Njia ntakayotumia kuboresha maeneo kama Magomeni, Mburahati, Kigogo, Mabibo, Manzeshe, Kinondoni, Mwananyamala, Kijitonyama, Sinza, Ilala, Keko n.k

Njia ntakayotumia kuboresha maeneo kama Magomeni, Mburahati, Kigogo, Mabibo, Manzeshe, Kinondoni, Mwananyamala, Kijitonyama, Sinza, Ilala, Keko n.k

Dennis Robert Shughuru

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2024
Posts
4,124
Reaction score
6,141
Hayo maeneo ni sehemu ya city centre kwa hiyo yanatakiwa yaboreshwe
Zifuatazo ni njia ntakazotumia kuboresha na kuyafanya ya kisasa ntatumia njia zifuafazo
  1. Hayo maeneo yatajengwa gorofa kuanzia 5 na mpaka 100
  2. Wale wote wenye maeneo watatoa maeneo hayo na kuwapa madeveloper
  3. Madeveloper watajenga gorofa na wale wenye maeneo watapewa floor moja kwenye kila gorofa bure na wataamua nini cha kufanyia
Kwenye hayo maeneo patapimwa na kuwekewa mambo yafuatayo
  • Kutawekewa huduma za maji za 24/7
  • Barabara zote zitapigwa lami
  • Kutapigwa paving hakutakuwa na vumbi
  • Kutakuwa na public garden nyingi
  • Kutakuwa na open space
  • Kutakuwa na sport centre
  • Kutakuwa na zoning sehemu nyingine zitakuwa za biashara na makazi ya watu hakutakuwa na vurugu kama ilivyo sasa
  • Barabara kuu zitatanuliwa mfano barabara ya morogoro itakua na njia nane
  • Kutakuwa na mtandao wa fiber
  • Kutakua na zoning za bar, guest na makazi ya watu changamoto ya sasa hivi ya haya maeneo kila kitu kipo sehemu moja hapa nyumba ya mtu jirani ni bar wanayokesha usiku kucha hili swala halitakuwepo
Faida zake
  • Idadi ya makazi ya watu itaongezeka maradufu tofauti ilivyo sasa
Hayo yote yanawezekana vizuri tu

unasahau jambo moja kubwa, kwa uchumi gani wa kuyafanya yote hayo? kwa taarifa yako tu kima cha chini cha mshahara tanzagiza ni < laki 5 /mwezi (kabla ya kodi) kwa hiyo wanaolipwa mshahara wa milioni 1 dar/mwezi (kabla ya kodi) ni <5% , hiyo investment ya huko mwananyamala, manzese &co. nani atailipia? kwa uchumi gani?

wakati mwingine naamini watanzagiza wako soo out of touch na hawajui hata how poor and backward tanzagiza is …
 
Uchumi lazima uutengeneze mazingi ya kukaa
Kwa uchumi huu huu inawezekana vizuri tu

Kwa hiyo ukiwa maskini na poor ndo hutakiwa au ni kosa kutafuta njia ya kujikwamua???
Kwamba tukubali sisi ni maskini tubaki hivi hivi
 
Uchumi lazima uutengeneze mazingi ya kukaa
Kwa uchumi huu huu inawezekana vizuri tu

unaweka cart before a horse wanasema wazungu au tela mbele ya punda badala ya punda mbele ya tela, mazingira mazuri ya kuishi ni lazima yalipiwe na ili wananchi waweze kulipia ni lazima wawe na kazi yenye kipato cha kuwawezesha kulipia.

sasa kipato kidogo hayo mazingira nani atalipia, usisahahu siyo majengo tu kuna gharama nyingine ambazo zinaendana na majengo kuna bili za umeme, maji, takataka, sijaongelea repair n.k.

haya mambo huja automatic kama wananchi wakiwa na kipato cha kutosha, kuna sababu kwa nini hayo maendeo yako hivyo jinsi yalivyo …
 
Unavyosikia maeneo ambayo ni City centre basi maeneo yafutayo;-magomeni, mburahati, kigogo, mabibo, manzeshe, kinondoni, mwananyamala, kijitonyama, sinza, ilala, buguruni, keko, tabata dampo na ubungo haya ni maeneo ya mjini lakin yako rafu sana na duni mno

Zifuatazo ni njia ntakazotumia kuyaboresha
  1. Maeneo hayo niliyoyataja yatapimwa upya
  2. Kutajengwa kuanzia majengo yenye urefu wa gorofa tano mpaka 100
  3. Wale wakazi watapewa gorofa moja na wengie mpaka mbili bure kama sehemu ya fidia
  4. Barabara ya morogoro road zitakuwa nane
  5. Barabara ya kigogo road zitakuwa sita
  6. Kutatengenezwa njia za treni ya umeme ili kuimarisha usafiri wa umma
Hayo maeneo yatakuwa na facility zifuatazo
  • Kutakuwa na public garden nyingi sana
  • Kutakua na sport centre
  • Kutakuwa na zoning sehemu za biashara na makazi ya watu
  • Barabara zote zitapigwa lami
  • Kutapigwa paving kote hakutakuwa na vumbi
  • Majengo yatakuwa na uniformity kama njia ya kuyapendezesha
Haya yanawezekana na Nikiwa Rais yatafanyika

unahitaji pesa ndefu sana kulipa fidia watu wa maeneo hayo. it is becoming too late, kadiri muda unavyoenda ndivyo thamani inaongezeka inawezafika kipindi serikali ikashindwa kulipa fidia value itakuwa zaidi. kumbuka kenya wanashindwa kufanya ujenzi hata wa miundombinu kwa sababu ya thamani ya ardhi. ila tungekuwa na mpunga, ni kuwaondoa wote na kupanga upya na kujenga majengo ya maana, hata TBA au NHC wakipewa wajenge nyumba za serikali tu tena zinazofanana kwa makasi kwa ubora wa kimataifa. Mungu ibariki Tanganyika.
 
Hakuna jambo rahisi ila tukiweka nia inawezekana
 
Kwamba watu wote wanaoishi hayo maeneo wanauza mkaa na genge,
Ila kwanini watanzania tunapinga mabadiliko

Kumbuka mabadiliko yanakuja na opportunity nzuri na kubwa zaidi ya zilizopo
Watu wengi wa uswahilini makazi Yao ndiyo biashara zao zilipo. Ukimuweka ghorofa ya kumi atauzaje vitumbua, samaki, visheti, ubuyu, mkaa, ndizi, duka, kusuka, library ya movie na chapati.
 
Manzeshe ndo wapi mkuu?? au ulimaanisha Manzese??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom