyika (Bunge la Mkoloni). Bunge hili liliundwa na Wabunge 20 waliokuwa wanateuliwa na Gavana ambaye ni Muingereza.

Mwaka 1957 kulitokea marekebisho ya madogo ya Sheria yaliyotaka Bunge liwe na uwakilishi wa Wabunge wa kupigiwa kura. Mnamo mwaka 1958 uchaguzi wa kwanza ulifanyika na hapo ndipo Bunge la Tanganyika likaitwa Tanganyika Legislative Council (LEGCO). Kupitia mabadiliko hayo ndipo Sir George Kahama alichaguliwa kuwakilisha Jimbo la West Lake ambalo lilikuwa linajumuisha maeneo yote ya Bukoba hadi Ngara. Baada ya Serikali kutangaza Mikoa eneo la Jimbo la West Lake liliitwa Mkoa wa Ziwa Magharibi na baadae mwaka 1980 Mkoa wa Ziwa Magharibi ulibadilishwa jina na Kuitwa Mkoa wa Kagera hadi sasa.

Kwa Msaada wa maarifa toka kwa baadhi ya wana Ngara nimekuandalia List nzima ya Wabunge waliowahi kuliongoza Jimbo la Ngara kwa nyakati tofauti tofauti:-

Sir. George Kahama(1958-1960)
Huyu aliongoza eneo la Ngara katika Kipindi cha Bunge la ukoloni Tanganyika (Tanganyika Legislative Council -LEGCO). Sir.Gorge Kahama aliiongoza Ngara kati ya Mwaka 1958-1960 katika Kipindi ambacho Ngara, Biharamuro na Karagwe ilitambuliwa kuwa ni Jimbo moja lililoitwa Jimbo la West Lake. Mbunge George Kahama alikuwa mwenyeji wa Karagwe.

Edward Barongo (1960-1965)
Mnamo Mwaka 1960 Bunge lilifanyiwa mabadaliko tena. Mabadiliko haya yalipelekea kuchaguliwa kwa Wabunge ikiwa ni maandalizi ya Tanganyika kupata Uhuru. Kupitia mabadiliko haya ndipo Edward Barongo akawa Mbunge wa Jimbo la Ngara hadi Mwaka 1965 ilipoanzishwa Bunge la kwanza la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika Kipindi hicho ndipo Ngara ikatambuliwa rasmi kama Jimbo la Uchaguzi. Uchaguzi wa Mwaka 1965 ndipo kwa mara ya kwanza Ngara ikapata Mbunge wa Jimbo la Ngara ambaye alikuwa Ndugu. Edwin Nyamubi.

Edwin Nyamubi (1965-1970)
Huyu alikuwa Mbunge wa Kwanza wa Jimbo la Ngara baada ya Tanganyika kupata Uhuru. Aliwakilisha Jimbo la Ngara katika Bunge la Kwanza la Tanzania kuanzia mwaka 1965- 1970. Katika Kipindi hiki Karagwe na Biharamuro zilitenganishwa na Ngara na kila Wilaya ikawa na Mbunge wake. Edwin Nyamubi alikuwa mwenyeji wa Murugwanza Ngara.

Filimon Niboye Biholabikenyeye (1970-1975)
Hakuna taarifa nyingi kuhusu Mbunge huyu zilizofanikiwa kukusanywa. F. N. Biholabikenyeye ni Mzaliwa wa Muruvyagira Wilayani Ngara.

Angus Gwasa Sebabili (1975-1990) na 1980-1985.
Huyu alikuwa Gwiji kweli kweli wa Siasa za Ngara. Alikuwa Mbunge wa kwanza kuongoza Ngara kwa Vipindi viwili Mfululizo na pia Mbunge wa Kwanza kuiongoza Ngara kwa Awamu tatu kwani aliiongoza Ngara tena mwaka 2000-2005. Angus Gwasa Sebabili alishika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Waziri wa Afya. Angus Gwasa Sebabili alikuwa mzaliwa wa Kata ya Kanazi.

