Mgawanyo wa mali za familia baada ya mume na mke kuachana [sehemu ya 2]

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
MGAWANYO WA MALI ZA FAMILIA BAADA YA MUME NA MKE KUACHANA.

SEHEMU YA 2

Mgawanyo wa mali za familia baada ya mume na mke kuachana unapaswa ufanyike kwa kuzingatia haki, ili kila mmoja apate kile anachostahili bila upendeleo.

Katika kupima mchango au jitihada za mume au mke juu ya upatikanaji wa mali za familia kumekuwa na mitazamo mbalimbali.

Kwenye kesi ya

ZAWADI ABDALLAH vs IBRAHIM IDDI [1981] TLR 311
Kulikuwa na Mitazamo miwili kama ifuatavyo;
(1). Lazima kuwe na mchango wa mojakwamoja wa mume au mke wa kifedha, mali au kazi katika upatikanaji wa mali husika.

•Hivyo kazi za nyumbani na malezi ya watoto havipaswi kuhesabiwa kama mchango juu ya upatikanaji wa mali husika.

=Huu ni mtazamo wa kihafidhina. Ni mtazamo wa kizamani na usioendana na mazingira au mahitaji ya sasa. Mtazamo huu sio sahihi.

(2). Sio lazima kuwe na mchango wa mojakwamoja wa kifedha, mali, au kazi katika upatikanaji wa mali husika za familia.

•Hivyo kazi za nyumbani na malezi ya watoto ni lazima kuzingatiwa na kutamburika kama mchango muhimu katika upatikanaji wa mali husika.

=Huu ni mtazamo huria. Ni mtazamo wa kisasa na unaoendana na mahitaji ya sasa. Mtazamo huu ni sahihi.

Kutokana na mtazamo huria, shughuri za nyumbani zinazofanywa na mke au mume zinatamburika mchango au jitihada za pamoja katika upatikanaji wa mali za familia.

Ndoa inapovunjika mwanandoa anayo haki juu ya mali za familia hatakama hakutoa mchango wa kifedha wa mojakwamoja juu ya upatikanaji wa mali husika.

Mume kuwa na kazi inayompatia kipato kikubwa kuliko mke au mke kuwa na kazi inayompatia kipato kikubwa kuliko mume hakupaswi kuwa sababu ya upande mwingine kukosa haki katika mgao wa mali za familia baada wawili hao kuachana.

BI HAWA MOHAMED vs ALLY SEFU [1983]TLR 32
Ni kesi ya kihistoria kuhusiana na mgao wa mali za familia.

Mahakama ya Rufani iliamua kwamba
"Kwasababu ustawi wa familia ni muhimu katika utendaji wa shughuri za kiuchumi za familia hivyo ni muhimu kuziangalia kazi za nyumbani anazofanya mke au mume kama sehemu ya mchango au jitihada juu ya upatikanaji wa mali husika."

NB: MGAO WA MALI SIO LAZIMA UWE 50%/50%
Je, unapenda kujua ni kwanini?
Inaendelea....

Prepared By
Mr George Francis
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
Contacts: 0713736006
 
MGAWANYO WA MALI ZA FAMILIA BAADA YA MUME NA MKE KUACHANA.

SEHEMU YA 3

Mgawanyo wa mali kwa wanandoa sio lazima uwe 50%/50%. Kila mtu anastahili kupata kile kilicho haki yake kupata.

Mwanandoa anapaswa kufahamu kwamba,
•Mchango hasi katika ustawi wa familia, matumizi mabaya ya fedha za miradi, biashara, ujenzi wa nyumba na kadhalika unaweza kusababisha mke au mume kujipunguzia kiwango cha mgao au hata kukosa kabisa.

MFANO:
Mume na mke walijenga pamoja nyumba mbili katika maisha yao ya ndoa arafu baadae mke akaja kuuza nyumba moja bila kumshirikisha mumewe na pesa kutumia anavyojua mwenyewe, siku wakiachana mke anaweza kukosa kabisa mgao wa nyumba iliyobaki au mali nyingine.

Mali za Wanandoa Huwekwa Katika Makundi Matatu,
(1). Mali ambazo mmoja kati ya wanandoa alikuwa nayo kabla ya kuoana.
MFANO: Mwanamke au mwanaume ameolewa au kuoa na kumkuta mwenzake tayari ana nyumba yake, gari lake au kiwanja chake.
_rejea kifungu cha 58 cha Sheria ya Ndoa.

