Nyalandu amtimua Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori

Nyalandu amtimua Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
2,438
Reaction score
4,465
Waziri wa Maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu, amemtimua Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa; kwa utendaji kazi mbovu na kushindwa kudhibiti vitendo vya ujangili. Amekaa kwenye nafasi hiyo kwa muda usiozidi mwaka mmoja akiwa amechukua nafasi ya Obeid Mbangwa. Hii Wizara ni mwiba wenye sumu!

Hili suala lina utata. Bado tunakumbuka namna Waziri Anthony Diallo (mwaka 2006), alivyohangaika kumng'oa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Severre. Mkurugenzi huyo aligoma kwa maelezo kwamba aliteuliwa na Rais na kwa sababu hiyo Waziri hana mamlaka ya kumwondoa. Katika hili ngoja tujiridhishe kama aliyeamtimua ni Nyalandu kweli au ni Rais mwenyewe.
 
Hivi inakuwaje kuajiriwa na Serikali na ufukuzwe na Waziri?

Mbona Pinda anawagwaya wateule wengine? Au wanafukuzwa wasio na Mizizi yao Magogoni?
Waziri wa Maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu, amemtimua Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa; kwa utendaji kazi mbovu na kushindwa kudhibiti vitendo vya ujangili. Amekaa kwenye nafasi hiyo kwa muda usiozidi mwaka mmoja akiwa amechukua nafasi ya Obeid Mbangwa. Hii Wizara ni mwiba wenye sumu!
 
mwacheni kijana wetu nyarandu afanye kazi tuliyo mtuma,hatutataki siasa kwenye kazi.hakuna cha profesa wala mkufunzi tena.go go nyarandu
 
Hivi tusaidiane jamani, ni tangazo gani lilipaswa kuja mwanzo (what to come 1st):
Kutangaza majina ya 'majangiri' 40 na kiongozi wao aliyeko Arusha au kumfukuza mkurugenzi wa wanayamapori!!??
 
Ugumu wa Wizara ya Maliasili
​

Katika kipindi cha miaka minane ya Serikali ya Awamu ya Nne, Wizara ya Maliasili na Utalii imeongozwa na mawaziri sita. Alianza Anthony Diallo, Profesa Jumanne Magembe, Shamsa Mwangunga, Ezekiel Maige, Balozi Khamis Kagasheki, na sasa Lazaro Nyalandu.
Tangu mwaka 2005 makatibu wakuu waliopitia wizara hiyo ni Salehe Pamba, Blandina Nyoni, Dk. Ladslaus Komba, na Maimuna Tarishi.

Ugumu wa Wizara hiyo unathibitika pia kwenye idadi ya Wakurugenzi wa Idara ya Wanyamapori; sehemu ambayo inatajwa kuwa ni ‘nono' mno.
Tangu mwaka 2005 Rais Kikwete alipoingia madarakani, Idara hiyo imeongozwa na Emmanuel Severe, Erasmus Tarimo, Obeid Mbangwa, Profesa Alexander Songorwa (aliyetimuliwa leo), na sasa nafasi yake inakaimiwa na Sarakikya.

Idadi kubwa ya Wakurugenzi wa Idara ya Wanyamapori imekuwa ikiondoka kwenye wadhifa huo kutokana na misukosuko mingi ya kiutendaji. Itakumbukwa kuwa Severe aliingia kwenye malumbano makubwa na Waziri Diallo; akipinga kuwa waziri hakuwa na mamlaka kisheria ya kumwondoa madarakani.
Februari 11, mwaka 2013 Rais Kikwete alitengua madaraka ya Mkurugenzi wa Wanyamapori, Tarimo na kumpatia likizo akisubiri kustaafu.
Kwa mujibu wa kifungu 8(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya Mwaka 2002, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliteua Mbangwa kuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo.
Hata hivyo, Mbangwa hakudumu kwenye nafasi hiyo kwani baadaye aliachishwa kazi kutokana na kashfa ya usafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi, wakati huo akiwa mwenye dhamana na kitengo kilichohusu masuala hayo.

Rais anateua watu wengi sana mwishowe inaleta mtafaruku katika utendaji.

Waziri na mkurugenzi wote wanateuliwa na rais, waziri akitaka kumuwajibisha mkurugenzi kwa kumtimua, mkurugenzi anamwambia "I serve at the pleasure of the president, he put me here, he will be the one to take me out"

Solution.

Rais apunguziwe nafasi za watu anaowateua.
 
Manyerere Jackton Huu ni ufujaji wa mali ya serikali, imagine haki zake zote anazimantain, kuanzia salary haitashushwa hata aende Sua kufunnza
 
Last edited by a moderator:
we mchagga ficha upumbavu wako

Nihukumu kwa UPUMBAVU wangu na siyo UCHAGA wangu. By the way inaelekea hujui kinachoendelea nyuma ya pazia. Jitahidi kuwa mfatiliaji wa mambo kwa kina ndipo uhukumu watu. NIMEKUSAMEHE
 
Kazungumza ukweli rais anawajua majangili mkurugenzi afanye nini?wewe ndiye mgonjwa

mkurugenzi ndio anatakiwa awajibike kulinda wanyamapori wake, hao majangiri ndio anatakiwa awajue zaidi kupita rais. we bongolala ni mwehu
 
Nihukumu kwa UPUMBAVU wangu na siyo UCHAGA wangu. By the way inaelekea hujui kinachoendelea nyuma ya pazia. Jitahidi kuwa mfatiliaji wa mambo kwa kina ndipo uhukumu watu. NIMEKUSAMEHE

we uko nyuma ya keyboard unajua nini kuhusu wanyamapori? labda wewe ni mmojawapo wa majangiri kwa sababu jina lako tu linaonyesha wewe ni mroho sana wa pesa na utajiri uko tayari kuiba au kuua wanyama pori wetu ili mradi tu upate pesa
 
mwacheni kijana wetu nyarandu afanye kazi tuliyo mtuma,hatutataki siasa kwenye kazi.hakuna cha profesa wala mkufunzi tena.go go nyarandu

Uwezo wako wa kufikiri ukoje wewe? Hana ubavu wa kumtimua mkurugenzi huyo. Kama Nyalandu anafanya kazi kweli basi amweleze bosi wake ampe majina ya majangili.Kama vipi ajiuzuru mwenyewe. Mkurugenzi ana ubavu gani wa kupambana na kina Kinana and Company?
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, lazaro Nyalandu, amemtimua Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa; kwa utendaji kazi mbovu na kushindwa kudhibiti vitendo vya ujangili. Amekaa kwenye nafasi hiyo kwa muda usiozidi mwaka mmoja akiwa amechukua nafasi ya Obeid Mbangwa. Hii Wizara ni mwiba wenye sumu!

Hili suala lina utata. Bado tunakumbuka namna Waziri Anthony Diallo (mwaka 2006), alivyohangaika kumng'oa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Severre. Mkurugenzi huyo aligoma kwa maelezo kwamba aliteuliwa na Rais na kwa sababu hiyo Waziri hana mamlaka ya kumwondoa. Katika hili ngoja tujiridhishe kama aliyeamtimua ni Nyalandu kweli au ni Rais mwenyewe.

Hiyo idara inatkiwa wapewe WAMASAI wenyewe ndiyo wanatawalinda wanyama wao.
 
Uwezo wako wa kufikiri ukoje wewe? Hana ubavu wa kumtimua mkurugenzi huyo. Kama Nyalandu anafanya kazi kweli basi amweleze bosi wake ampe majina ya majangili.Kama vipi ajiuzuru mwenyewe. Mkurugenzi ana ubavu gani wa kupambana na kina Kinana and Company?

Hana uwezo wa kumtimua mkurugenzi? ndo ameshamfukuza hivyo sasa.
 
Back
Top Bottom