Nyalandu amtimua Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori

Nyalandu amtimua Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori

Tunafanya kazi kama sinema za Holliwood...si mchezo.
 
Rais yeye aliyajuaje majangili, alikwenda mbugani?

mkuu, huyu lyimo ni mwendawazimu, anataka kulazimisha rais awajue majangiri zaidi ya mkurugenzi wa wanyamapori, sasa huyo mkurugenzi anafanya kazi gani?
lyimo ni kiazi sana
 
Hiki ni kichekesho cha mwaka, MKURUGENZI anatakiwa afanye kazi MBUGANI ya kudhibiti MAJANGILI wanaojulikana na mh.Rais

Not kujulikana tu ila ni waliotumwa na Rais kufanya ujangili.
 
Hivi inakuwaje kuajiriwa na Serikali na ufukuzwe na Waziri?

Mbona Pinda anawagwaya wateule wengine? Au wanafukuzwa wasio na Mizizi yao Magogoni?
Serikali ni nini? Waziri sio serikali? Use ur brain effectively
 
Hivi tusaidiane jamani, ni tangazo gani lilipaswa kuja mwanzo (what to come 1st):
Kutangaza majina ya 'majangiri' 40 na kiongozi wao aliyeko Arusha au kumfukuza mkurugenzi wa wanayamapori!!??
Naona majangili 40 wangetajwa kwanza then ije hii ya kinafiki!!
 
mwacheni kijana wetu nyarandu afanye kazi tuliyo mtuma,hatutataki siasa kwenye kazi.hakuna cha profesa wala mkufunzi tena.go go nyarandu

Tena afanye restruction kwenye hiyo Idara atakuta vilaza na vyeo vya chupi kibao, watu kama hawa ndio wanaharibu sura na hadhii maliasili ya taifa letu Tanzania maana hawana taaluma au ufanisi juu ya idara hii ila wanajiegesha kwa ukuta wa hongo hiyo chafuu!!
 
Naona majangili 40 wangetajwa kwanza then ije hii ya kinafiki!!
Mkuu sio swala la kuwataja tu bali kuwakamata weka behind bars na sheria ikachukua mkondo wake,bila shaka rais alipotamka tayari alikuwa na uhakika na kauli yake.
Labda kama ana mpango wa kuwasamehe endapo watarudisha nyara zetu kama waheshimiwa wa EPA.
 
ndio maana DAIL MAIL wanasema JK na serikali yake ndio chanzo,hapa utabadilisha watu lakini tembo wanazadi kupungua na wanyama pori wanazidi kupotea lazima maamuzi kama haya yawakumbe pia majangiri ambao JK amekiri yeye mwenyewe kuwafahamu kwa majina,alisema kuwa wapo 40,sasa kwanini asiwataje na wananchi tukashuhudia wenyewe hatua stahiki za kisheria zikichakuliwa dhidi yao?hapo ndipo wazungu wanasema JK HAYUPO SERIOUZ KABISA KWENYE SUALA LA UJANGILI
 
Kuna jamaa anaitwa Okudo yuko wizarani upande wa CITES huyo jamaa cheo cha ukurugenzi kwani yuko straight sana!
 
Hiki ni kichekesho cha mwaka, MKURUGENZI anatakiwa afanye kazi MBUGANI ya kudhibiti MAJANGILI wanaojulikana na mh.Rais

great question....

i think Nyalandu is just wiping his arse because he knows kwamba kwa system iliyopo ni ngumu sana kuzuia chochote kwasababu rais is fully entangled into the micro level issues za serikali

unaweza kukuta hata issues za OCD zinaamuliwa ikulu siku hizi

lets see what happens
 
Rais anateua watu wengi sana mwishowe inaleta mtafaruku katika utendaji.

Waziri na mkurugenzi wote wanateuliwa na rais, waziri akitaka kumuwajibisha mkurugenzi kwa kumtimua, mkurugenzi anamwambia "I serve at the pleasure of the president, he put me here, he will be the one to take me out"

Solution.

Rais apunguziwe nafasi za watu anaowateua.

Kiranga nakubaliana na wewe. Rais amerundikiwa madaraka ya uteuzi kwa nafasi nyeti kiasi cha kuathiri utendaji.Wajumbe wa bunge la katiba walifanyie kazi eneo hilo la mamlaka ya uteuzi wa rais.
 
Sasa nimeamini wanasiasa ni watu waongo sana! Zitto Zuberi Kabwe alishawakusema yuko tayari kuwataja waliolimbikiza Fedha kule Uswiss akaaa kimya! Sasa na huyu Lazaro Nyalandu naye juzi nimemsoma akisema atawataja watu 40 wanaohusika na ujangili wa Pembe za Ndovu lakini mtaona atakaa kimya! Wiki mbili tatu zilizopita Raisi wa Nchi hii Jakaya kikwete akiwa anahojiwa na kituo kimoja huko majuu alisikika akisema KUNA JAMAA MMOJA PALE ARUSHA TUNAMJUA ANAHUSIKA NA BIASHARA YA PEMBE ZA NDOVU, HALAFU AKASEMA SITAKI KUMTAJA JINA!

Eeeh Mungu tunakuomba uiokoe nchi hii!😛ray:
 
ampeleke kinana mahakama kama nguvu za kutosha
 

Ugumu wa Wizara ya Maliasili

Katika kipindi cha miaka minane ya Serikali ya Awamu ya Nne, Wizara ya Maliasili na Utalii imeongozwa na mawaziri sita. Alianza Anthony Diallo, Profesa Jumanne Magembe, Shamsa Mwangunga, Ezekiel Maige, Balozi Khamis Kagasheki, na sasa Lazaro Nyalandu.
Tangu mwaka 2005 makatibu wakuu waliopitia wizara hiyo ni Salehe Pamba, Blandina Nyoni, Dk. Ladslaus Komba, na Maimuna Tarishi.

Ugumu wa Wizara hiyo unathibitika pia kwenye idadi ya Wakurugenzi wa Idara ya Wanyamapori; sehemu ambayo inatajwa kuwa ni ‘nono’ mno.
Tangu mwaka 2005 Rais Kikwete alipoingia madarakani, Idara hiyo imeongozwa na Emmanuel Severe, Erasmus Tarimo, Obeid Mbangwa, Profesa Alexander Songorwa (aliyetimuliwa leo), na sasa nafasi yake inakaimiwa na Sarakikya.

Idadi kubwa ya Wakurugenzi wa Idara ya Wanyamapori imekuwa ikiondoka kwenye wadhifa huo kutokana na misukosuko mingi ya kiutendaji. Itakumbukwa kuwa Severe aliingia kwenye malumbano makubwa na Waziri Diallo; akipinga kuwa waziri hakuwa na mamlaka kisheria ya kumwondoa madarakani.
Februari 11, mwaka 2013 Rais Kikwete alitengua madaraka ya Mkurugenzi wa Wanyamapori, Tarimo na kumpatia likizo akisubiri kustaafu.
Kwa mujibu wa kifungu 8(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya Mwaka 2002, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii aliteua Mbangwa kuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo.
Hata hivyo, Mbangwa hakudumu kwenye nafasi hiyo kwani baadaye aliachishwa kazi kutokana na kashfa ya usafirishaji wanyamapori hai nje ya nchi, wakati huo akiwa mwenye dhamana na kitengo kilichohusu masuala hayo.


Mkuu Jacton Manyerere, Waziri hana mamlaka ya kumtimua Mkurugenzi pengine kama amemsimamisha na kujulisha Mamlaka husika iliyo mteua! Na Katibu Mkuu Kiongozi akisema huyu jamaa hana kosa lolote itakua aibu ya Waziri Nyalandu.
 
Back
Top Bottom