(2). Mali ambazo zimepatikana wakati wapo kwenye ndoa.
MFANO: Baada ya kuaona mume na mke wakaanza kununua kiwanja na kuanza kujenga au kukamilisha nyumba, kununua gari au kufungua biashara.
_rejea kifungu cha 60(b) cha Sheria ya Ndoa.

(3). Mali ambazo zimepatikana kwenye ndoa lakini hazina uhusiano wa kindoa.
MFANO: Mmoja wa wanandoa kurithi au alipewa zawadi peke yake.
_rejea vifungu vya 60(a) na 61 vya Sheria ya Ndoa.

Mali ambayo mume au mke aliipata kabla ya ndoa itaendelea kuwa yakwake na haitahusika katika mgao baada ya kuachana.
MFANO: Kama ni nyumba au gari mume au mke alikuwa nayo kabla ya ndoa itaendelea kuwa yake peke yake na haitahusika katika mgao inapojitokeza.

LAKINI, mali hiyo iliyopatikana kabla ya ndoa inaweza kuinginzwa katika mgao ikiwa mambo yafuatayo yamejitokeza.
(a). Kuna mchango wowote wa kuiendeleza uliotolewa na mwenza.
MFANO: kama nyumba ilikuwa ya chumba kimoja lakini katika kipindi cha ndoa imeboreshwa na kuwa vyumba vitatu, hapo itaingizwa katika mgao na kuangalia kiwango cha mchango wa kila mmoja katika uendelezwaji huo na kila mmoja kupata haki anayostahili.

Kama hakuna uendelezwaji wowote nyumba inabaki kuwa ya mume au mke peke yake kama mmiliki na haitahusika katika mgao inapojitokeza.

(b). Mmiliki mwenyewe kuamua kwa hiayari yake kuwa mali hiyo ihusishwe kama mali ya familia.
MFANO: Mume alijenga nyumba kabla ya ndoa lakini baadae akaamua kwa hiyari yake itamburike kama mali ya familia na ihusike katika mgao.

VILEVILE, hata mali iliyopatikana katika kipindi cha ndoa lakini haina uhusiano wa kindoa inaweza kuingizwa kwenye mgao kama mali ya familia.

Hii ni endapo mali hiyo itaendelezwa na mwenza au kwa juhudi za pamoja za mume na mke.

Lakini ikiwa mali hiyo haitaendelezwa itabaki kuwa ni mali ya mrithi pekee au mpewa zawadi pekee na haitahusika katika mgao.

Mwisho tufahamu tu kwamba katika mgao wa mali za familia baada ya mume na mke kutalikiana, tunachoangalia suala sio hati ya umiliki wa mali hiyo ina jina la nani bali nani ana mchango gani juu ya upatikanaji wa mali husika.

Ahsante sana kwa kuwa nami katika mada hii muhimu. Nikuombe ufuatilie mada nyingine nyingi nilizowahi kushare na nitakazoshare kuhusiana na mambo mbalimbali katika sheria, dini na maisha kwa ujumla.

JINA: Mr George Francis
SIMU: 0713736006
BARUA PEPE: mr.georgefrancis21@gmail.com
Untitled-1.png
 
Ndoa ni jambo la kheri
mkuu asante kwa elimu.

Nina maswali kadhaa,
Kuna watu nilishawahi kusikia kwamba ipo sheria ya watu kuorodhesha mali zao kabla ya ndoa kufungwa sikumbuki kitaalamu inatwaje
Hii imekaaje hapa nchini kwetu?

Halafu wakishagawana mali bado mwanaume anaendelea na kjutunza watoto lakini mwanamke hafanyi hivyo ni kweli?
 
Nadhani unaongelea Prenuptial agreement.

Sio common sana Tanzania..ila kwa wenzetu wa Ulaya.

Hapa katika Prenuptial Agreement, kabla ya kuoana (ndoa), Wanandoa watarajiwa, huingia makubaliano ya nini/kipi kitahesabika kuwa ni mali ya pamoja na kipi kitahesabika kuwa ni mali ya binafsi.

