JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,309
- 5,464
Mwenyekiti wa Baraza la Kata ya Kivavi, Muhimba Payovela amebainisha kuwa ni kweli kwa sasa anapokea migogoro mingi ya Wanandoa kuliko ya ardhi huku akieleza kuwa sababu kubwa ya Wanandoa wengi kudaiana Talaka ni kutoaminiana na wengine kuendekeza tamaa.
"Ndoa 61 kila mmoja anataka kuvunja ndoa yake hakuna anayekuja kusema anataka kusuluhisha ndoa ila kila mmoja anasema sitaki tena ndoa," amesema Payovela.
Baadhi ya Wananchi wa Mji wa Makambako wamesema maombi ya Talaka kwa Wanandoa yanachangiwa na wengi wao kutoridhika na walichonacho na baadhi ya Wanawake kutaka usawa ndani ya ndoa zao huku wengine ikiwa ni vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa.