Nisamehe Mpenzi

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
152,998
453,945
Mtunzi Juma hiza Sehemu ya 01

Hali ya hewa ilikuwa shwari katika jiji la Daresalaam. Ndani ya chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kilichokuwepo maeneo ya Posta mtaa wa Shaaban Robert, msichana mrembo aliyejulikana kwa jina la Evelyne alionekana akitoka darasani huku akiwa anakimbia, machozi yalikuwa yakimdondoka kwa wakati huo.

“Evelyne! Evelyne! Evelyne,” ilisikika sauti ya msichana mwingine ambaye alikuwa akimfuata nyuma Evelyne baada ya kutoka darasani.

Evelyne aliongoza moja kwa moja mpaka kwenye kimbweta, alipofika hapo aliketi na kuanza kulia huku akiwa amejiinamia.
“Evelyne kuna nini mbona sikuelewi?” aliuliza msichana huyo aliyekuwa akimfuata nyuma Evelyne, alionekana kutoelewa chochote kilichokuwa kikiendelea kwa wakati huo.

“Hapana Happy siwezi kuendelea kuwa eneo hili acha niondoke zangu,” alisema Evelyne kwa sauti iliyoandamana na kilio cha kwikwi.

“Unaondoka unaenda wapi sasa na wakati darasani kuna kipindi?” aliuliza Happy huku akimtazama Evelyne ambaye aliendelea kulia muda wote huo.
“Narudi zangu nyumbani,” alijibu Evelyne.

“Unajua sikuelewi Evelyne,” alisema Happy lakini kabla ya Evelyne kumjibu lolote aliinuka na kuondoka eneo hilo la chuo, Happy alibaki akimtazama Evelyne huku asijue ni nini kilichokuwa kikiendelea.

Evelyne na Happy walikuwa ni marafiki wakubwa sana katika chuo hicho, walikuwa wakisaidiana mambo mengi sana, walishiriki kusaidiana katika masomo na hata katika mipango yao ya kimaisha pia walishirikishana.

Happy alikuwa akimfahamu vyema rafiki yake huyo tangu walipoanza kusoma katika chuo hicho mpaka kufikia mwaka waowa mwisho wa Digrii ambao ndiyo walikuwa wameubakiza. Walikuwa wakisomea Uhasibu.

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha ya Evelyne, Happy alikifahamu na kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha ya Happy, Evelyne naye alikifahamu, kwa kifupi walikuwa ni marafiki waliyoshibana.

Walikuwa wakiishi pamoja katika chumba kimoja walichokuwa wamepanga maeneo ya Kigamboni.
Screenshot_20190211-192125.jpeg
 
Sehemu ya 02.

Wakati Happy akiwa bado amesimama eneo lile ghafla! aliisikia sauti ya kiume ikimuita nyuma yake, haraka aligeuka na kukutana na mtu aliyekuwa akimuita. Alikuwa ni Richard.

“Niambie Shem.”
“Poa tu!vipi mbona Evelyne ametoka darasani kuna nini?”
“Sijui.”
“Yuko wapi?”
“Ameondoka, ameniambia anarudi nyumbani hawezi kuendelea kuwa eneo hili.”

“Mbona unanichanganya?”
“Richard kwani kuna kitu gani kimetokea kati yenu?”
“Hakuna kitu.”

“Mbona sasa Evelyne amebadilika ghafla! baada ya kukuona.”
“Mimi mwenyewe sielewi chochote.”
“Una uhakika?”

“Ndiyo Happy inamaana huniamini?”
“Nakuamini sana,” alijibu Happy.
Richard alikuwa ni mvulana aliyekuwa akitokea katika familia ya kitajiri sana, alikuwa ni kijana mtanashati, mwenye mwili uliyojengeka vyema kimazoezi uliyosindikizwa na muonekano nadhifu ambao ulimpagawisha kila msichana aliyemuona katika chuo hicho.

“There’s something I want to tell you,” (Kuna kitu nataka kukuambia Richard,) ilikuwa ni sauti ya msichana mmoja aliyejulikana kwa jina la Monalisa ambaye alimuita Richard chemba na kuzungumza naye.

“What’s that Monalisa?” (Kitu gani hicho Monalisa?)aliuliza Richard huku akimtazama Monalisa ambaye alikuwa akijing’atang’ata kucha za vidole vyake kwa wakati huo.

“But I feel like I’m going to make a mistake,” (Lakini nahisi kama nitakukosea,) alisema Monalisa huku akijishtukia, macho yake alikuwa ameyalegeza.

“No, tell me don’t be afraid,” (Hapana niambie usiogope,) alisema Richard huku akiwa makini kumsikiliza. Kwa muonekano ambao aliuona kwa Monalisa akilini mwake alikwisha fahamu ni kitu gani ambacho msichana huyo alitaka kumueleza lakini hakutaka kuwa na papara ya kukurupukia mambo, alihitaji kumpa muda msichana huyo wa kujieleza ili asahili kile alichokuwa kikifikiria.

