Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
- Thread starter
- #61
Sehemu ya 23.
Wazo lililomjia Richard kwa wakati huo ilikuwa ni kwenda Kigamboni nyumbani alipokuwa akiishi Evelyne na Happy, hakutaka kuendelea kubaki katika mabishano na Happy, alitamani kufahamu ni nini kilichokuwa kimemtokea mpenzi wake bila kujua kuwa kumbe yeye ndiye alikuwa sababu ya mambo yote hayo kutokea.
“Let’s go.” (Twende zetu.)
“Where?” (Wapi?)
“I say let’s go.” (Nasema twende.)
“Where?” (Wapi?)
“Kigamboni.”
“Okay, but let me then I take a bag to class,” (Sawa ila ngoja basi nikachukue begi darasani.”
“Hurry up,’ (Fanya haraka,) alisema Richard kisha Happy akafanya kama alivyoomba, aliporudi safari ya kwenda kigamboni ikaanzia hapo.
Richard hakutaka kwenda na gari lake ili kuepuka usumbufu ambao wangeweza kukutana nao kivukoni, waliamua kupanda bajaji ambayo iliweza kuwafikisha mpaka kivukoni.
Mpaka kufikia muda huo Richard alitamani sana kumuona mpenzi wake ili aweze kuzungumza naye, moyoni aliamini katika mapenzi ya dhati ambayo aliahidi kamwe yasingeweza kufa.
Alimpenda sana Evelyne na aliamini hakukuwa na msichana mwingine ambaye angeweza kuiziba nafasi hiyo katika moyo wake, wakati ambao alikuwa akiendelea kuyawaza hayo nyuma ya pazia hakujua kuwa kumbe alikuwa amepigwa picha za utupu na Monalisa ambazo zilitumwa kwa Evelyne na picha hizo ndizo ambazo zilimfanya abadilike kiasi cha kuondoka kabisa eneo la chuo.
Walipokuwa wamepanda kwenye panton Richard alitamani liongeze mwendo ili aweze kufika haraka nyumbani alipokuwa akiishi Evelyne, alitamani kumuona mpenzi wake na kuzungumza naye kwa wakati huo.
Alipokuwa ameketi alipaona kuwa kama kuna misumari iliyomchoma hivyo hakutaka kuendelea kuketi sehemu hiyo, alisimama na kuanza kuzunguka huku na kule kama mtu aliyeanza kuchanganyikiwa, kitendo hicho kiliwafanya baadhi ya watu waliyokuwemo kwenye panton hiyo waanze kumshangaa Richard.