Makosa ya Mwalimu Nyerere ya kushindwa kutupatia katiba bora inalighalimu Taifa

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
CCM INAMTAFUTA MCHAWI.
Ukisikiliza hotuba ya Rais wakati akipokea Report ya CAG unaona CCM ilivyochoka akili mpaka Mh.Rais anataka kulia machozi kabla ya kutafakali kauli Rais Samia kwanza turudi kwa Mwl.Julius Kambarage Nyerere kama kiongozi aliyekandamiza demokrasia kutokana na uamuzi wa Serikali yake wa mwaka 1965 wa kufuta mfumo wa vyama vingi iliourithi kutoka kwa wakoloni. Mbali na kufuta Demokrasia ya vyama vingi wanasiasa walioonekana kuwa na mitazamo tofauti kisiasa na Serikali aliyoiongoza walikumbana na wakatu mgumu sana katika kipindi chote ambacho nchi ilifuata siasa za chama kimoja ukiachilia mbali aliyekuwa rafiki yake na Katibu mkuu wa chama wakati ule Oscar Kambona alichukizwa na vitendo vya Mwalimu Nyerere kuendesha chama kibabe bili kushirikisha kamati kuu uku akisisitiza maamuzi ya Mwalimu kupitia kamati ili kuyatathmini na kuondoa athari kwa jamii lakini Mwalimu Nyerere hakutaka mawazo yake yajadiliwe na yeyote. Kuna waliompinga hadharani kama kina James Mapalala, Mwinyijuma Othman Upindo na wengine wengi ambao walidai kurejeshwa kwa siasa za vyama vya siasa nakujikuta wakiwekwa kizuizini badae uhamishoni kwa takribani miaka minne ata wale wasomi waliokuwa wamerudi nchini walilazimika kukimbia nchi wenginebhawakurudi mpaka leo na wengine kufia nje wakiogopa kufungiwa ndani ata wasomi waliomzidi elimu kama Wahaya wa kule Kagera ambao wao walisomea nchini Uganda kutokana na mfumo wa elimu kipindi kile Uganda ulituzidi mbali kielimu. Turudi nyuma kidogo wakati wa vuguvugu la kudai UHURU Nyerere alienda Uganda kusoma digree yake ya UALIMU alipofika chuo kikuu cha Uganda Makelele alikuta pale wafukunzi waTanzania alipopoleleza akakuta ni Wahaya akaogopa maana alidhani yeye angekuwa msomi mkubwa nchini ilo likamuhumiza ata alipomaliza akawashawishi warudi Tanzania kukomboa nchi na kutumikia nchi yao wale wasomi wakampa maelekezo kwamba Wakoloni wako tayari kuachia nchi yetu kama tunarudi nchini kwetu basi nchi yetu itaongozwa kwa mfumo huu apo Nyerere akashtuka na kuamua kurudi nchi kuendelea na madai ya uhuru

Tusogee mbele kidogo--- Uhuru wa maoni ulikuwa ndani ya chama kimoja Bara na Visiwani yaani TANU bara na ASP Zanzibar na badae mwaka 1977 Chama Cha Mapinduzi (CCM)kuwa na HAKI pekee ya kufanya siasa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini jicho la pili linaweza kumuangalia Mwalimu Nyerere kuwa mwanasiasa aliyesalimu amri kutokana na Dunia ilivyokuwa ikibadilika alilazimika kubadili gia angani kishingo upande kuwa chama kimoja kisingeweza kwenda na dunia mpya iliyokumbwa na wimbi kubwa la mageuzi kuanzia barani Ulaya hadi Afrika.
Ukuta wa Berlin uliozitenganisha nchi za Ujerumani Mashariki na Magharibi uliangushwa mwaka 1989 baada ya Serikali ya Kikomunist ya Ujerumani Mashariki kuachia ngazi na kuamusha nguvu ta wananchi amba wakiukimbilia ukuta huo uliokuwa na urefu wa mail 28 na kuanza kuubomoa kwa shoka na dhana nyingine zilizopatikana miaka ile ili kupata njia kwenda Ujerumani Magharibi kuonana na wenzi wao waliokuwa wanazuiwa na ukuta na sheria za kipindi kile.

Hiyo ilikuwa ni ishara kubwa duniani ya kisiasa ambako hakujuwa na demokrasia ya Uhuru wa mawazo inayokandamizwa sasa.

