Elimu ya talaka, namna ya kudai talaka, vigezo na masharti ya kuandika talaka

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,090
1,882
Habari za Leo wanajforum?
Tafadhari, naomba tupeane elimu ya talaka hapa jamvini. Elimu ya talaka ni muhimu sana lakini bado haitolewi vya kutosha, tangu nisome elimu yangu, sikuwahi kukutana na mada ya kutalikiana kwa wanandoa, huenda ni elimu ya watu wazima tu. Lakini hatuna budi kujifunza kutoka kwa wazoefu waliowahi kutoa au kupewa taraka.
Itasaidia wanandoa kujua faida na hasala za talaka. Karibuni sana

============

Dhana ya Talaka
Maana: ni utaratibu wa kuvunja mkataba wa ndoa baina ya mume na mke mbele ya mashahidi wawili kwa kuzingatia sheria ya Kiislamu.

- Talaka katika Uislamu si jambo linalopendeza bali linaruhusiwa tu pale inapobidi.
Ibn Umar (r.a) amesimulia kuwa, Mtume (s.a.w) amesema:

“Katika halali inayochukiza mbele ya Allah ni talaka” (Abu Daud)

- Hekima ya talaka ni kuwapa wawili wanaoachana fursa ya kwenda kuanzisha na kuendeleza maisha mengine ya familia kwa furaha na amani ili kufikia lengo.

Suluhu kati ya Mume na Mke Kabla ya Kutolewa Talaka

Ikitokea mume na mke wamegombana kabla ya kufikia hatua ya talaka, suluhu itafanyika kwa utaratibu ufuatao;

i. Mume na mke wafanye subra na kusuluhishana kwa kutakana radhi na kusameheana baina yao.
Rejea Qur’an (24:22), (42:40), (41:28)

ii. Mume na mke kuonyana na kukumbushana kurejea kwa Allah (s.w) na Mtume wake (s.a.w).

iii. Mume na mke watatengana kimalazi kwa kipindi kisichopungua miezi minne.

Rejea Qur’an (2:226-227)

iv. Jamaa kwa upande wa mume na mke wakutane ili kuwasuluhisha.

Rejea Qur’an (4:35)

Haki za Kutaliki
- Katika Uislamu haki ya kutaliki iko kwa mume na mke au mahakama ya Kiislam.

- Mume humtamkia au kumwandikia mkewe “nimekuacha” na mke hudai talaka.

a) Haki ya mume kutoa talaka
- Mume amepewa nafasi ya kutaliki kwani ndiye anayetoa mahari, posa na ndiye kiongozi wa familia.

b) Haki ya mke kumuacha mumewe
  • Kama tangu mwanzo, mume alikubaliana na mkewe kuwa huru kuvunja ndoa iwapo atamfanyia jambo lililo kinyume na sheria au asilolipenda.
  • Kwa msingi huu, mke atadai talaka ya “Khul’u” au kwenda kwa Kadhi.

c) Kuvunja ndoa kwa makubaliano ya mume na mke
- Ikitokea mume na mke wakaamua kuachana kwa wema kwa talaka ya
“Mubaarat” itafaa kama haitavunja sheria au kupoteza haki ya mwingine.

d) Haki ya Mahakama ya Kiislamu kuvunja ndoa
- Wakati mwingine hata bila ya makubaliano ya mume na mke, mahakama ya Kiislamu ina haki ya kuvunja ndoa. Mfano wa talaka hii ni “Li’aan”.

Aina za Talaka
Kuna aina kuu mbili za talaka

a) Talaka rejea
b) Talaka isiyo rejewa

a) Aina za Talaka Rejea
- Ni aina ya talaka inayompa mume fursa ya kumrejea mkewe baada ya kumpa talaka katika kipindi cha twahara.
i. Talaka moja

Ni aina ya talaka ambapo mume humtamkia au kumuandikia mkewe

“nimekuacha” kwa talaka moja akiwa twahara.

ii. Talaka mbili
Ni aina ya talaka ambapo mume humuacha mara ya pili baada ya kumuacha kwa talaka moja kisha akamrejea katika twahara mbili tofauti.
Rejea Qur’an (2:229)

iii. Talaka ya ‘Ilaa
Ni aina ya talaka ambapo mume humtenga mkewe kwa zaidi ya miezi mine.

Rejea Qur’an (2:226)

iv. Talaka ya Zihaar
Ni aina ya talaka ambapo mume humsusa mkewe kwa kumfananisha na mama yake mzazi au maharim wake.
Kama hatatubia kabla ya kuisha miezi minne, mkewe atakuwa ameachika.

Rejea Qur’an (58:3-4)

v. Talaka ya Khul’u
Hii hupatikana kwa mke kudai talaka au kujivua katika ndoa kutokana na makubaliano tangu mwanzo katika mkataba wa ndoa.

Mke anayedai talaka, atalazimika kumrejeshea mume mahari aliyompa ili ajikomboe.
Rejea Qur’an (2:229)

vi. Talaka ya Mubaarat
Ni aina ya talaka ambapo mume na mke hukubaliana kuachana kwa wema baada ya kutofikia lengo la ndoa.

vii. Talaka kabla ya Jimai
Ni kuvunja mkataba wa ndoa kabla ya kufanya tendo la jimai (ndoa).

Talaka hii ina taratibu zifuatazo;
- Hapana kukaa eda kwa mwanamke aliyeachwa kabla ya tendoa la jimai.

- Kama mume ndiye aliyemuacha na ameshatoa mahari, hatadai chochote.

  • Mume atalazimika kumpa mkewe kitoka nyumba kama ndiye aliyeamua kumuacha.
  • Ikiwa mume alikuwa hajatoa mahari, atalazimika kutoa nusu ya mahari.

- Kama mke ndiye aliyedai talaka atamrudishia mumewe mahari aliyompa

Rejea Qur’an (2:236-237)

b) Aina ya Talaka Zisizorejewa
- Ni aina ya isiyompa mume fursa ya kumrejea mkewe baada ya kumuacha kwa talaka mbili ila mpaka aolewe na mume mwingine kisha aachike kisheria.
i. Talaka tatu (Tahliil)

Ni talaka ambayo mume humuacha mkewe baada ya kumrejea kutoka talaka mbili alizomuacha na kumrejea hapo awali.
Rejea Qur’an (2:230), (65:1)

ii. Talaka ya Li’aan
Ni talaka inayopatikana baada ya mume au mke kumshika ugoni mwenzake bila ya kuwa na mashahidi wanne.

Kila mmoja ataishuhudilia nafsi yake kwa kula kiapo mara tano mbele ya kadhi na baada ya hapo ndoa itavunjika na kutorejeana tena.
Rejea Qur’an (24:6-9)

Taratibu na Sharti za Kutaliki Kiislamu
i. Talaka hutolewa kwa matamshi au maandishi kuwa “nimekuacha” au maneno yenye maana mfano wake.

ii. Talaka itamkwe au itolewe mke akiwa katika kipindi cha twahara na wasiwe wamefanywa tendo la ndoa ndani ya twahara hiyo.

iii. Utoaji wa talaka ushuhudiwe na mashahidi wawili waadilifu.

iv. Mke aliyetalikiwa hukaa nyumbani kwa mumewe mpaka eda iishe ambapo hutengana tu kimalazi.

v. Kama mume na mke wataamua kurejeana kabla ya eda kwisha, watarejeana kwa wema kwa kumuahidi Allah (s.w) kuwa wataishi kwa wema.

vi. Baada ya eda kwisha, mume na mke watalazimika kuachana kwa wema kama anavyoamrisha Allah (s.w).

vii. Si halali kwa mume aliyetoa talaka kuchukua au kudai chochote katika vile alivyompa mkewe.

viii. Mume aliyemuacha mkewe, analazimika kumpa mtaliki wake kitoka nyumba.

Rejea Qur’an (2:236)

ix. Mke aliyeomba talaka anawajibika kujikomboa kwa kumrudishia mtalaka wake mahari aliyompa, na mume akisamehe hapana ubaya.
 
Talaka ni haki aliyonayo kila mwanandoa. Kama ilivyo haki ya kufunga ndoa ndivyo ilivyo haki ya talaka pia. Yeyote kati ya wenye ndoa anaweza kuomba talaka. Awe mwanamke au mwanaume. Lakini hii ni katika sura ya 29 ya Sheria ya ndoa na si katika imani ya dini yoyote.

1.TALAKA NI NINI.

Talaka ni amri /tamko maalum la mahakama linalotamka kuhusu kuvunjika kwa ndoa. Hii ndio maana ya talaka lakini kwa mujibu wa sheria.
Katika maana hiyo twapata kujua kuwa talaka ni lazima itolewe na mahakama.

