Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Kwa visingizio vya kutokwenda kanisani kila jumapili atakua keshajiongeza.. 🤣
 
There is only one answer in anything.
Hakunaga majibu mawili.

Sasa yupi atachomwa na yupi ataachwa?

Huoni braza aligundua hili akaamua kuachana na imani zotee maana kila mtu huvutia kwake?

#YNWA
Mkuu, wewe weka juhudi katika hicho unachoamini, full stop
 
Kila kitu kina chanzo hii ni universal principle haiwezi kutumika kwa baadhi ya vitu kisha vingine uviache. Unalazimisha uongo ukubalike kwa kanuni ya kipumbavu kama hii

Nipe chanzo cha allah, nani kamuumba
Nani aliyekuambia Mungu ni kitu?

Na ni nani aliyekuambia Mungu yupo ndani ya universe au principle zake zinaendana na za universe?

Mungu hajaumbwa na hana chanzo.
 
Sasa hoja ya kwamba kwenye uislamu hakuna uhuru watu wanauliwa ukibadili dini au kuwa atheist inakuaje ikiwa kumbe hicho kitu kinafanyika kwa nchi zenye kufuata sharia tu? Hizo nchi za kufuata sharia ni chache kuliko nchi ambazo hazifuati sharia na kuna waislamu wengi tu mfano Tanzania,kwahiyo hoja yangu ni kupinga madai ya kwamba et waislamu huogopa kubadili dini au kuwa atheist kwa sababu ukifanya hivyo unauliwa wakati kumbe penye kufanyika hivyo ni baadhi tu ya nchi chache.
Na swali la kwanini atheist wengi ni wakristo lilikuwa worldwide sio Tanzania tu..
Sasa ishu ya kuua wanaoacha dini ndo uislam unavyosema na nchi zinazotawaliwa na uislam ziatekeleza lakini hizi zingine ambazo hawawezi kukuua kuna visa watakufanyia either utatengwa na familia,ukoo au utaonekana Chizi au watakuita majina ya dharau au kama umeoa asiye muislam utaambiwa umeolewa(Hii nishaiona sana)...Au kama ndo unaenda kuoa wanagoma kuhudhuria harusi na wanakususa
inshort kwenye jamii ya kiislam ambayo haina uwezo(bado haijaupata) wa kukuua watafanya mbadala (na ofcoz sio wote sio familia au koo zote ila nyingi ndo huwa hivyo na tunaona sana)..
Yaani
Backlash ya muislam kuacha dini yake ni kubwa kuliko mtu wa dini yoyote ile ...Nigeria hamna Sharia lakini vipo visa vingi tu vya waislam wanaoacha dini huko kutengwa au kutishiwa maisha.
Mwaka jana morogoro jamaa aliukejeli uislam akachana Quran kuna tim ya waislam ilifunga safari kutoka dodoma kuja kummaliza ikabidi basata waingilie kati na Serikali imfiche jela.
 
Ndio nikakuambia huwa mnachanganya uislamu na muislamu.Aliyesema kuhusu Rushd ni Muislamu sio uislamu.Pia huwa mnachanganya sheria ya nchi ya kiarabu na uislamu,au nchi ya Uajemi na uislamu.
Sisi sio mafala wewe...Tambua unaongea na watu wenye akili leta Hoja za akili sio maneno ya kitoto...Sasa nani kasema nchi za kiarabu ni uislam?Haya Uislam ulishashuka chini na kukataa Rashin sio Muislam?acha kutafuta vichaka vya kitoto...Sometimes tuwe tunajadili kiungwana Bana sio kila siku unaleta vyenga vyenga mambo yaliyo wazi kabisa
 
