Nyalandu amtimua Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori

Nyalandu amtimua Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori

Nyalandu yuko sawa huyu prof alikuwa anakaimu bado raisi alikuwa ajamteua kwa hyo waziri ana mamlaka ya kumfukuza kazi mara moja
 
Hivi tusaidiane jamani, ni tangazo gani lilipaswa kuja mwanzo (what to come 1st):
Kutangaza majina ya 'majangiri' 40 na kiongozi wao aliyeko Arusha au kumfukuza mkurugenzi wa wanayamapori!!??

hapa ndo hadithi ya "kifaranga na yai nani alianza" inapopata maana
 
Nyalandu yuko sawa huyu prof alikuwa anakaimu bado raisi alikuwa ajamteua kwa hyo waziri ana mamlaka ya kumfukuza kazi mara moja

Ukiona mkurugenzi wa wizara anafukuzwa kiholela na kirahisi rahisi ni kutaka kudhoofisha utendaji wa watumishi wa serekali.watumishi hawa huajiriwa au huteuliwa kwa kuzingatia sheria.wakikosea wanatakiwa washughulikiwe kisheria.vinginevyo ni kutaka utumishi wa umma ufanye kazi kwa woga au kujikomba.jambo ambalo ni baya sana.itakuwa vizuri kufahamu uataratibu na mamlaka uliotumika kumfukuza mtumishi wa serekali ambaye anazo haki zake na wajibu wake.tusifurahie kufuzwa fukuzwa kwa watumishi kwa kudhani ndio ubingwa.hatutegemei kila waziri achague watu wake.utumishi serekalini uheshimike usiwe kichaka cha kujifunzia kazi,kutolea uvivu au kutafutia umaarufu.
 
Kweli inachekesha , mgonjwa anatatizo la figo, anamfanyia operesheni ya kichwa.
Subiri tuone kama atapona mtu hapo.
 
Nihukumu kwa UPUMBAVU wangu na siyo UCHAGA wangu. By the way inaelekea hujui kinachoendelea nyuma ya pazia. Jitahidi kuwa mfatiliaji wa mambo kwa kina ndipo uhukumu watu. NIMEKUSAMEHE

Pole kaka yamgu ninachokiona sipendi kukiamini kwamba ukiwa MCHAGGA basi haki zako zote kama MTANZANIA zinakwisha,na mbaya zaidi ukawa MCHAGGA , MKATOLIKI halafu ukawa mwanachama wa CDM ndiyo hautakiwi hata kuishi ,inasikitisha labda tuwaulize wanaotunanga waCHAGGA nchi yetu ni ipi?
 
Yaani umemjibu TataMadiba huko nyuma na amekuelezea vizuri tu bado unakuja Page ya tatu unaanza kuuliza kitu kilekile?

Sijui hata kwa nini nimekujibu maana nilichokifanya ni kama Chizi kanichukulia nguo zangu nikioga bwawani na mie naanza kumfukuza uchi wa Mnyama barabarani. Go rumba Meeen!!!
iweje waziri mkuu ashindwe kumtimua mkurugenzi (ref. Jailo) lakini waziri wa kawaida awe na uwezo huo? Kutakuwa kuna maelezo ya ziada

Pinda alishindwa kumtimua mkurugenzi au Katibu Mkuu wa Wizara.?

ndio haohao sababu wote wanateuliwa na RAIS

Serikali ni nini? Waziri sio serikali? Use ur brain effectively
 
KWA MANEO MENGINE UNATAKA "WAJITAJE" SIO 😛eep:
 
Nyalandu anapoteza mwelekeo wa tuhuma dhidi yake anachunguzwa na TAKUKURU kwa ufisadi. Source: Gazeti la wazalendo la leo yaani MWANAHABARI.
 
Ndiyo mana comrade Kubenea alikuwa akilipua waandishi wenzake wa hovyo. Angalia, leo hii Nyalandu ameandikwa na gazeti MWANAHABARI ana chunguzwa na TAKUKURU kwa ufisadi wengne wanataka kumpamba! Itafika hatua bora tulipue waandishi wajinga wajinga wanaotetea mafisadia!
 
Hivi tusaidiane jamani, ni tangazo gani lilipaswa kuja mwanzo (what to come 1st):
Kutangaza majina ya 'majangiri' 40 na kiongozi wao aliyeko Arusha au kumfukuza mkurugenzi wa wanayamapori!!??

Huenda anahusika ndio Maana amefukuzwa ila ili kumjengea heshima Kama kawaida ya mafisadi wameamua kutotaja uhusika wake
 
Yea right afwanye kazi sana. Kwa nini akiwa arusha sasa mabodigadi kibao si alikopa kwa hao hao majangili na akawaahidi atawapendelea kurudisha mkopo ? Lile jumba kajenga nani na siajabu sasa hizi ni pilika pilika za kuweka watu wao ktk nafasi nyeti ili waendeleze ujangili vizuri.

Si tumeambiwa majangiri maaruf wapo arusha wale 40 ambao FJ anawajua yeye tu na nyalandu ?? Mbona hamtimui pia mkurugenzi wa tanapa maana hawa tembo hawauawi kipawa au kipunguni !!!

mwacheni kijana wetu nyarandu afanye kazi tuliyo mtuma,hatutataki siasa kwenye kazi.hakuna cha profesa wala mkufunzi tena.go go nyarandu
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu, amemtimua Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa; kwa utendaji kazi mbovu na kushindwa kudhibiti vitendo vya ujangili. Amekaa kwenye nafasi hiyo kwa muda usiozidi mwaka mmoja akiwa amechukua nafasi ya Obeid Mbangwa. Hii Wizara ni mwiba wenye sumu! Hili suala lina utata. Bado tunakumbuka namna Waziri Anthony Diallo (mwaka 2006), alivyohangaika kumng'oa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Severre. Mkurugenzi huyo aligoma kwa maelezo kwamba aliteuliwa na Rais na kwa sababu hiyo Waziri hana mamlaka ya kumwondoa. Katika hili ngoja tujiridhishe kama aliyeamtimua ni Nyalandu kweli au ni Rais mwenyewe.
Ee Prof. Mbona kule lecture hall ulikuwa serious kiasi hiki halafu leo hii unatimuliwa na mtu hana hata masters? Prof. Hata tembo wa Robanda village umeshindwa kuwalinda?
 
we uko nyuma ya keyboard unajua nini kuhusu wanyamapori? labda wewe ni mmojawapo wa majangiri kwa sababu jina lako tu linaonyesha wewe ni mroho sana wa pesa na utajiri uko tayari kuiba au kuua wanyama pori wetu ili mradi tu upate pesa

Lymo achana na huyo jamaa , ukiona mtu anashambulia kabila lako kisa limeendelea na kuonyesha chuki wazi wakati wote ss ni wa Tz na fursa ziko wazi kwa wote , jua jamii yao walichagua mbadala ya elimu na kufanya kazi kwa bidii na kumtegemea Mungu
 
Ee Prof. Mbona kule lecture hall ulikuwa serious kiasi hiki halafu leo hii unatimuliwa na mtu hana hata masters? Prof. Hata tembo wa Robanda village umeshindwa kuwalinda?
Ndugu siku zote jaribu kufuatilia utagundua kuwa siasa huidhalilisha taaluma mf REDET.
 
Back
Top Bottom