Mahakama ndicho chombo chenye dhamana kuu katika kubatilisha ndoa kwa namna ya talaka.

2. JE UNAWEZA KUOMBA TALAKA MUDA GANI BAADA YA KUFUNGA NDOA.

Ili uweze kuomba talaka ni lazima ndoa itimize miaka iwili . Huwezi kufunga ndoa mwezi huu halafu mwezi ujao ukakimbilia mahakamani ukitaka talaka. Ndoa ikifikisha miaka miwili basi haki ya talaka inafunguka.

3. TOFAUTI YA KUTENGANA NA TALAKA.

Sio kila kuachana ni talaka. Aina nyingine za kuachana zina sifa za kutengana na sio talaka. Kutengana ni hatua ambapo wanandoa wanaacha kuishi chini ya paa au dari moja. Wanaweza kuishi nyumba moja lakini vyumba tofauti.Halikadhalika wanaweza kuishi nyumba tofauti na hata pakawa mbali ya nchi kwa nchi, mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya,kijiji kwa kijiji n.k.

Tofauti kubwa kati ya talaka na kutengana ni kuwa katika talaka kunakuwa na tamko maalum kutoka mamlaka maalum linalositisha mahusiano ya ndoa, wakati katika kutengana hakuna tamko lolote kutoka katika mamlaka linalotangaza kuisha au kusitishwa kwa mahusiano ya ndoa.

Kutengana kupo kwa aina mbili. Kwanza ni kutengana kwa hiari ambapo wanandoa kwa hiari yao wanatengana, na pili ni kutengana kwa kuiomba mahakama kuwatenganisha. Yapo mazingira ambapo kumtenga mwenza kunaweza kuwa kugumu kutokana na mazingira kadha wa kadha na hapo ndipo unapoweza kuiomba mahakama iwatenganishe.

4. UNAPOHITAJI TALAKA FUATA HATUA HIZI.

( a ) Hatua ya kwanza kabisa kabla ya kwenda mahakamani lazima upeleke ombi lako baraza la usuluhishi wa migogoro ya ndoa. Kwa waislamu baraza hilo ni BAKWATA na wengine baraza hilo ni ustawi wa jamii . Kila makao makuu ya wilaya ustawi huu upo ukiuliza utaelekezwa.

Baraza hili litajaribu kusuluhisha na likishindwa litakuandalia fomu maalum kuhusu kushindwa kwake kusuluhisha. Fomu hiyo inaitwa fomu namba 3.

( b ) Hatua ya pili utakapokuwa umepewa fomu hiyo utatakiwa kuandaa maombi ya kisheria ya kutaka kuvunja ndoa huku ukiambatanisha hati hiyo.

Katika maombi hayo utatakiwa kuthibitisha uwepo wa ndoa halali, sababu inayokupelekea kuomba talaka, watoto mlionao kama wapo, na mali mlizonazo kama zipo. Mahakama itasikiliza na itatoa uamuzi.

5. JE NIENDE MAHAKAMA IPI KUDAI TALAKA.

Shauri la talaka ni shauri la ndoa. Na mahakama zenye mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ndoa ni Mahakama ya mwanzo, ya wilaya, ya hakimu mkazi na mahakama kuu. Unaweza kufungua shauri lako katika mahakama yoyote kati ya hizi. Isipokuwa ni lazima iwe mahakama ile iliyo katika wilaya yako na mahakama kuu iwe katika kanda yako.

SOURCE: Mwanasheria blog
 
Ahsante sana, umeshare kitu kizuri sana🙏🙏🙏🙏
 
Kuna jilani yangu hapa, ni mkiristo, ndoa yao ilikuwa na migogoro mingi japo sio mikubwa sana. Ingawaje katika migogoro yao mkewe ndo alikuwa kama kisababishi kutokana na maneno mengi na kauli za moja kwa moja kama nipe talaka, nipe talaka etc.sasa majuzo hapa wamegombana, jamaa akiwa kazin mkewe na mjomba wake wakaja na kuchukua mali zote za ndani wakaondoka ile jamaa anapigiwa simu akajibu mwache aende hadi sasa ni mwezi wa nane yameenda hivyo wana mtoto mmoja nwenye umri miaka 4.

Kisheria hapa wanapasea kufanya nini ili watengane jumla?

Nani anapaswa kwenda kuanza mchakato wa kudai au kutoa talaka na kwa muda gani maana imepita miezi nane,

Hakuna mali walizochuma pamoja ila zilizokuwepo kabla hawajaoana.
 
Talaka ni haki aliyonayo kila mwanandoa. Kama ilivyo haki ya kufunga ndoa ndivyo ilivyo haki ya talaka pia. Yeyote kati ya wenye ndoa anaweza kuomba talaka. Awe mwanamke au mwanaume. Lakini hii ni katika sura ya 29 ya Sheria ya ndoa na si katika imani ya dini yoyote.

1.TALAKA NI NINI.

Talaka ni amri /tamko maalum la mahakama linalotamka kuhusu kuvunjika kwa ndoa. Hii ndio maana ya talaka lakini kwa mujibu wa sheria.
Katika maana hiyo twapata kujua kuwa talaka ni lazima itolewe na mahakama.

Mahakama ndicho chombo chenye dhamana kuu katika kubatilisha ndoa kwa namna ya talaka.

2. JE UNAWEZA KUOMBA TALAKA MUDA GANI BAADA YA KUFUNGA NDOA.

Ili uweze kuomba talaka ni lazima ndoa itimize miaka iwili . Huwezi kufunga ndoa mwezi huu halafu mwezi ujao ukakimbilia mahakamani ukitaka talaka. Ndoa ikifikisha miaka miwili basi haki ya talaka inafunguka.

3. TOFAUTI YA KUTENGANA NA TALAKA.

Sio kila kuachana ni talaka. Aina nyingine za kuachana zina sifa za kutengana na sio talaka. Kutengana ni hatua ambapo wanandoa wanaacha kuishi chini ya paa au dari moja. Wanaweza kuishi nyumba moja lakini vyumba tofauti.Halikadhalika wanaweza kuishi nyumba tofauti na hata pakawa mbali ya nchi kwa nchi, mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya,kijiji kwa kijiji n.k.

Tofauti kubwa kati ya talaka na kutengana ni kuwa katika talaka kunakuwa na tamko maalum kutoka mamlaka maalum linalositisha mahusiano ya ndoa, wakati katika kutengana hakuna tamko lolote kutoka katika mamlaka linalotangaza kuisha au kusitishwa kwa mahusiano ya ndoa.

Kutengana kupo kwa aina mbili. Kwanza ni kutengana kwa hiari ambapo wanandoa kwa hiari yao wanatengana, na pili ni kutengana kwa kuiomba mahakama kuwatenganisha. Yapo mazingira ambapo kumtenga mwenza kunaweza kuwa kugumu kutokana na mazingira kadha wa kadha na hapo ndipo unapoweza kuiomba mahakama iwatenganishe.

4. UNAPOHITAJI TALAKA FUATA HATUA HIZI.

( a ) Hatua ya kwanza kabisa kabla ya kwenda mahakamani lazima upeleke ombi lako baraza la usuluhishi wa migogoro ya ndoa. Kwa waislamu baraza hilo ni BAKWATA na wengine baraza hilo ni ustawi wa jamii . Kila makao makuu ya wilaya ustawi huu upo ukiuliza utaelekezwa.

Baraza hili litajaribu kusuluhisha na likishindwa litakuandalia fomu maalum kuhusu kushindwa kwake kusuluhisha. Fomu hiyo inaitwa fomu namba 3.

( b ) Hatua ya pili utakapokuwa umepewa fomu hiyo utatakiwa kuandaa maombi ya kisheria ya kutaka kuvunja ndoa huku ukiambatanisha hati hiyo.

Katika maombi hayo utatakiwa kuthibitisha uwepo wa ndoa halali, sababu inayokupelekea kuomba talaka, watoto mlionao kama wapo, na mali mlizonazo kama zipo. Mahakama itasikiliza na itatoa uamuzi.

5. JE NIENDE MAHAKAMA IPI KUDAI TALAKA.

Shauri la talaka ni shauri la ndoa. Na mahakama zenye mamlaka ya kusikiliza mashauri ya ndoa ni Mahakama ya mwanzo, ya wilaya, ya hakimu mkazi na mahakama kuu. Unaweza kufungua shauri lako katika mahakama yoyote kati ya hizi. Isipokuwa ni lazima iwe mahakama ile iliyo katika wilaya yako na mahakama kuu iwe katika kanda yako.

SOURCE: Mwanasheria blog
Barikiwa sana Mkuu!
 
Back
Top Bottom