Mkuu hii kaya iliyooza kuna wa kum-vet mwenzie kweli? Bila kuondoa huu mfumo tusahau kabisa maendeleo ambayo hayawezi kamwe kuletwa na akili zile zile zilizoyadunisha.
Natamani Uamsho, Ponda, na wanaharakati wengine focus yao kubwa ingekuwa kuwaunganisha watanzania wote dhidi ya upuuzi kama huu badala ya kujiangalia wao binafsi au makundi yao. Tuna safari ndefu mno.
PART II:
Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Idara yake ya Habari na Uenezi kitaibuka soon kuipongeza Bodi ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu kutokana na tuhuma mbali mbali.
Aidha, chama kitawaonya watendaji wengine wote wa taasisi za umma kutojihusisha na vitendo vilivyo kinyume na maadili ya kazi zao kwani sio sera ya chama wala ya serikali ya CCM.
Mwisho, chama kitawaomba watanzania wote kuwa watulivu wakati huu hatua stahiki dhidi ya "TUHUMA" hizo zikiendelea kuchukuliwa na mamlaka husika. Vilevile, kitawataka wanasiasa hususan wa upinzani na wanaharakati kutojitafutia umaarufu kwa kuzungumzia suala hili.
Itatolewa Leo,
Idara ya Habari na Uenezi, Makao Makuu.
Halafu, UWT, UVCCM, Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, TAHLISO, na jumuiya nyingine za Chama zitatoa "press releases" kuunga mkono hatua hiyo. Kisha UVCCM wataomba kibali cha maandamano kuiunga mkono serikali halafu Jeshi la Polisi litayazuia kutokana na hali tete iliyopo nchini.
NA MCHEZO UTAKUWA UMEISHIA HAPO. Ha ha ha ha ha!