Lazima uelewe kila kikundi chochote cha watu,wanaunda umoja wao wana katiba yao,ya kuendesha kikundi husika.Kwa mfano viko vikundi,vimeweka masharti fulani,usipoyafuata umeshajitoa uanachama,kwa mfano hujahudhuria vikao vitatu vya chama,bila maelezo yoyote ya kuridhisha,tayari uwanachama huna.Zipo dini,usipohudhuria katika nyumba zao za ibada,tayari umeshatoka katika dini hiyo,hata ukifariki hawakuziki.
Na katika uislamu una kitabu cha Qur'an na muongozo wa Mtume Muhammad,katika uislamu mtume anasema "Tofauti kati ya muislamu na asiye muislam ni SWALA",USIPOSWALI HUNA UISLAMU.
Kwahyo jana hukuenda Msikitini wewe tayari sio muislam leo umeenda umerudi kwenye uislam kesho hujaenda umetoka tena kwenye uislam kama danadana...Bana eeh em fanya kama unaongea na wasomi sio wadogo zako apo nyumbani.
Kuacha dini ni kutoamini tena katika hiyo dini
Onesha source inayosema asiyeswali swala tano kila siku siyo muislam
 
Muhammad,katika uislamu mtume anasema "Tofauti kati ya muislamu na asiye muislam ni SWALA",USIPOSWALI HUNA UISLAMU.
Basi tusiwaangalie waislam maana waislam hawaui mtu ambaye haswali... kwa maelekezo yako Turudi kuangalia kwenye Uislam.

Muhammad alisema anayeacha dini Auwawe; na kama unasema kutoswali ni kuacha dini basi ambao hawaswali wote wanatakiwa wauwawe.

Na kama hapa Tz hawauliwi inamaana waislam hawafati maagizo ya Muhammad na kama hawayafuati inamaana sio waislam...Kwahyo in conclusion Hapa Tanzania(possibly dunia nzima) Hakuna Muislam hata mmoja.
 
Nadhani sababu wakristo wapo huru zaidi kuliko Waislam.

Mkristo yupo huru kufungua kanisa lake au kuhamia kanisa jingine ama Dini

Kwa Waislam ni tofauti, ni dini ya itikadi Kali zaidi, madhehebu yao wenyewe kwa wenyewe wanapigana Vita, kufunga Ramadan wanalazimishwa, kuna nchi nyingine ukibadili dini adhabu yake ni kifo
Siyo nchi nyingine, ni sheria kwenye hiyo dini mtu ukibadili dini unatakiwa upigwe mawe hadi ufe! Too harsh!
 
Wakuu habari,

Mimi ni siamini kuhusu masuala ya dini, ila naamini binadamu tunapaswa kuishi kwa upendo kati yetu na tuwapende pia viumbe wengine, naamini hii ndio 'perfect' na 'universal dini'.

Matatizo kama vita, njaa, mauaji, talaka, pengo kati ya matajiri na masikini n.k vyote hivi tungevipunguza kwa kiasi kikubwa kama tungezingatia hii 'universal dini' zaidi kuliko nyingine

Mke wangu ni mtu wa Dini sana, ametokea familia ya walokole.

Amekuwa akinisumbua kuhusu kwenda kanisani kila mara, nimekuwa nikimpa visingizio vya hapa na pale ili nisiende naye kanisani, ila naona visingizio vimeisha.

Sasa nimechoka kelele za kuhusu kanisani, nafikiria nimchane kuwa siamini masuala yake ya kanisani na sitaki usumbufu tena.

Nitakuwa harsh sana au kuna mbadala wa kuyamaliza?
Endelea kumdanganya danganya tu
 
Naamini Allah yupo..Kaumba mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo.. Kaniumba Mimi kutoka kwenye tone la manii

Kasimamisha mbingu bila nguzo.. jua linawaka na usiku Kuna mwezi...hizo zote Ni DALILI KWA WENYE KUTAFAKARI
Kwa hiyo anga ambalo ni intangible ulitaka liwe na nguzo ambazo ni tangible ndio uamini kua sio mungu?

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
 
Nani aliyekuambia Mungu ni kitu?

Na ni nani aliyekuambia Mungu yupo ndani ya universe au principle zake zinaendana na za universe?

