Nitatoa zawadi ya 200,000

Nitatoa zawadi ya 200,000

Kama sio yeye, kwanini alikubali kua amezipokea na akazitoa?

Kama sio yeye kwanini alikubali kwamba anazirudisha?

Kama sio yeye kwanini amepotea kwenye namba ya simu nili mtumia?

Kama nilimtumia hiyo pesa tarehe 23 March, jaribu kuoanisha na alichokuja kuki post kwenye account yake ya facebook tarehe 26 March
Samahani kama bado utakuwa na hilo tatizo nitafute nitakupa mtu hata kama kavunja lain stapatikana ndani ya wiki moja tu
 
Samahani kama bado utakuwa na hilo tatizo nitafute nitakupa mtu hata kama kavunja lain stapatikana ndani ya wiki moja tu
Asante Mkuu.....
Nashkuru kwa ukarimu wako
 
Hongera sana Mkuu Ushimen..ndio faida ya kuleta hili suala humu..ukizingatia kuna watu wa kila aina..shukurani kwao though!
 
Nilishawahi kumtumia Tapeli mmoja hvi Pesa yangu laki 2 na 50 nilimtoa kupatana! Nikatuma hela toka mpesa kwenda Tigo pesa! Akanizungusha kama siku 2/3 hivi......baadae akapotea kabisaa!!! Iliniuma sanaa hela yangu! Nikawapigia simu VODA wkasema niwasiliane na Tigo ila wanauhakika hela atakuwa ameshaitoa

Nikawapigia simu tigo....wakasema Hela jamaa alishaitoa siku ile ile na hawawezi kunisaidia....labda niwe napiga simu kwao mara kwa mara nikielezea tatizo languu ili kama ameweka pesa watamkata!

Nikawapigia simu voda tena akapokea Dada mmoja hvi nikamuelezea akasema Suala langu analipeleka idara husika!!

Mimi nikawa nawapigia simu Tigo mara kwa mara kama walivyo niambia....Nilipiga kama mara tano ndani ya mwezi tigo wakanifungia nikawa siwezi kuwasiliana nao kisa cha kunifungia ni nimepiga simu mara nyingi kwao! Iliniuma nikarudi tena kwa voda nikawapigia simu wakasema suala lako liko idara husika!

Jamaa simu hapokei wala text hajibu.....nikaaa kama 2 wks hivi machungu yameisha nikaona text ya M-PESA Nimerudishiwa Laki 2 na 50 daaaaaaa nilifurahi sanaaaa sijui Toka Siku hiyo Tigo pesa nikaacha kutumia mimi ni MPESA tuuuuu

Ila huyo Tapeli namsaka leo Hadi kesho maana anaendelea kutapeli wengine kule kupatana
 
Hongera sana mkuu naona yeye aliumia Mara mbili yako maana Pesa inaingia anakimbia kwa wakala anaambiwa pesa imerudi na ukute alikuwa anadaiwa hela ya pango hahaah
 
Wewe hujaelewa kinachozungumzwa
Mkuu kuna jamaa hapa USHIROMBO karibu na bazizan alikuja kutoa laki 2 na ninamfahamu kabisa inaweza kuwa ni yeye, labda ungenipa maelezo hayo malipo ulikuwa unawalipa watu wa idara gani ili iwe rahisi kupata uhakika wa ninachokihisi.
 
Kama hujampata mwizi wako njoo pm nikupe details jinsi ya kumpata,naogopa kuweka details hapa kwa sababu mwizi anaweza kuwa yupo kwenye hili jukwaa
 
Back
Top Bottom