Jeremiah Jared John Gachocha (1985-1990 na 1990-1995)
Mbunge huyu alikuwa Mbunge wa Pili kuiongoza Ngara kwa Awamu Mbili Mfululizo. Mbunge Gachocha anakumbukwa Sana kwa Harakati zake ndani ya Bunge kwani alikuwa sehemu ya Wakundi 55 waliokuwa wakiunda Kundi la G55 ambalo lilikuwa likidai Uwepo wa Serikali ya Tanganyika ili kuwa na Serikali Tatu.
waliosimama Bunge wakiongoza na Njelu Kasaka kudai Tanganyika na mageuzi ya Katiba. Kipindi kile akiwa Bungeni, japo lilikuwa Bunge la chama kimoja, lakini Gachocha alipata umaarufu mkubwa wa kuwa mtetezi wa hoja nzito za kuibana Serikali.
Kundi la akina Gachocha lilitaka Muungano wa Tanganyika na Zanzibar utizamwe upya kwani ulizaliwa bila kupata baraka za wananchi wengine na hivyo kuwa na mapungufu. Walifikiria kwamba kwa wakati huo Muungano ulizaliwa kwa makubaliano tu kati ya TANU na Afro-Shiraz Party (ASP), lakini bila ridhaa ya wananchi.
Kwa muda mrefu Jared Gachocha ameishi Mkoani Mwanza na Mwaka 2010 aligombea ubunge Ilemela na kushindwa kura za maoni.
Gachocha alikuwa mzaliwa wa Kata ya Kanazi Wilayani Ngara.

Pius Ngeze (1995-2000)
Pius Ngeze alianza safari yake ya Siasa kama Mwenyekiti wa kwanza wa
TANU tawi la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Iringa
Mnano mwaka 1974 mpaka mwaka 1975 na
mjumbe wa kamati ya siasa ya Tawi la Ofisi ya
Waziri Mkuu na Makamu wa pili wa Rais
Dodoma toka mwaka 1975 mpaka mwaka
1977. Baada ya TANU kubadili Jina na Kuitwa Chama cha Mapinduzi (CCM),Pius Ngeze alishika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera.
Mwaka 1995 mpaka mwaka 2000, alikuwa
Mbunge wa jimbo la Ngara ambapo aliongoza Jimbo la Ngara kwa awamu moja pekee. Pius Ngeze ni Mzaliwa wa Tarafa ya Murusagamba lakini akiwa na Makazi Tarafa ya Rulenge Wilayani Ngara pamoja na Wilaya ya Bukoba Mjini.

Angus Gwasa Sebabili (2000-2005)
Ndugu Angus Gwasa Sebabili aliongoza Jimbo la Ngara kwa awamu nyingine kati ya mwaka 2000-2005 baada ya kuongoza Jimbo hilo katika awamu mbili kati ya 1975-1980 na 1980-1985).

Prof. Feetham Philipo Banyikwa (2005-2010)
Huyu ni Msomi wa Ngazi za Juu katika Masuala ya Mimea akiwa amesoma katika vyuo Vikuu mbalimbali kama vile Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Syracuse University kutoka Marekan na pia Muhadhiri wa Vyuo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Aliiingoza Ngara kama Mbunge kati ya Mwaka 2005-2010. Profesa Banyikwa anaingia pia katika kundi la Wabunge walioiongoza Ngara kwa awamu moja. Professor Banyikwa ni Mzaliwa wa Mabawe Wilayani Ngara.

Deogratias Ntukamazina. (2010-2015)
Moja ya Wabunge wanye wasifu Mkubwa katika Utumishi wa Umma nchini Tanzania. Alihudumu kama Mbunge wa Jimbo ka Ngara kati ya Mwaka 2010-2015 kwa awamu moja. Deogratias Ntukamazina ndiye Mbunge pekee aliyestaafu Ubunge kwa Hiyari yake tofauti na wengine ambao waliangushwa kupitia Kura za Maoni. Deogratias Ntukamazina ni Mzaliwa wa Tarafa ya Rulenge Wilayani Ngara.

Alex Raphael Gashaza. (2015-2020)
Alex Gashaza ni mwanasiasa ambaye alipambana bila kuchoka kutetea nafasi ya Kuliongoza Jimbo la Ngara toka zilipoanza Siasa za Vyama vingi Mwaka 1995. Mara zote alizoshiriki uchaguzi iliaminika kuwa ameshinda kutokana na ushawishi aliokuwa nao. Alex Gashaza alikuwa mwanachama machachali wa NCCR- Mageuzi na aligombea Ubunge wa Jimbo la Ngara mwaka 2000 akiwa NCCR- Mageuzi dhidi ya Angus Sebabili Alex Gashaza alikuwa kijana mwenye hoja za ushawishi, alivutia wengi na kupata umaarufu, mkubwa kupitia NCCR Mageuzi. Mnamo mwaka 2005 alihamia CCM. Alitangaza Kugombea Ubunge Kupitia CCM mnamo mwaka 2005 na 2010 japo hakufanikiwa kwenye Kura za maoni. Alitangaza nia ya kugombea tena Ubunge mwaka 2015 na alifanikiwa kuteuliwa kuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ngara kupitia CCM. Alex Gashaza alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara kwa awamu moja pia. Alex Gashaza ni Mzaliwa wa Mulukurazo na Mkazi wa Kata ya Ngara Mjini.

Ndaisaba George Ruhoro (2020- Mpaka sasa)
Mbunge Kijana, Msomi wa Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Aliingia Madarakani Mwaka 2020. Ndaisaba George Ruhoro ni Mzaliwa wa Kanazi Wilayani Ngara.

Hitimisho: Wabunge waliofanikiwa Kuliongoza Jimbo la Ngara kwa zaidi ya Awamu moja ni wawili pekee ambao ni, Gwasa Sebabili 1975-80, 1980-85 na Mwaka 2000-2005, Mbunge wa Pili kuliongoza Jimbo la Ngara kwa zaidi ya awamu moja ni Ndugu Jared John Gachocha 1985-90, na 1990-95. Je Mbunge wa sasa Ndugu Ndaisaba George Ruhoro atafanikiwa Kuweka Record ya Kuwa Mbunge wa Tatu kuongoza Jimbo la Ngara kwa zaidi ya awamu moja?

(Unaweza kuboresha andiko hili kwa kuongeza taarifa za Kweli na za Uhakika Pekee).

By Josias Charles
Credit : Sam Ruhuza
Images Sir George Kahama and Ndaisaba George RuhoroView attachment 2842384
Huyu wa Sasa ameshindwa kaba hajashindwa si huyu ndio anatoa picha yake kwa wafanyabiashara waweke eneo la biashara
 
Hawa wote asilimia Kubwa ya uraia wao ni Wanyarwanda; hususan 20% Watanganyika/ Watanzania kwa sababu kijiografia wapo Tanzania; lakini 80% ni Wanyarwanda kwa sababu Mila na desturi zao ni za Kinyarwanda ikiwa ni pamoja na majina.
Nawakumbuka zaidi Sir George Kahama na Edward Barongo maana walikuwa "vichwa."
Majina yao yalitawala vyombo vya habari kutoka ushiriki wao kwenye masuala ya kitaifa kutoka na nafasi zao.
Gwasa Sebabili naye hakuwa nyuma; na kwa wenyeji wa mkoa wa Shinyanga, Wahenga hatuwezi kumsahau kwa sababu alikuwa Mkuu wetu Mkoa.
Hao miamba tuliwafahamu sisi wenyeji wa mkoa wa Shinyanga kuliko hata wabunge wetu akina Nzingula, Limihagati, Makolo, Makune, MwanaDerefa, Mfaume, Maige na wengineo waliofuata miaka ya karibuni hata sasa hivi!!
Heri yao watu wa Kahama ambao walikuwa na Lembeli na mbunge wao wa sasa hivi ambaye anasikika; sisi wana-Shy (Mjini, Kishapu na Solwa), hatujapata mtu sahihi wa kutuletea mabadiliko; ndio maana Shy yetu imebaki kuwa dull, tunawatumbulia macho wana-Kahama tu.🙄🙄
 
Back
Top Bottom