Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Nitamwambiaje Mke wangu mimi ni 'Atheist'?

Bado hapo unanijadili mimi binafsi,nishasema hakuna nilipodai kuwa nina uthibitisho wa kuwepo Mungu kwahiyo usielekeze nguvu kwangu mimi binafsi.
Sasa kama hauna uthibitisho wa kuwepo mungu we umejuaje kua mungu yupo?

Na kwanini unahoji kutaka kujua specifications za uthibitisho ili utoe uthibitisho wakati huna uthibitisho?
 
Suala la familia ni swala linalohitaj umakini mkubwa hususani kwenye masuala kama yakufanya maamuzi. Tuliza kichwa chukua karatasi andika faida ya kumwambia na faida ya kutomwambia utapata jibu

kubomoa ni rahisi kuliko kujenga
 
swali lako lipo wazi lakini sio sahihi
anaedai ameoa ndio anatoa cheti cha ndoa, na yeye ndie anayechagua kutoa cheti cha ndoa kama ushahidi; jukumu ni lake na sio la mwingine
mimi kama judge, kazi yangu ni kupinga au kukubari ushahidi wake

nina sababu zangu za kukataa kukujibu swali lako; nakuelewa unachouliza; lakini najua unachofanya

mi nina ushahidi kwamba huna ushahidi wowote kuhusu kuwepo kwa mungu wako

kwani ungekuwa na ushahidi, hata kama punje, ungekuwa umesha utoa
ila unanipa hiyo kazi mimi: yani nichague ushaidi ninao utaka alafu nikuombe
NO

wewe ndo mwenye madai kwamba mungu yupo
MI NASEMA HAKUNA USHAHIDI YUPO
mi nasema nipe ushahidi wowote

NIPE PICHA
NIPE SAUTI
NPE KIPIMO
NIPE CHOCHOTE zaidi ya maneno yalioandikwa na wakoloni, wasomi wakijeudi, king james, na wengineyo

TOA USHAHIDI WOWOTE

lakini najua uwezi, kwani una zaidi ya ku-quote maandishi
ndo maana unataka mimi ndo nikufanyie kazi ya kufikilia
Kwanza hakuna niliposema kuwa mimi nina ushahidi wa kuwepo Mungu,mimi nimekuja moja kwa moja hilo swali sasa ukianza kusema sijui sina ushahidi hiyo hoja kwangu. Nilichouliza yeyote anaweza kuuliza hata asiyeamini Mungu.

Nimesema hata mahakamani kuwa sio kila ushahidi unatambulika hata kama ni kweli ni ushahidi hivyo wana taratibu zao,sasa najaribu kuangalia sifa za huyo Mungu ndipo naujiuliza huyo mwenye kutaka ushahidi ni kitu gani anakitajia kukipata ili akubali kuwa ni ushahidi?
 
Sasa kama hauna uthibitisho wa kuwepo mungu we umejuaje kua mungu yupo?

Na kwanini unahoji kutaka kujua specifications za uthibitisho ili utoe uthibitisho wakati huna uthibitisho?
Wapi niliposema nimeuliza hilo swali ili nitoe uthibitisho unaweza kunionesha?

Suala la mimi kujua Mungu yupo linahusika na imani kwa hivyo linahusu sababu zenye kunifanya mimi niamini kuwa Mungu yupo,ila tofauti ni kwamba wewe unataka uthibitisho sio sababu za kuamini.
 
Mimi ukiniambia kuhusu Athiest na Ndoa inakufa HAPO
 
Wapi niliposema nimeuliza hilo swali ili nitoe uthibitisho unaweza kunionesha?
Sasa ulikua ubauliza kwa minajili ipi?

Kwanini ulikua unakomalia kupatiwa sababu ambayo hutaifanyia kazi kwa kutoa majibu ambayo waulizaji wanayataka?
Suala la mimi kujua Mungu yupo linahusika na imani kwa hivyo linahusu sababu zenye kunifanya mimi niamini kuwa Mungu yupo,ila tofauti ni kwamba wewe unataka uthibitisho sio sababu za kuamini.
Kwa maana hiyo wewe huwezi kuthibitisha nje ya imani mungu yupo?

Kwa mantiki hiyo huwezi kusema una hakika mungu yupo kwasababu upo ndani ya imani
 
Sasa ulikua ubauliza kwa minajili ipi?

Kwanini ulikua unakomalia kupatiwa sababu ambayo hutaifanyia kazi kwa kutoa majibu ambayo waulizaji wanayataka?

Kwa maana hiyo wewe huwezi kuthibitisha nje ya imani mungu yupo?

Kwa mantiki hiyo huwezi kusema una hakika mungu yupo kwasababu upo ndani ya imani
Nimeshaeleza kwanini nauliza hilo swali na tatizo badala kulijibu hilo swali kama lilivyoulizwa mnajadili msimamo au imani wa muuliza swali.

Kuwa ndani ya imani ndio kukosa uhakika? Kwa maana nyengine unataka kuniambia nina mashaka na uwepo wa Mungu?
 
Nimesema lack of belief kisha nimeishia hapo, sijatia neno lingine sasa kivipi utwist hoja yangu kwa kunilazimisha nijibu hoja ambayo mimi sijaiandika?

Hoja yangu ni kwamba kila mtu alizaliwa akiwa atheist, atheism ni lack of beliefs.

Hata aliyeanzisha dini asili yake ni atheist
Ndio nimekuuliza swali kwamba atheism ni lack of belief ila sio kwamba atheist haamini?
Yani atheist sio mtu ambaye haamini?
 
