NYARAKA: Madudu mengine ya William Mhando ndani ya TANESCO

NYARAKA: Madudu mengine ya William Mhando ndani ya TANESCO

Mimi si mnafiki, ni wakati wa Zitto sasa kubeba kwa mikono miwili maneno yake na kipima uzito; na huyu ndie anaetaka urais......

Mungu ameamuwa kutuhurumia, miaka 50 tunatawaliwa kimabavu na CCM, kama haitoshi wanatokea tena Mafisadi Janjaweed kuja kuwadanganya hasa vijana waliopata Elimu ya kukalili vyuoni mwetu na kujifanya ndio Masiah kupitia Upinzani kumbe ni bora kuongozwa na Shetani kama Lowasa ambaye ameshaiba vya kutosha.

Taratibu sasa Watanzania wataanza kuelewa bila kutafsiliwa ni kwa nini kuna Wanasiasa uchwara wanataka katiba yetu iwekwe vipengere vya kuwaruhusu wao wagombee Urais kabla ya Maturity age. Hatudanganyiki.
 
Umeshalewa Mvinyo wa Leka Dutigite sasa unategemea unaweza kuuona ufisadi wa kipenzi chako Zitto? Mmeliwa kweupee.......

Kuna siku JF Member alilalamika kuwa Mh. Zitto maelezo yake mengi huwa hayana neno 'labda', 'nadhani' na mengine kama hayo...kwa maneno mengine. Mara nyingi kila jambo analolisema anakuwa na uhakika nalo.

Kwa suala hili la Mhando, huyo JF Member malalamiko yake juu ya Mh. Zitto yana mantiki kuwa wakati mwingine Mh. Zitto anawadanganya watanzania na ulimwengu kwa ujumla.

Kitendo hiki cha Mh. Zitto kutoa kauli ambazo baadaye inagundulika sio za kweli kina mshushia hadhi kama mbunge kijana mwenye maono ya kulisaidia taifa la Tanzania kutoka kwenye hali mbaya ya kiuchumi nakadhalika. Pia kinatoa taswira mbaya juu ya uwezo wa vijana kulisaidia taifa hili.

Jambo hili la Mhando limsaidie Mh. Zitto kubadilika ili kubadilisha taswira mbaya kwa uwezo wa vijana kusaidia nchi ambayo anajitahidi kuijenga kwa kusema baadhi ya mambo ambayo siyo ya kuwasaidia watanzania (kutetea watu ambao siyo wasafi kiutendaji).
 
Tanzania kutoka si leo. Kama serikali inaingia mikataba na wawekezaji wezi kwa siri mnategemea nini huku chini. Tanzania kila kitu ni siri.
 
Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Idara yake ya Habari na Uenezi kitaibuka soon kuipongeza Bodi ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu kutokana na tuhuma mbali mbali.

Aidha, chama kitawaonya watendaji wengine wote wa taasisi za umma kutojihusisha na vitendo vilivyo kinyume na maadili ya kazi zao kwani sio sera ya chama wala ya serikali ya CCM.

Mwisho, chama kitawaomba watanzania wote kuwa watulivu wakati hatua stahiki dhidi ya "TUHUMA" hizo zikiendelea kuchukuliwa na mamlaka husika.

Idara ya Habari na Uenezi, Makao Makuu.

Halafu, UWT, UVCCM, Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, TAHLISO, na jumuiya nyingine za Chama zitatoa "press releases" kuunga mkono hatua hiyo. Kisha UVCCM wataomba kibali cha maandamano kuiunga mkono serikali halafu Jeshi la Polisi litayazuia kutokana na hali tete iliyopo nchini.

NA MCHEZO UTAKUWA UMEISHIA HAPO. Ha ha ha ha ha!
 
Ushahidi wote huo halafu Board of Directors inasema kwamba Mhando hawezi kushitakiwa kwa kuwa makosa aliyofanya ni ya kinidhamu! Makosa ya kinidhamu yako wapi hapo haya ni makosa ya kijinai tu.

Kanchi haka bwana huenda tayari kuna Memorandum of Understanding kwamba asishitakiwe kwa kuwa akishitakiwa kutakuwa na mafuriko yatakayowakumba wengi.

Hivi sheria si inaruhusu Private Prosecutors, si wajitokeze wamshitaki tu huyu Mhando ili liwalo na liwe.
 
