NJOMBE: Watu 61 wadai talaka ndani ya miezi 6

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Wanandoa 61 wamepeleka maombi ya talaka kwa ajili kuvunja ndoa zao katika Baraza la Kata ya Kivavi Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe kwa kipindi cha mwezi mmoja na wiki mbili kuanzia November hadi December 20 mwaka huu.

AyoTV imezungumza na Mwenyekiti wa Baraza hilo Muhimba Payovela aliyethibitisha kupokea migogoro mingi ya Wanandoa kuliko ya ardhi huku akieleza kuwa sababu kubwa ya Wanandoa wengi kudaiana talaka ni kutoaminiana na wengine kuendekeza tamaa.

“Ndoa 61 kila mmoja anataka kuvunja ndoa yake hakuna anayekuja kusema anataka kusuluhisha bali kila mmoja anasema sitaki tena ndoa” - Payovela

Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Makambako wamesema maombi ya talaka kwa Wanandoa yanachangiwa na wengi wao kutoridhika na walichonacho na baadhi ya Wanawake kutaka usawa ndani ya ndoa zao huku wengine wakitaka kuzivunja kutokana na vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa.
 
“Ndoa 61 kila mmoja anataka kuvunja ndoa yake hakuna anayekuja kusema anataka kusuluhisha bali kila mmoja anasema sitaki tena ndoa” - Payovela
Ukiona hivyo kuna ring leader mwenye ushawishi ulioshiba
 
7oreq4.jpg

Ni muda wa mabadiliko kataa ndoa mwaka 2024 ni mwaka wa mabadiliko.......

Tunza Afya na maokoto yako
 
Back
Top Bottom