Lazima uelewe kila kikundi chochote cha watu,wanaunda umoja wao wana katiba yao,ya kuendesha kikundi husika.Kwa mfano viko vikundi,vimeweka masharti fulani,usipoyafuata umeshajitoa uanachama,kwa mfano hujahudhuria vikao vitatu vya chama,bila maelezo yoyote ya kuridhisha,tayari uwanachama huna.Zipo dini,usipohudhuria katika nyumba zao za ibada,tayari umeshatoka katika dini hiyo,hata ukifariki hawakuziki.
Na katika uislamu una kitabu cha Qur'an na muongozo wa Mtume Muhammad,katika uislamu mtume anasema "Tofauti kati ya muislamu na asiye muislam ni SWALA",USIPOSWALI HUNA UISLAMU.