Wabunge ambao tayari wameweka misimamo yao wazi kumtetea Mhando ni pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka. Zitto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, wakati Sendeka ni mjumbe katika Kamati ya Nishati na Madini.
Soma: Raia Mwema - Bosi wa TANESCO amtetea mkewe


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe, naye ana msimamo kuwa Mhando ameonewa na wizara inaweza kujiokoa kwa kumrejesha ofisini kisha ufanywe uchunguzi maalumu utakaoendeshwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG).
Soma:
Vita kubwa TANESCO

Kwa kweli Zitto aliyataka mwenyewe. Kwa hili naona ndiyo wamemmaliza. Labda awe na ngozi ya Lowassa.

Mkuu Sikonge: Zitto siyo mkaguzi wa Tanesco, yeye anafanya kazi kulingana na ripoti ya CAG na ndio maana aliomba CAG afanye ukaguzi maalumu.
 
Mwisho naamini zitto anasoma haya yote na kama ayupo basi wajomba shangazi wajuku wake wako humuw anasoma na kumfikishia ujumbe kwa imani kabisa naamini atachukua uamuzi mzito mgumu na wa kueleweka kama mtetezi wa wanyonge anaetafuta urais...nakutakia siasa njema.......
 
Mwananchi hujenga nchi, mwananchi huvunja nchi..........!

Kwa hili sidhani kama tutafika huko kwenye maendeleo wakati hawa mchwa wanatutafuna hivi
 
sikupaii mkuu
you mean tuanze upya tuwaache waliotuibia wandelee kuzifaidi siyo!!
what a good idea!

South Africa ilikuwa juu ya apartheid siyo wizi- tofautisha
Sio kuwaacha kabisa ila nimejaribu kuangalia katika jicho la kuyatatua haya matatizo kwanza alafu from there tujenge utamaduni wa kuwajibika once mtu anapokosea, nikalinganisha na hiyo ya South Africa though maudhui yanatofautiana ila nimeangalia kwa nchi yetu kuna issue ya watu wanaingia katika uongozi kwa makundi hivyo inakuwa ngumu kumchulia hatua mwana mtandao mwenzao anapofanya kosa (that's why nikasema kuna haja ya kukaa chini na kuelezana ukweli ili huu utamaduni ukome maana mtu anafanya kosa alafu analindwa na kama atalipuliwa anajenga chuki, najua ni ngumu ila nikafananisha na SA kama kuna uwezekano tuje na utaratibu mpya wa kwamba makundi ni kwa ajili ya kuoigiana kampeni lakini isiwe ndio sababu ya ufanye utakacho na kulindwa kisa ulikuwa bega kwa gega katika kuhakikisha mgombea wenu anaingia katika uongozi)
 
Summary ya mchezo mzima iko hivi,

Mhando atatoa kiingilio cha 10Mil,

Kisha atatafuta wateja (Tanesco) na kuwapeleka kwenye kampuni ile. Mc Donald yeye atakua akipiga mzigo hapo kuhakikisha kazi inafanyika poa, huku Partner mwenza bwana Mhando akijificha nyuma yake.

Mapato watagawana 30% Mhando, 30% Mc Donald na 40% iliyobaki inabaki kwa kampuni.

Kwa wasiomjua Mc Donald ndio aliotapeliwa au kuchunwa na muigizaji wa Bongomovie aitwae Johari mtaji wa kuanzisha kampuni ya filam ambayo anaimiliki kwa ubia na msanii mwenzie Ray ya RJ Film. Johari alitoa mtaji, Ray akatoa idea......

Huyu mnyakyusa mwenzangu Mc Donald nilikutana naye Rwanda kwenye pilika za maonyesho ya mambo yao ya Umeme.Jamaa ni Predeshee wa ukweli ,kwanza nilijiuliza maswali mengi sana kuhusu mafanikio yake ya kutisha kumbe haya ndio madudu wanayofanya.

Kweli nchi yetu inatafunwa
 
Si ndogo. Something is very wrong somewhere.....

Nahisi vyombo vya USALAMA vina incompetent heads (exception natoa Jeshini kwenye hili)

Labda vimekua vyombo vya kutumika kwa ajili ya Rais alie madarakani badala ya WANANCHI.

Ila incompetence ndo nahisi itakua inawasumbua.
 
Ushahidi wote huo halafu Board of Directors inasema kwamba Mhando hawezi kushitakiwa kwa kuwa makosa aliyofanya ni ya kinidhamu! Makosa ya kinidhamu yako wapi hapo haya ni makosa ya kijinai tu.

Kanchi haka bwana huenda tayari kuna Memorandum of Understanding kwamba asishitakiwe kwa kuwa akishitakiwa kutakuwa na mafuriko yatakayowakumba wengi.

Hivi sheria si inaruhusu Private Prosecutors, si wajitokeze wamshitaki tu huyu Mhando ili liwalo na liwe.......