Mfano, watarajiwa wote ni waajiriwa. Mnaingia makubaliano ya kisheria kuwa, asilimia kadhaa ya mshahara wa mwanaume ni mali ya pamoja na asilimia kadhaa ya mshahara wa mwanaume utakuwa mali ya pamoja. Asilimia zinazobaki, ni mali binafsi na hakuna mwenye haki ya kuchungulia
 
utaratibu wa mwanamke aliyepewa talaka (ndoa walifunga msikitini na cheti kipo) anayetaka kufungua madai ya mgawanyo wa mali anaanzia wapi? Nimegee hatua kwa hatua kiongozi
 
MGAWANYO WA MALI ZA FAMILIA BAADA YA MUME NA MKE KUACHANA.

SEHEMU YA 2

Mgawanyo wa mali za familia baada ya mume na mke kuachana unapaswa ufanyike kwa kuzingatia haki, ili kila mmoja apate kile anachostahili bila upendeleo.

Katika kupima mchango au jitihada za mume au mke juu ya upatikanaji wa mali za familia kumekuwa na mitazamo mbalimbali.

Kwenye kesi ya

ZAWADI ABDALLAH vs IBRAHIM IDDI [1981] TLR 311
Kulikuwa na Mitazamo miwili kama ifuatavyo;
(1). Lazima kuwe na mchango wa mojakwamoja wa mume au mke wa kifedha, mali au kazi katika upatikanaji wa mali husika.

•Hivyo kazi za nyumbani na malezi ya watoto havipaswi kuhesabiwa kama mchango juu ya upatikanaji wa mali husika.

=Huu ni mtazamo wa kihafidhina. Ni mtazamo wa kizamani na usioendana na mazingira au mahitaji ya sasa. Mtazamo huu sio sahihi.

(2). Sio lazima kuwe na mchango wa mojakwamoja wa kifedha, mali, au kazi katika upatikanaji wa mali husika za familia.

•Hivyo kazi za nyumbani na malezi ya watoto ni lazima kuzingatiwa na kutamburika kama mchango muhimu katika upatikanaji wa mali husika.

=Huu ni mtazamo huria. Ni mtazamo wa kisasa na unaoendana na mahitaji ya sasa. Mtazamo huu ni sahihi.

Kutokana na mtazamo huria, shughuri za nyumbani zinazofanywa na mke au mume zinatamburika mchango au jitihada za pamoja katika upatikanaji wa mali za familia.

Ndoa inapovunjika mwanandoa anayo haki juu ya mali za familia hatakama hakutoa mchango wa kifedha wa mojakwamoja juu ya upatikanaji wa mali husika.

Mume kuwa na kazi inayompatia kipato kikubwa kuliko mke au mke kuwa na kazi inayompatia kipato kikubwa kuliko mume hakupaswi kuwa sababu ya upande mwingine kukosa haki katika mgao wa mali za familia baada wawili hao kuachana.

BI HAWA MOHAMED vs ALLY SEFU [1983]TLR 32
Ni kesi ya kihistoria kuhusiana na mgao wa mali za familia.

Mahakama ya Rufani iliamua kwamba
"Kwasababu ustawi wa familia ni muhimu katika utendaji wa shughuri za kiuchumi za familia hivyo ni muhimu kuziangalia kazi za nyumbani anazofanya mke au mume kama sehemu ya mchango au jitihada juu ya upatikanaji wa mali husika."

NB: MGAO WA MALI SIO LAZIMA UWE 50%/50%
Je, unapenda kujua ni kwanini?
Inaendelea....

Prepared By
Mr George Francis
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
Contacts: 0713736006
Habari mujarabu kabisa hii....nitaiweka kwenye makabrasha yangu!!
 
Thank you so much
Nina kampuni kubwa tu ya kibiashara na nimeoa mke akaja kaikuta inaendelea vizuri. Family ikawa inahudumiwa Kwa kutumia hiyo kampuni yangu aliyoikuta tayari ninayo. Tumeishi ndan ya miaka mitano. Tumeachana.

Swali lang hapa. Je hapo hapo mgawanyo Mali umekaaje? Je tutagawana 50 Kwa 50? Kama ni Ndio huon hii Sheria inatuumiza sisi wanauana?
 
Back
Top Bottom