Njia pekee ya Polepole kuimarisha uongozi nchini ni kujiunga na Chadema au ACT Wazalendo kama mgombea uraisi asaidie kupata wabunge wengi wa upinzani

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
14,176
Reaction score
25,919
Huko nyuma niliwahi kupendekeza kwamba ni vema Raisi Samia ajitoe kuwa mgombea Uraisi na kumwachia Polepole apambane na Lissu, kwa sababu uwepo wa Samia katika nafasi yake unaleta migongano mikubwa ambayo pia inatishia kuanzushwa uhasama kati ya Tanzania bara na Visiwani.

Baada ya barua ya Polepole ya kujiuzulu sio raisi Polepole akawa mgombea mbadala wa Samia, na huenda hata CCM wakamvua unanachama wa CCM kwa kile watakachoita utovu wa nidhamu.

Hivyo basi, kama Polepole ana uchungu na nchi hii katika suala la uongozi, ushauri wangi ni kwamba asijiuzulu na kukaa nyumbani. Anapaswa aunge mkono juhudi zinazofanya na Chadema au ACT wazalendo kuwa na mfumo wa kuuwajibisha uongozi, hata kama uongozi huo utaendelea kuwa wa CCM, pamoja na ubovu wao. Ikiwezekana aombe kuteuliwa kuwa mgombea uraisi wa mojawapo wa vyama hivi, kukiwa na maridhiano Chadema warudishwe kwenye kushiriki uchaguzi Mkuu.

Kwa hali ya hewa ya siasa nchini na mambo yalivyo ndani ya CCM, Polepole anaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika kupata kura za watu ambao wako ndani ya CCM lakini wanakerwa sana na mambo yanayoendelea ndani ya chama hicho. Polepole anaweza kuleta "mafuriko ya watu yasiyozuiliwa kwa mikono" kama ilivyokuwa kwa Lowasa.

Ideally, kama Samia hataki kujitoa, basi tuwapambanishe Samia na Polepole kwenye kinyang'aniro cha uraisi na tuone Watanzania wataamua vipi.
 
Siku ambalo hili lidude ChiChieMu likigawanyika tukawa hata na timu 2 kubwa zenye nguvu zinazokaribiana ndo tiba ya Siasa ya nchi hii.. Hivi vyama akina ACT na wengine bado ni project zao,,,
 
Kwanini kumekuwa na wimbi kubwa sana la fikra zinazofanana na andiko hili ? Yaani mwana-CCM akinyooka au akitoka CCM anaonekana anafaa kugombea urais upinzani ?
 
Nyie watu ni washamba na mnachotwa akili kirahisi sana

Mnamshobokea huyo jamaa mwisho wa siku anakuja kuwatukana na anaendelea na CCM yake kwenye V8
Unajua nini, compaed to Samia, people think Polepole is an angel.

Hata kama Polepole hafai, sometimes you are forced to choose between two devils, and you go for the lesser devil. Angalau hawezi kuuza maliasili za Tanzania bara kwa sababu hana wajomba huko Uarabuni, that much we know.
 
Kwanini kumekuwa na wimbi kubwa sana la fikra zinazofanana na andiko hili ? Yaani mwana-CCM akinyooka au akitoka CCM anaonekana anafaa kugombea urais upinzani ?
Kumbuka maneno ya Nyerere; upinzani wa kweli utatoka CCM. Kisha kumbuka ushuhuda wa Lowasa - the only time Bunge lilikuwa na wabunge wengi wa upnzania.

Bado tu hutajifunza kitu?
 
Huko nyuma niliwahi kupendekeza kwamba ni vema Raisi Samia ajitoe kuwa mgombea Uraisi na kumwachia Polepole apambane na Lissu, kwa sababu uwepo wa Samia katika nafasi yake unaleta migongano mikubwa ambayo pia inatishia kuanzushwa uhasama kati ya Tanzania bara na Visiwani.

Baada ya barua ya Polepole ya kujiuzulu sio raisi Polepole akawa mgombea mbadala wa Samia, na huenda hata CCM wakamvua unanachama wa CCM kwa kile watakachoita utovu wa nidhamu.

Hivyo basi, kama Polepole ana uchungu na nchi hii katika suala la uongozi, ushauri wangi ni kwamba asijiuzulu na kukaa nyumbani. Anapaswa aunge mkono juhudi zinazofanya na Chadema au ACT wazalendo kuwa na mfumo wa kuuwajibisha uongozi, hata kama uongozi huo utaendelea kuwa wa CCM, pamoja na ubovu wao. Ikiwezekana aombe kuteuliwa kuwa mgombea uraisi wa mojawapo wa vyama hivi, kukiwa na maridhiano Chadema warudishwe kwenye kushiriki uchaguzi Mkuu.