Wanajua kweli kupanga maneno eti wanasema NI KOSA LA KIUADILIFU KWANI HAJAONYESHA MGONGANO WA KIMASLAI WA KAMPUNI ZILE ZA FAMILIA NA TANESCO HAIJAPATA HASARA KUTOKANA NA KOSA HILO.

Sasa hapa ni kichekesho leo wameangalia upande wa hasara hawajaangalia kama utamaduni huu ukiendelea mwisho wake nini maana kulikuwa na uwezekano wa kupata kampuni nyingine ambayo huenda ikafanya kazi Tanesco katika kiwango cha juu kuliko hao waliowachagua.

Kuna haja ya kwa watendaji wa serikali katika ngazi zote kuanzia ngazi ya kijiji mpaka serikali kuu wanapewa uzito sawa maana kuna viongozi hasa wa taasisi kubwa ambao wanakula na wanasiasa (assumption though dalili za kula pamoja zinaonekana).

Pamoja na wasiasa kwa ujumla pindi wanavyofanya makosa tunaambiwa tume inaundwa uchunguzi unafanywa na majibu yanakuja kama haya yaliyotolewa kwa Mhando.

L
akini likija kwa viongozi wa serikali katika ngazi za chini vijijini, kata au mtumishi wa halmashauri kama watakosea anatimuliwa bila kufanya uchunguzi wakati mwingine anafukuzwa mbele ya mkutano wa hadhara.

Tuache hii kasumba aliotuachia J.K ya "HAWA WEZI WA EPA SIO WA KUKURUPUKA KUWASHITAKI WANA HELA HAWA WANAWEZA KUISHITAKI SERIKALI IKITOKEA UPEPELELEZI WA KINA WA KUWATIA HATIANI HAUJAFANYIKA" (wanasahau haki huwa inapatikana kwa gharama yoyote mpeleke mtu sehemu inayohusika.

Kama akikushinda lipa gharama na ndio taasisi zetu zitajifunza kufanya upepelezi maana kuna shida hapa na SIO KUWACHUKULIA HATUA WANANCHI WA KAWAIDA KWA WIZI USIO NA USHAHIDI TENA AKIWA POLISI TAYARI ANAITWA JAMBAZI AU MWIZI wakati mahakama bado haijatoa hukumu huku watu wa level ya Mhando wao wanapewa treatment tofauti)
 
haya hao wabunge kwenye ile kamati ya nishati na madini waliotaka mhando abaki na kwamba wakawa wanamtetea na wakawa mpaka na mpango wa kutoipitisha bajeti ya wizara ya nishati na madini wako wapi? Naomba tuwataje hao wabunge hapa....we should name and shame them!!




wa kwanza wao ni zitto
shame on him..!
Shame to ccm,shame to all those hand to mouth politicians...!
Shame to us tunaoishia kulalamika miaka nenda rudi na kusahau kua vizazi vyetu vitakuja kutulaani kwa kutoichukulia hatua za makusudi hali kama hii..
 
Wengine hatujui kiingereza msaada wa ufafanuzi tafadhali
 
Kudadadeeeki jamiiforum ni zaidi ya Cnn,Bbc,Dw, idhaa ya kiswahili, idhaa ia kiarabu,idhaa ya kihaya (kama ipo)
Duh hata pierce morgan haoni ndani
 
Lakini mbona wakati Mhando bado yupo Tanesco hii issue haikuibuliwa? Inaibuliwa leo wakati ameshatimuliwa!
Alikuwa anogopwa au?

hapa kuna utata wale walioibua haya na madudu alafu wakakaa kimya ndio wa kwanza kuwajibishwa kama wanajulikama,
please "mazingira magumu kama na majibu yake ni lazima yawe magumu pia bila tunaumizana sisi wenyewe,
 
mungu ameamuwa kutuhurumia, miaka 50 tunatawaliwa kimabavu na ccm, kama haitoshi wanatokea tena mafisadi janjaweed kuja kuwadanganya hasa vijana waliopata elimu ya kukalili vyuoni mwetu na kujifanya ndio masiah kupitia upinzani kumbe ni bora kuongozwa na shetani kama lowasa ambaye ameshaiba vya kutosha.

Taratibu sasa watanzania wataanza kuelewa bila kutafsiliwa ni kwa nini kuna wanasiasa uchwara wanataka katiba yetu iwekwe vipengere vya kuwaruhusu wao wagombee urais kabla ya maturity age. Hatudanganyiki.



zitto ni mnafiki sana...!!
Ana roho mbaya sana...
 
Back
Top Bottom