Nimeshaeleza kwanini nauliza hilo swali na tatizo badala kulijibu hilo swali kama lilivyoulizwa mnajadili msimamo au imani wa muuliza swali.
Kama unauliza kwa mantiki ambayo sio ya kutaka kuthibitisha basi hakuna umuhimu wa kukomalia upatiwe vigezo vya uthibitisho
Kuwa ndani ya imani ndio kukosa uhakika?
Yes ukiwa na imani huna uhakika
Kwa maana nyengine unataka kuniambia nina mashaka na uwepo wa Mungu?
Kama huna mashaka thibitisha mungu yupo nje ya imani
 
Dini ni mfumo wa maisha ila sio kila mfumo wa maisha ni dini...Inshort ili iwe dini lazima ihusishe imani ya vitu supernatural sasa huwezi kuwa na mfumo wa kibepari ikaitwa dini
Nini maana ya mfumo wa maisha?
 
Ndio nimekuuliza swali kwamba atheism ni lack of belief ila sio kwamba atheist haamini?
Yani atheist sio mtu ambaye haamini?
Wewe ni believer ambaye ni theist kutoka theism. Na msingi wenu ni kuamini nguvu ya supernatural power (Mungu)

So according to that brief explanation, unaweza ukasema theism ni imani ya kuwepo kwa mungu ila theist hana imani ya kuwepo kwa mungu?
 
Mimi ukiniambia kuhusu Athiest na Ndoa inakufa HAPO
Mi ukiniambia kuhusu dini nitakuuliza yafuatayo...

Imani gani?
Maana hili nalo ni somo JENGINE.

Waislamu wanaamini wao ndio sahihi na wengine wotee MOTONI (wanaofanya shiriki)

Wakristo wanakwambia usipompokea Kristo (Yoh 14:1-7) Basi wewe motoni, huendi kwenye mji ule bila kupitia Kristo Yesu?

Shiah Vs Sunni nayo ni mada nyengine bila kusahau Catholic Vs Protestants na Sabath Vs Other Christian.

Ukiniambia dini fulani ndio sahihi (Mf: kristo) mi nitakuuliza ina maana Mungu alitaka nizaliwe muislamu ili niabudu dini sio halafu anichome?

IMANI GANI NI SAHIHI NA IPI ITAENDA MOTONI?

#YNWA
 
Ambazo kila mtu kwa dini nyingine tofauti na yake ameandikwa ataenda motoni

Yani wewe muislam kwenye dini ya mkristo ni wa motoni, na mkristo kwenye mafunzo ya kiislamu ni kafiri hivyo ataenda motoni

See how it sounds?

so unamtishiaje atheist kua ataenda motoni wakati maelfu ya dini zinazopingana nayako zimekuhesabia kua ni mtu wa motoni?
Tatizo lako una pupa ya kujibu hauna pupa ya kusoma kwa kuelewa.

Binadamu si anasema hakuna Mungu na hakuteremsha muongozo wa aina yoyote! Wengine wanasema Mungu yupo ila hakuteremsha muongozo ambao unafahamika kwa jina la dini. Wengine wanasema Mungu yupo na muongozo wake ni huu! Wengine wanasema hapana muongozoz sahihi ni huu.

Nini maana ya siku ya hukumu?
Ni maana Mungu wa ukweli atafahamika ni yupi kwa sababu kila dini si ina itikadi ya Mungu wake, sasa hiyo siku Mungu wa kweli atafahamika ni yupi na ndiye atakayefafanua hitilafu zilizokuwa baina ya viumbe wake akiwemo binadamu na kuhukumu.

Hapo haijalishi uwe mkristo, Muislam, Budha, Hindu au asiye amini kuwepo kwa Mungu. Maadamu kakuumba yeye basi yeye ndiye Mungu wako.

Wa motoni ataenda motoni na wa peponi ataenda peponi. Haina haja ya pressure yakini itamuangukia kila nafsi.
 
Kwa maana hiyo hata wewe saizi ni ngumu kuthibitisha kua dini yako ni ya kweli na ni sahihi kuliko dini zingine mpaka siku ya hukumu ikifika?
 
Unapouliza kwa kusema "kila kitu" kina chanzo unamaanisha nini?

Nataka nijue hiyo kila kitu inakua na mipaka au haina mipaka

Maana kuna mwingine anaweza kusema kila kitu kina chanzo kwa dhana isiyo na mipaka halafu ukaja kukubaliana naye kwa baadhi ya vitu tu kua ndio vina chanzo kwa kuweka mipaka kua kitu fulani hakina chanzo

Kama ina mipaka basi swali lako la kuuliza kila kitu linakosa mantiki kwasababu kuna vitu viko nje ya dhana ambavyo navyo vilipaswa kuhusihswa ila hujataka kuvihusisha

Kama kila kitu ni neno ambalo liko openly na universal lisilo na mipaka tunaweza tukakupatia majibu

Ila kwanza tukabaliane hapo
Kijana hivi akili uliyopewa unaitumiaje aisee, maana naona unaihujumu ? Kisha nikikuuliza maswali unakimbia.

Kitu ni tamko lisilo fungamana na wakati, yaani ni jina. Sasa jibu swali hili.

Kwanza kabla ya kunipa majibu au jibu (Ambalo najua huwezikunipa), naomba nitajie vitu viwili au mambo mawili tu ambayo hayana mpaka na uniambie umejuaje hilo ?
 
Nataka nijue hiyo dhana ya "kila kitu" ni universal principle au ni kikanuni ulichokiweka ili kikupe majibu ambayo yapo umejisetia?

Yaani namaanisha hiyo kanuni isiwe na neno "isipokua" au neno lolote ambalo linaonesha kuweka mpaka katika dhana ambayo hutaki kuihusisha katika kundi la "kila kitu"
 
Back
Top Bottom