Mungu hajaumbwa na hana chanzo.
Hata mtu sio kitu, ila unapokuja kuanza kuelezea dhana ya kila kitu unakua hufungwi na mipaka huachi kitu una include vyote vilivyo vitu na visivyo vitu

Kokote kule ambako mawazo yenu yanafikiri mungu yupo, naweza nikajenga hoja kwa kum-refer as kitu kwa kutumia universal principle "kila kitu kina chanzo"

"Mungu hajaumbwa na hana chanzo", ebu thibitisha mungu yupo kwanza kisha huko mbeleni tutajua kama anamuumba au lah
 
Hayo yote wasema wewe peke yako,hukuyakuta ulipozaliwa ul,sio wengi wanasema hivyo.Ingekuwa hayo unayosema,yalisemwa,na wewe ukayakuta,ulipozaliwa,ndio yanakuwepo.
hili ndo tatizo lenu huwa hamtafakali kabla ya kuongea

ni kiwango kipi unachotumia kupima uzito wa madai yasio kuwa na ushahidi wowote

unasema sikuyakuta! kama vile ukikuta kitu kinasemwa basi ni sahihi au kina uzito
na zaidi ya hapo, kwanini mda kupita iwe kigezo
kwahiyo niliyoyasema ni sahihi baada ya miaka 50, 100, au 1000
kwahiyo baada ya miaka 100 kutakuwa na nyani wenye mabawa, kwasababu nilisema mie

2. kutumia umati kama kipimo
kama nikikubali hili, utapaswa uniambie ni watu wangapi wanahitajika kufanya madahi kuwa na uzito
je ni watu 100, 1000, au laki?
kama idadi ya uwatu ndo inaleta uzito wa dai, basi zingatia dai hili bila ushahidi; a> dunia ni tambale b>mungu ni ngombe c>mungu ni tembo c> mungu ni mwanamke c> watu weusi ni nyani : yote haya ni madai yanasemwa na mabillioni ya watu, zaidi ya hapo yameanza kusemwa tangu miaka ya kabla ya historia (enzi za ukoloni, sultan, na India)

HILI NDO TATIZO LENU; FIKILIENI dah...
 
Kwanza hakuna niliposema kuwa mimi nina ushahidi wa kuwepo Mungu,mimi nimekuja moja kwa moja hilo swali sasa ukianza kusema sijui sina ushahidi hiyo hoja kwangu. Nilichouliza yeyote anaweza kuuliza hata asiyeamini Mungu.

Nimesema hata mahakamani kuwa sio kila ushahidi unatambulika hata kama ni kweli ni ushahidi hivyo wana taratibu zao,sasa najaribu kuangalia sifa za huyo Mungu ndipo naujiuliza huyo mwenye kutaka ushahidi ni kitu gani anakitajia kukipata ili akubali kuwa ni ushahidi?
ki academia unacho kiongelea kinaitwa proving a negative

"Proving a negative or negative proof may refer to:
Proving a negative, in the philosophic burden of proof
Evidence of absence in general, such as evidence that there is no milk in a certain bowl
Modus tollens, a logical proof
Proof of impossibility, mathematics
Russell's teapot, an analogy: inability to disprove does not prove"

Huu ni mtego unaojulikana katika kila dicpline ya masomo
Ndo Maana hata katia mahaka wana sytem ya BURDEN OF PROOF: MDAI NDI ANA WAJIB WA KUTOA USHAHIDI
"it has been said whoever makes a claim carries the burden of proof regardless of positive or negative content in the claim"

Ni kama mimi kusema; "hakuna ushahidi unaoweza toa, kudhihilisha kwamba hakuna mbuzi mwenye mabawa ambae ahonekani"

Ndugu yangu TZ huu mtego wa fikra watu walishaujadili sana na kuugutikia

Mdai ndie atoae ushahidi; na kama awezi kufikilia iana ya ushahid, basi hana ushahidi...
 
Back
Top Bottom