Mgawanyo wa mali za (wanandoa) familia

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
MGAWANYO WA MALI ZA FAMILIA BAADA YA MUME NA MKE KUACHANA.

SEHEMU YA 1

Kumekuwa na maswali mengi kuhusu mgawanyo wa mali za familia kwa wanandoa baada ya kuachana. Makala hii inajibu maswali yako unayojiuliza kila siku bila kupata majibu sahihi.

Hii inahusu watu wote, wale waliofunga ndoa inayotamburika au wale walioishi uchumba kama mume na mke au katika dhana ya ndoa kwa lugha ya kisheria.

Kifungu cha 114 cha Sheria ya Ndoa kimetoa mamlaka au nguvu kwa Mahakama kuamua juu ya mgawanyo wa mali za wanandoa baada ya kutalikiana.
_rejea kufungu cha 114(1) cha Sheria ya Ndoa.

Katika mgawanyo huo wa mali, kwa mujibu wa kifungu cha 114(2)(a-d) cha Sheria ya Ndoa,
Mahakama inazingatia mambo muhimu yafuatayo;
(a). Mila na desturi za jamii husika ambayo wanandoa wanatokea.
(b). Mchango wa kila mwanandoa katika upatikanaji wa mali husika.
Mfano: Mchango wa fedha, mali au kazi.
(c). Kama kuna deni lolote ambalo wanandoa walikopa au mmoja kati ya wanandoa alikopa kwa faida ya wote kama familia.
(d). Mahitaji ya watoto pamoja na mambo mengine muhimu yanayoweza kusaidia mgao kufanyika kwa haki bila upendeleo wowote.

Mali zinazohusika katika mgawanyo ni mali za familia tu.
Mali hizi ni zile zilizopatikana katika ndoa au kabla ya ndoa na mmoja kati ya wanandoa ambayo imekuja kuendelezwa na wanandoa wakiwa katika ndoa au katika maisha ya pamoja kama mke na mume.

Kuendelezwa huku kwa mali hiyo kunaweza kuwa kumefanywa na mwanadoa mwingine au kutokana na jitihada za pamoja za wanandoa husika.
_rejea kifungu cha 114(3) cha Sheria ya Ndoa.

Mali za familia zinaweza kuwa ni nyumba, vitu vya ndani, shamba, kiwanja, gari, duka au fedha na mali nyinginezo ambazo mume na mke wote wana haki juu ya mali husika.

Lakini unaweza kujiuliza, jitihada za pamoja ni nini?
au Je, kazi za nyumbani za mume au mke zinaweza kuzingatiwa kama jitihada?

Kifungu cha 114(2)(b) cha Sheria ya Ndoa, kimesema Mahakama inapaswa kuzingatia mchango wa kifedha, mali au jitihada katika upatikanaji wa mali husika inayotakiwa kugawanywa kwa wanandoa.

Unaweza kujiuliza, huu mchango unapimwa vipi?
Nini hasa kinazingatiwa ili kuhakikisha haki inatendeka?

Soma sehemu inayofuata...

Prepared By
George G Francis
Contacts: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 
Tuendelee
 
Back
Top Bottom