Mkuu hii kaya iliyooza kuna wa kum-vet mwenzie kweli? Bila kuondoa huu mfumo tusahau kabisa maendeleo ambayo hayawezi kamwe kuletwa na akili zile zile zilizoyadunisha.
Natamani Uamsho, Ponda, na wanaharakati wengine focus yao kubwa ingekuwa kuwaunganisha watanzania wote dhidi ya upuuzi kama huu badala ya kujiangalia wao binafsi au makundi yao. Tuna safari ndefu mno.
PART II:
Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Idara yake ya Habari na Uenezi kitaibuka soon kuipongeza Bodi ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu kutokana na tuhuma mbali mbali.
Aidha, chama kitawaonya watendaji wengine wote wa taasisi za umma kutojihusisha na vitendo vilivyo kinyume na maadili ya kazi zao kwani sio sera ya chama wala ya serikali ya CCM.
Mwisho, chama kitawaomba watanzania wote kuwa watulivu wakati huu hatua stahiki dhidi ya "TUHUMA" hizo zikiendelea kuchukuliwa na mamlaka husika. Vilevile, kitawataka wanasiasa hususan wa upinzani na wanaharakati kutojitafutia umaarufu kwa kuzungumzia suala hili.
Itatolewa Leo,
Idara ya Habari na Uenezi, Makao Makuu.
Halafu, UWT, UVCCM, Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, TAHLISO, na jumuiya nyingine za Chama zitatoa "press releases" kuunga mkono hatua hiyo. Kisha UVCCM wataomba kibali cha maandamano kuiunga mkono serikali halafu Jeshi la Polisi litayazuia kutokana na hali tete iliyopo nchini.
NA MCHEZO UTAKUWA UMEISHIA HAPO. Ha ha ha ha ha!
Nilikuwa nikimuomba mungu awaumbue wale wote ambao wamekuwa waiihujumu nchi yetu nilifarika sana wakati ambapo hatimaye raisi alipohamua kulivunja baraza la mawaziri. Wengi mtakumbuka tanesco ilikuwa na matatizo lukuki lakini mengi yalikuwa ni yakutengenezwa migao ya umeme haikuisha ili watu wajipatie tenda za kuzalisha umeme wa dharura lakini leo namshukuru mungu amejibu kwa kiasi maombi yangu na ya wale wote waliokuwa wa kiiombea mema tanzania. Tangu ngeleja aondoke tanesco imekuwa imara na kila siku inazidi kuimarika waziri mpya ametuhakikishia kuwa hakutakuwa na mgao wa umeme. Pia amekataa kuongezwa kwa bei ya umeme na ameahidi kuanzia mwakani gharama za kuunganishiwa umeme zitapungua maradufu kwa asilia kati ya 60 na 75 nampa pongezi sana waziri muhongo. Aliwataja bungeni baadhi ya wabunge kuwa ni wala rushwa na baadhi yao walihongwa ili kuikwamisha bajeti yake hata hivyo iliundwa kamati kuchunguza tuhuma zilizotolewa na muheshimiwa waziri lakini tangu mwanzo sikuwa na imani na kamati ile kwa sababu hata spika wengi hatukuwa na imani naye. Na kweli hatimaye kamati ile imetoa report ambayo inaonyesha kuwasafisha watuhumiwa nao wameshikia bango kwamba isomwe bungeni ili waziri awaombe msamaha na kuwasafisha hata hivyo nilifurahishwa na msimamo wa waziri aliposema kamwe hawezi kuwaomba msamaha wezi. Ndugu zangu watanzania tunapaswa kuunga mkono waziri muhongo ili wale wanaomhujumu kwa kuwa maslahi yao binafsi na si watanzania yameguswa wapate kuaibika lakini pia tuzidi kumuomba mungu ili 2015 akatuinulie watu wenye moyo wa uzalendo na taifa letu ili liwezo kuokoka kutoka mikononi mwa mafisadi. AMEN