TANZIA Augustino Mrema, Mwenyekiti wa chama cha TLP afariki dunia

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Mwenyekiti wa chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki duninia leo Jumapili 21 August 2022, saa 12.15 asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam. Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo mkoani Kilimanjaro.

Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia 16 August 2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo. Enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

PIA, SOMA:

- Augustine Mrema-Gwiji wa siasa za Upinzani za Tanzania wa wakati wote

- Augustine Lyatonga Mrema: Jinsi alivyohama CCM na kwenda NCCR-Mageuzi mwaka 1995


1661060768203.png

Augustino Mrema ni mwanasiasa wa Tanzania aliyezaliwa tarehe 31 Desemba 1944 na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania. Alibadilisha uanachama wa chama Februari 1995 na kujiunga na NCCR-Mageuzi na baadaye akabadilika tena na kuwa Tanzania Labour Party (TLP) ambako aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa chama. Aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo mara kadhaa kabla ya kushindwa katika uchaguzi wa kitaifa na James Mbatia wa NCCR MAGEUZI mwaka 2015. Kisha akachaguliwa na Rais John Joseph Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Tanzania mwaka 2016.

Augustino Mrema ni wa pili kati ya ndugu watano na ni wa kabila la Wachaga wa kijiji cha Kiraracha karibu na mlima Kilimanjaro. Augustino Mrema alisoma shule ya msingi na sekondari mjini Moshi mwaka 1955 hadi 1963, kisha akajiunga na Chuo cha Ualimu cha Mtakatifu Patrick ambako alimaliza elimu yake ya sekondari mwaka 1965. Augustino Mrema aliendelea kuandika mitihani ya Chuo Kikuu cha Cambridge O-level mwaka 1968 kisha akaendelea na masomo, kujiunga na Chuo cha Elimu ya Siasa, Kivukoni. Baadaye alienda Marangu kuendeleza masomo yake.

Augustino Mrema Nafasi Serikalini

Augustino Mrema ameshika nyadhifa kadhaa katika Serikali ya Tanzania, Shirika la Usalama wa Taifa na chama cha CCM tangu mwaka 1966; nafasi 5 alizoshika ni pamoja na zifuatazo:
  1. Mwalimu wa Uraia Vijijini 1974-1980
  2. Mwalimu katika Chuo cha Usalama cha Taifa 1980-1982
  3. Naibu Msaidizi wa Usalama wa Taifa katika Mkoa wa Dodoma 1982-1984
  4. Naibu Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Dodoma 1983-1984
  5. Naibu Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Shinyanga 1985-1987
Augustino Mrema Kisiasa

Ingawa Augustino Mrema alikuwa akigombea urais nchini Tanzania tangu jimbo hilo lilipoanzisha demokrasia ya vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990, maisha yake ya kisiasa yalianza mwaka 1985 alipogombea ubunge katika jimbo alilozaliwa la Kilimanjaro. Ugombea wake ulizuiwa na Mahakama ya Juu, hata hivyo, baada ya mchakato mrefu wa kukata rufaa, alitangazwa rasmi kuwa mshindi mwaka wa 1987. Alifanikiwa kushika kiti chake mwaka 1990 bila ushindani mkubwa. Kuwa Mbunge kulimruhusu Rais kumteua katika nyadhifa mbalimbali za Baraza la Mawaziri. Kuanzia 1990 hadi 1995 Mrema alishika nyadhifa mbalimbali za Baraza la Mawaziri na za juu serikalini:
  1. Waziri wa Mambo ya Ndani 1990-1994
  2. Waziri wa Kazi, Maendeleo na Michezo 1994-1995
Mwaka 1995 Augustino Mrema alihama CCM na kujiunga na Mkutano Mkuu wa Taifa wa Ujenzi na Mageuzi-Mageuzi ambacho kilikuwa chama kipya wakati huo. Katika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, alisimama kama rais wa NCCR-Mageuzi ambayo ilikuwa ni muungano kati ya Mkutano Mkuu wa Taifa wa Ujenzi na Chama cha Mageuzi-Mageuzi, alifanikiwa kupata asilimia 27.77 ya kura zote akishika nafasi ya tatu baada ya wakati huo aliyekuwa Rais Benjamin Mkapa aliyekuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Ibrahim Lipumba aliyesimama kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).

Katika uchaguzi uliofuata alisimama kwa tiketi ya TLP na kupata asilimia 7.80 ya kura zote. Katika uchaguzi wa Desemba 14, 2005 alichaguliwa tena kuwa rais wa TLP na kumaliza wa nne na kupata 0.75% ya kura. Hayati Magufuli alimteua kushika wadhifa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole kuanzia 2016 hadi 2019.

Mrema anajutia nini kwenye maisha yake ya siasa?
"Sikufanya hesabu zangu sawa sawa wakati nikitoka CCM kwenda NCCR. Ningejitahidi walau kuondoka na vigogo walau watano hivikutoka katika chama hicho. Labda na viongozi wa chama wa mikoa na hata mabalozi.

"Sasa mimi niliondoka mwenyewe. Peke yangu. Nilipoona umati wa watu unajaa katika mikutano yangu ya hadhara na wanawake wanatandika khanga kila ninapopita, nikajua nimemaliza kazi". Mrema
 
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema (77) amefariki Dunia, leo Jumapili, Agosti 21, 2022, saa 12.15 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa Desemba 31, 1944, Vunjo Mkoani Kilimanjaro.

Msemaji wa MNH, Aminieli Eligaisha amesema Mrema alilazwa hospitalini hapo kuanzia Agosti 16,2022 na kufikwa na mauti asubuhi ya leo.

Enzi za uhai wake, mwanasiasa huyo aliwahi kuwa mgombea urais kupitia NCCR-Mageuzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi amefikwa na mauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

Mwananchi
 
Rip

Nakumbuka 1994 ulikataa kujiunga Chadema ili ugombee Urais ukasema hutaki Chadema kionekane kuwa Chama Cha Wachagga na ukajiunga na Nccr Mageuzi

Wewe ndio umewaibua Wanasiasa mashuhuri kama Tundu Lisu, Mchungaji Msigwa na Godbless Lema

Mungu wa mbinguni amrehemu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom