PreGE2025 No reforms, no election itakuwa kama UKAWA tu!

PreGE2025 No reforms, no election itakuwa kama UKAWA tu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Sawa ila watajua kabisa hawatakiwi
ivi heche ndo anaongoza ivi vichwa 🤣 🤣 , ccm ndo chama kikubwa kuliko vyote AFRIKA nzima na #10 duniani, hata tukisema vyama vyote vya upinzani viungane na tuwape wanachama kutoka ccm nusu nzima bado hamuwezi kua na kura za kutosha
 
Hadi sasa Mtandaoni yenyewe imepungua juzi ilikua kila page unakuta wamejazana ila sahivi unakuta moja moja
Unaona sasa…..

Sustained indignation [or lack thereof] ndo hiyo ninayoizungumzia.

Siuamini kabisa uwezo wa Watanzania kuweza ku sustain mpaka kieleweke.
 
huezi kua na ela ukawa unasupport movement za kihuni, tafuta ela sana
Hizo sio movement za kihuni, wahuni ni nyie mnaolazimisha kukubalika wakati hamkubaliki, wananchi wanataka nchi yao, elewa hilo. Pesa zipo tu na hazijawahi kutosha. Wewe kama unazo unafanya nini huku jukwaani
 
elewa nilicho andika hapo sijaizungumzia chadema, nimezungumzia ninaielewaje hii slogan ya NRNE

Kama kumbu kumbu zangu zipo sawa sawa..... Wewe ni mtu ulikua unahoji sana kwanini CDM inakubali kushiriki chaguzi ambazo inajua sheria zinaibana na kuwafanya watawala kuamua nani mshindi

Na walipo anzisha ukaunga mkono kwa juhudi zote
Lakini sasa ni kama UNASHANGAA as if ulikua hujui kitakachokuja kutokea

Mkuu this is a process...... tunaweza kuwa tunataka njia za matokeo ya haraka kama “wengine” waliofanikiwa lakini tukumbuke tabia za watu(tamaduni) zina akisi kwa kiasi kikubwa namna wanaweza kutimiza hili

I still trust the process
Endelea ku-trust the process Teh Hag mwisho wake tunaujua.
 
Ni kujidanganya tu ngabu, mapenzi ya Mungu huwa hayana kikwazo cha binadamu kuzuiya. Tuombe Mungu tuvuke salama kwa uhuru na haki
 
Hizo sio movement za kihuni, wahuni ni nyie mnaolazimisha kukubalika wakati hamkubaliki, wananchi wanataka nchi yao, elewa hilo. Pesa zipo tu na hazijawahi kutosha. Wewe kama unazo unafanya nini huku jukwaani
huezi kua na ela ukasupport uhuni, mtu yoyote mwenye ela anasupport development, mega infrastructure, kwahio tafuta ela sana
 
If history is any guide, this no reform, no election craze is headed down the path of doom, as did others such as UKAWA.

Watanzania hatuwezi kabisa ku sustain indignation.

Hii kampeni inaenda kufa tu kama ilivyokufa UKAWA.

Nani anaikumbuka UKAWA? Ilishasahaulika kabisa katika msamiati 🤣. Oh, na yale maandamano yao [ambayo hayakutokea] nani anayakumbuka?

Pia, wakati wa Magufuli kuna baadhi ya watu walianza kuzichoma kadi zao za CCM. Wengi wao walifanya hivyo kwenye mitandao ya kijamii.

Leo hii wako wapi hao watu? CCM ilipoteza wanachama wangapi kutokana na kadi zake kuchomwa?

Idadi kubwa sana ya Watanzania hata hawaelewi maana ya hiyo slogan ya NRNE.

Watanzania walio wengi wala hawaoni tatizo lolote lile lililopo katika uongozi wa nchi.

Wengi wao wanaamini kila kitu ni hisani ya Rais. Ujinga bado ni mwingi sana.

Vilevile, wengi hata hawajui kiini cha matatizo ni nini.

Hata wale wenye uelewa mdogo, nao wame stuck na mtu mmoja tu ambaye hata hayupo tena, kuwa yeye ndiye chanzo cha matatizo yote yaliyopo.

Naomba muikumbuke hii mada ili yakishatimia, tuje tukumbushane vizuri kwa rejea.

NRNE ni movement mfu!
Uchaguzi utakuwepo na baada ya Uchaguzi ndio mwisho wake.

Na baada ya hapo Chadomo watakuja na swaga za maandamano na kichapo watakula na maisha yanaendelea
 
Attachments

  • Screenshot_20250609_143407_Instagram.jpg
    Screenshot_20250609_143407_Instagram.jpg
    298.4 KB · Views: 7
Pls tell us, CDM inawezaje zuia vyama 18 visishiriki uchagu ukinielewesha hiyo methodology/majic mtayotumia na nikaielewa nitajiunga na hiyo NrNe. So far naona tu slogan za NRNE na process za uchaguzi zinaendekea smoooothly:CaptFailFish:
Wanaodai NRNE wameona kuna tatizo la mfumo wa uchaguzi. Je unasadiki kuwa kuna tatizo ktk mfumo wa uchaguzi?
 
If history is any guide, this no reform, no election craze is headed down the path of doom, as did others such as UKAWA.

Watanzania hatuwezi kabisa ku sustain indignation.

Hii kampeni inaenda kufa tu kama ilivyokufa UKAWA.

Nani anaikumbuka UKAWA? Ilishasahaulika kabisa katika msamiati 🤣. Oh, na yale maandamano yao [ambayo hayakutokea] nani anayakumbuka?

Pia, wakati wa Magufuli kuna baadhi ya watu walianza kuzichoma kadi zao za CCM. Wengi wao walifanya hivyo kwenye mitandao ya kijamii.

Leo hii wako wapi hao watu? CCM ilipoteza wanachama wangapi kutokana na kadi zake kuchomwa?

Idadi kubwa sana ya Watanzania hata hawaelewi maana ya hiyo slogan ya NRNE.

Watanzania walio wengi wala hawaoni tatizo lolote lile lililopo katika uongozi wa nchi.

Wengi wao wanaamini kila kitu ni hisani ya Rais. Ujinga bado ni mwingi sana.

Vilevile, wengi hata hawajui kiini cha matatizo ni nini.

Hata wale wenye uelewa mdogo, nao wame stuck na mtu mmoja tu ambaye hata hayupo tena, kuwa yeye ndiye chanzo cha matatizo yote yaliyopo.

Naomba muikumbuke hii mada ili yakishatimia, tuje tukumbushane vizuri kwa rejea.

NRNE ni movement mfu!

Hii ya CHADEMA ya kutaka mabadiliko ktk mifumo yetu ya uchaguzi ili kuruhusu chaguzi HURU, za HAKI, za WAZI na za KUAMINIKA inayochagizwa na kauli mbiu ya NO REFORMS NO ELECTION ni kali na haiwezi kurudi au kufa bila kuzaa matunda...

Moja ya sababu kuwa hii ni kaa la moto na lazima liunguze, ni hoja zinazoibeba ambazo ni za kweli, wazi na zinazomgusa na zilizokwisha kumwathiri kila mmoja wetu kiasi ambacho watu wengine tulishaachaga muda mrefu kupiga kura kwa sababu tulishaona hata ukienda kupiga kura ni kupoteza muda wako na kujisumbua bure tu kwa kuwa si sanduku la kura wala kura za wapiga kura zinazoamua nani awe kiongozi...

Ndio maana movement hii imepokelewa na wananchi kwa mikono miwili na kuungwa mkono na kila mpenda haki...

Kwa upande wa pili, wa CCM (wanaoongoza serikali) ambao ni wanufaika wa mfumo huu mbovu na wa dhuluma, wanajua fika kwamba, hii kitu ni hatari kwao, inatishia maslahi yao kisiasa na inatishia uwepo wao madarakani...

They're using any possible means to make sure that it's not going anywhere. Hata kauli yako ya "HII NI KAMA UKAWA TU" lengo lake ni hilo tu...

Lakini ukweli ni kuwa, hii si kama UKAWA. Hii ni kitu kingine kabisa kilichosukwa kikasukika. Hii ni lazima itoke na watu...
 
Back
Top Bottom