Nazungumzia Norway niliishi. CCTV zipo kwa sababu nyingi na siyo wizi tu. Naweza kusema bila shaka yoyote kuwa nchi kama Norway unaweza kuegesha mlango bila kufunga kwa ufunguo na ukaenda kazini na kurudi na kila kitu kikawa kiko salama. Watu hawana tabia ya wizi kama Bongo, hata simu kali kabisa ukidondosha unaweza kuipata (labda uwe na bahati mbaya iokotwe na mgeni mwizi). Magari yanalazwa nje na watu hawachomoi vioo au taa. NB: siyo kwamba hakuna wizi kabisa lakini inatokea mara chache chache hasa mateja wa madawa ya kulevya ndiyo wezi