Inabidi serikali ikae chini ije na mpango kabambe kama walivyofanya South Africa chini ya tume ya upatinishi iliyoongozwa na Desmond Tutu ya kusahau yaliyopita na kuanza upya bila kufikiria mabaya ya nyuma, hivyo na sisi ifike mahala watu waape kiapo cha utii na once mtu atakapofanya kosa ni kuchukuliwa hatua tu hata kama ni mwanamtandao mwenzako.
Tatizo hizi kambi za kuweka viongozi ndio zinasababisha maana kila mtu ana watu wake kuanzia ngazi ya siasa mpaka kwa watendaji hivyo hata kama mtu ataharibu inachukuliwa poa. Tufike mahala mtu ukifanya kosa hata kama ni kambi moja unachukuliwa hatua kali
maana halisi ya mtandao au makundi ni kulindana