Kwa hali ya hewa ya siasa nchini na mambo yalivyo ndani ya CCM, Polepole anaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika kupata kura za watu ambao wako ndani ya CCM lakini wanakerwa sana na mambo yanayoendelea ndani ya chama hicho. Polepole anaweza kuleta "mafuriko ya watu yasiyozuiliwa kwa mikono" kama ilivyokuwa kwa Lowasa.

Ideally, kama Samia hataki kujitoa, basi tuwapambanishe Samia na Polepole kwenye kinyang'aniro cha uraisi na tuone Watanzania wataamua vipi.
Kosa lililofanywa na cdm la kumpokea Lowassa halitakaa lirudiwe tena. Tumejifinza vya kutosha kwa kuokota wagombea ambao wana tamaa ya madaraka ila akili na hofu zao ni ccm. Ondoa wazo hilo, labda ACT ndio wanataka watu wa kuokoteza.
 
Mna akili finyu kweli kweli...uchaguzi 🙄 uchaguzi upo wapi ?
 
Nyie watu ni washamba na mnachotwa akili kirahisi sana

Mnamshobokea huyo jamaa mwisho wa siku anakuja kuwatukana na anaendelea na CCM yake kwenye V8
Tulishazoea kutukanwa na wana CCM wakiwa kwenye ma-V8 yao. Kila siku barabarani wanapita na ving;ora vinaimba makapuku tokeni barabarani wenye nchi tupite tunawahi ofisini au nyumbani. Sasa geni hapa ni lipi? Wengi tumeshaamua ni afadhali kutukanwa na Polepole kuliko Mwigulu au Mchengerwa!
 
Kumbuka maneno ya Nyerere; upinzani wa kweli utatoka CCM. Kisha kumbuka ushuhuda wa Lowasa - the only time Bunge lilikuwa na wabunge wengi wa upnzania.

Bado tu hutajifunza kitu?
Karne hii bado unaleta falsafa za Nyerere? Bunge lilikuwa na wapinzani wengi sio kwa ajili ya Lowassa acha upotoshaji usio na maana yoyote. Kazi kubwa ya kisiaasa ya cdm nchi nzima kuanzia 2010/15 ndio ilileta kura zile na sio huyo Lowassa.
 
Kosa lililofanywa na cdm la kumpokea Lowassa halitakaa lirudiwe tena. Tumejifinza vya kutosha kwa kuokota wagombea ambao wana tamaa ya madaraka ila akili na hofu zao ni ccm. Ondoa wazo hilo, labda ACT ndio wanataka watu wa kuokoteza.
Mkuu wewe sio mwanasiasa. Unaamini Slaa angeshinda na ilikuwa kosa kumeta Lowasa? Kumbuka pia, Lowasa hakushindwa. Muulize Prof. Tibaijuka.
 
Tulishazoea kutukanwa na wana CCM wakiwa kwenye ma-V8 yao. Kila siku barabarani wanapita na ving;ora vinaimba makapuku tokeni barabarani wenye nchi tupite tunawahi ofisini au nyumbani. Sasa geni hapa ni lipi? Wengi tumeshaamua ni afadhali kutukanwa na Polepole kuliko Mwigulu au Mchengerwa!
Sawa
 
Karne hii bado unaleta falsafa za Nyerere? Bunge lilikuwa na wapinzani wengi sio kwa ajili ya Lowassa acha upotoshaji usio na maana yoyote. Kazi kubwa ya kisiaasa ya cdm nchi nzima kuanzia 2010/15 ndio ilileta kura zile na sio huyo Lowassa.
Umeshasema falsafa, na kama huo ni mtizamo wako kuhusu falsafa, basi nenda shule kaongeze elimu. Unajua kina Hadi leo tunajifunza na tunatumia falsafa za kina Aristotle, wa 384-322 BC; kina Plato wa maelfu ya miaka iliyopita na bado ni kichocheo za falsafa za Ulaya. Sembuse Nyerere! Falsafa hazifi, watu ndio wanakufa.
 
Mkuu wewe sio mwanasiasa. Unaamini Slaa angeshinda na ilikuwa kosa kumeta Lowasa? Kumbuka pia, Lowasa hakushindwa. Muulize Prof. Tibaijuka.
Ebu acha hizo, wakati tunajiandikisha kwa hasira na kuita kitambulisho cga kura kichinjio, Lowassa alikuwa ccm. Slaa angeshinda, na hata asingeshinda bado chama kingebaki na haiba yake ya muda mrefu ya kupambana na ufisadi. Nasisitiza, katika upuuzi waliowahi kufanya cdm ni kumuokota Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais.
 
Back
Top Bottom