Anguko la pili na funzo kwa Mwalimu Nyerere na wote waliokuwa na mawazo kama yake lilisababishwa na mageuzi (Perestroika) ndani ya chama cha Kikomunist cha umoja wa Kisoviet (CPSU) na unazi (grassnot) yaliyoanzishwa na katibu mkuu wa chama hicho Mikhai Gobacheb miaka ya themanini mwishoni na mwanzoni mwa miaka ya tisini wakati dola ilo la Kisoviet lilipoanguka na baadhi ya nchi kujitoa ndani ya Urusi na sasa wanatumia nguvu kuzirudisha uku wakua watu bila sababu na Watanzania wawili tayari wamepoteza maisha katika jitihadha za Urus kulazimisha kurudisha nchi zilizojitoa miaka ya themanini.

Ndugu msomaji hii ilikuwa ishara tosha ya kuonyesha kumalizika kwa vita baridi iliyoigawa dunia pande mbili pili kuanguka kwa dola la Urusi (sasa Russia) yaani ushindi wa Demokrasia Duniani.

Wimbi la mageuzi liliendelea kusambaa sehemu nyingine na hatimaye lijafika Afrika ambapo vyama vilivyoshiriki ukombozi na badae kuamua kufuata siasa za chama kimoja vilijikuta katika wakati mgumu na kulazimika kurejesha siasa za vyama vingi zikiwamo Zambia ambapo Rais Kenneth Kaunda aliangushwa na chama na chama cha upinzani mwaka 1991.

Wakati wimbi ilo la mageuzi likiendelea kusambaa Mwalimu Nyerere hakuwa kando na mijadala ya kuingiza siasa za ushindani chini maana alishaona upepo wa mbisho akajiandaa. Kila alipopata wasaa wa kuzungumza na makundi ya watu alijikita kwenye umuhimu wa kuwepo na mijala ya dhati kabla ya kukubali au kukataa siasa za vyama vingi uku akitahadhalisha yaliyowapata wenzake. Moja ya kauli ngumu aliyotoa Mwalimu Nyerere kuonyesha kuwa mabadiliko sasa ni lazima wala sio ombi ile aliyotoa katika mkutano mkuu wa CCM wa kumpitisha Benjamin Mkapa kuwa mgombea urais wa chama mwaka 1995 Mwalimu Nyerere alisema" Watanzania wanataka mabadiliko wasipoyaona au kuyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM",
Wengi walimshangaa maana waliwaza karibu kuliko yeye aliendelea kusema "CCM si mama yangu ikiyumba naondoka", kauli hii iliondoa dhana ya kuondoka CCM ni usariti maana kama yeye angeondoka nani angemuita msariti? Apo hakusema ikifa alisema ikiyumba sasa tujiulize CCM imeyumba au imekufa? Jibu unalo msomaji kama utasoma kwa tafakuri.

Nyuma kidogo wakati wa Rais All Hassan Mwinyi (mzee wa rukhsa) alipoteuliwa kutetea chama chake mwaka 1990 habari za mageuzi zilishakuwa kubwa mpaka vyuoni kiujumla hapakuwa na uficho tena wakati huo Mwali Nyerere alishang'atuka Ikulu ila alibaki na uenyekiti wa chama (CCM)

16 August 1990 kwenye mkutano mkuu Mwalimu Nyerere aliwambia wajumbe wake kuwa mjadala wa mabadiliko ya kurejesha mfumo wa vyama vingi ulikuwa mkubwa ivyo wajiandae kisaikolojia kuupokea. Mwishoni mwa hotuba yake nimechukua sehemu ndogo ili niende sehemu nyingine alisema"kwakweli sifa moja ta demokrasia ya kweli ni kwamba inawapa nafasi wachache nafasi ya kisheria kujaribu kushawishi wengi waone ubora wa maoni yao, hii ndiyo njia pekee ya kuleta mawazo mapya na tabia mpya katika jamii kwa amani na utulivu. Ni demokrasia gani inayozuia wananchi kuhoji katiba yake au sheria nyingine yoyote katika nchi? Demokrasia ikichukua sura ya udikteta wenyewe utakuwa na sura gani"?

Baada ya kupitia maeneo tofauti kujifunza uku na kule sasa narudi kwenye nyakati hizi ambapo nchi inayumba mwalimu alisema CCM ikiyumba sasa nchi inayumba mafisadi wanatikisa nchi pesa zinaibiwa mbichi na kavu wananchi wanalia ukata, Wabunge wanalia, Mawaziri wanalia, Rais wa nchi analia fedha za nchi zinavyoibiwa na majitu yasiyo na huruma kila Wilaya anakopita CAG anakuta wizi wa kutisha hatua zinazochukuliwa na kuhamisha wezi akiiba Bukoba anahamishiwa Katavi akiiba Katavi anahamishiwa Nachingwea hakuna kuwajibika ni full nalalamiko mwisho wa siku Rais anaishia kutukana. Nani alikwambia wezi wanaogopa matusi? Wezi wanaogopa jera sio matusi wezi wanajua wakifungwa pesa zao zitaliwa na wengine na kuna uwezekano mkubwa wa kudhulumiwa wakitoka wakawa omba omba.
Juzi nimemsikiliza waziri wa Tamisemi akiapa kupambana na wanaokwamisha miradi ya maendeleo Bukoba yaani jamaa katunisha misuri kweli aliokuwa anahutubia %98 ni makada wa chama chake alilalama kana scania iliyoshindwa kupanda sekenke uku makada wenzake wakicheka mpaka nikajiuliza awa anaosema wanakwamisha miradi ya maendeleo walizuia Soko kuu ka Bukoba kujengwa, walizuia stendi kuu kwayairabwa kujengwa walizuia kingo za mto kanoni kujengwa walizuia barabara njia nne kujengwa yawezekana ndio wanazuia ata viwanda kujengwa Kagera yawezekana ndio wanazuia ata meli na speed bort kutoka Mwanza kuja Bukoba zinashindwa kufanya safari zake kupungunza ukali wa bei wa vifaa vya ujenzi nk. Awa ni kina nani? Je Waziri amesema bila tafiti? Kwanini mnaendelea kufumbia macho maadui wa maendeleo? Je ni makada wa Chadema? Ni kinanani ao ambao serikali inasalmu amri kwa miaka zaidi ya 60?

Waziri anasema Rais Samia kasikia kilio cha mbunge wa Bukoba mjini Je serikali ilisubiri kilio cha mbunge? Ni kweli tuna vyombo vya ulinzi na usalama? Kama vipo vinasaidiaje kuwafichua awa watu wenye uwezo wa kuitetemesha serikali? Chama tawala hakijawahi kujitokeza kutwambia awa wanaohujumu maendeleo ya Bukoba ni kinanani? Nakumbuka baadavya Mbungu wa Bukoba mjini kuangua kilio kwamba anakwamishwa chama kilionyesha mashaka ya kilio cha mbunge na kudai hakina raarifa ya kukwamishwa kwa mbunge ambaye ndiye anabeba CCM.Swali dogo tu ivi Waziri naye kakurupuka kusema kuna watu wanapambana kukwamisha miradi ya maendeleo?

Ivi apo kuna uongozi wa mkoa? Apo kuna uongozi wa Wilaya? Bado mnaamini CCM ipo mbali na kuendelea kulinda waharifu wanye nia ya kumkwamisha Rais? Mnadhami Mwalimu Nyerere angekuwa hai angeendelea kubaki CCM?

Ushauri wa jumla Rais kupitia Tamisemi vunja baraza la Madiwani fukuza kabisa tena wengine wachukuliwe hatua haraka shughli zote rudisha kwa mkurugenzi mpaka uchaguzi ujao. Kwa upande wa wananchi jitafakari awa madiwani ata kama hwakuchaguliwa wote kwamaana ya uchaguzi ulivyogeuzwa uchafuzi na kupata ata wasiostahili ni muda wa kujutia na kujiandaa kupata baraza safi litakalofanya kazi bega kwa bega na serikali kuinua ustawi wa wanajimbo, mkoa na nchi kwa ujumla.

Mimi @katikabakama naungana na wote wenye mapenzi mema na Kagera na niko tayari wakati wowote kutumika bila kudai ujira, furaha yangu ni kuona Bukoba inayooendeza iliyojaa upendo na siasa safi. Nawatakia sikukuu njema nikijaliwa nitaungana nanyi kusheherekea sikukuu za Christims na Mwaka mpya.
#BukobaKwanzaVyamaBadae
 
Maneno yako mengi hakuna mtu mwenye muda wa kuyasoma zaidi ya kusoma kichwa. Sasa wewe unajiona una akili kuliko Nyerere?
 
Back
Top Bottom