“Richard I love you so much and I’m ready to do anything for you, please say yes don’t let my kid,” (Richard ninakupenda sana na nipo tayari kufanya lolote kwa ajili yako, tafadhali sema ndiyo usinikatalieombi langu,) alisema Monalisa huku akianza kumsogelea Richard kwa lengo la kumbusu.
 
Sehemu ya 03.

“No, don’t do that,” (Hapana usifanye hivyo,) alisema Richard huku akimzuia Monalisa, kitendo hicho kikamkwaza Monalisa, akahisi kukataliwa, alijisikia vibaya mno.

Monalisa hakuwa msichana wakwanza na wa mwisho kumsumbua Richard, kila msichana alitamani kuwa naye kimapenzi na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kupokea usumbufu kila kukicha lakini hakukuwa na msichana aliyewahi kuipata nafasi hiyo kwa Richard.

Moyo wa Richard ulizama kimapenzi kwa msichana mmoja ambaye ndiye alikuwa ameishikilia nafasi hiyo ya kimapenzi na kuwazibia wasichana wengine wote waliyokuwa wakiitamani kuipata.Hakukuwa na mtu ambaye alitaka kuamini kuwa Evelyne msichana aliyeonekana kuwa na uzuri wa kawaida ndiye ambaye alifanikiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Richard, wengi wao waliamini kuwa kwa muonekano wa kuvutia aliyokuwa nao Richard pamoja na kutokea katika familia ya kitajiri basi ni lazima angekuwa na msichana ambaye alitikisa chuo kizima kwa uzuri wake au aliyetokea katika familia ya kitajiri lakini haikuwa hivyo.

“Huyu kinyago ndiyo anatuzibia riziki yetu,” alisema Monalisa huku akiwaambia wasichana wenzake watatu walipokuwa hostel wameketi kitandani, wote walikuwa wakimtamani Richard.
“Nani ndiyo huyu Evelyne?” aliuliza mmoja wao.

“Ndiyo hivi ana uzuri gani yule msichana mpakawa kutembea na Richard kama sio uchawi,” alisema Monalisa huku akiwa ameubetua mdomo wake.

“Atakuwa mwanga yule sio bure,” alisema msichana mwingine maneno yaliyowafanya wote wakacheka kwa sauti kubwa kisha wakigongeana.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuibuka kwa chuki kati ya wasichana hao na Evelyne, walitokea kumchukia sana pale chuoni baada ya kugundua kuwa alikuwa akijihusisha na mahusiano ya kimapenzi na Richard, hilo lilizidi kumuumiza kila msichana ambaye aliwahi kumtamkia neno nakupendaau kuibuka kwa chembechembe zozote za kimapenzi kwa mvulana huyo aliyetokea kuipagawisha mioyo ya wasichana wengi chuoni hapo.
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
Usikose toleo lijalo.
 
Sehemu ya 04.

Monalisa ndiye msichana ambaye alionekana kumpenda zaidi Richard kuliko wasichana wengine pale chuoni, licha ya Richard kumkatalia ombi lake la kuwa wapenzi lakini bado hakutaka kukubali hilo, aliamini kwa vyovyote iwezekanavyo ni lazima mvulana huyo angefanikiwa kummiliki.

Kuna kipindi kichwani mwake yalimjia mawazo ya jinsi ambavyo alivyofanikiwa kumpata Richard kisha wakawa wanayafurahia mapenzi yao katika ufukwe wa bahari ya Hindi, alizidi kulifurahia hilo katika moyo wake maradufu na hata pale mawazo hayo yalipomtoka kichwani alionekana kukasirika mno, hakutaka kuamini kama kweli alikuwa akiwaza kwa wakati huo.

Moyo wa mapenzi ukazidi kumuendesha vilivyo, alikuwa amezama katika dimbwi la mapenzi ya Richard mvulana ambaye na yeye moyo wake ulikuwa umekufa umeoza kimapenzi na msichana mwingine chuoni hapo.

“Kwanini Richard anashindwa kunikubalia hivi inamaana sina uzuri wa kumvutia au?” aliuliza Monalisa huku akiwatizama wale mashoga zake watatu walipokuwa hostel.

“Sio kwamba humvutii isipokuwa Richard ameshatekwa na Evelyne,” alijibu msichana mmoja huku akionekana kuwa bize na simu yake.

“Sitaki kumsikia huyo mpumbavu tena nitamkomesha mwanaharamu yule,” alisema Monalisa huku akionekana kuchukia mno baada ya kulisikia jina la Evelyne likitajwa na rafiki yake huyo aliyejukana kwa jina la Penina.

“Shoga yangu mimi nimeshachoka kumfuatilia huyo Richard kwani hakuna wavulana wengine hapa chuo kwani yeye nani?” aliuliza Mary.

“Jamani Richard ni Handsome mimi mwenyewe bado sijaona mvulana anayemfikia kwa uzuri hapa chuoni,” alisema Adela msichana aliyeikamilisha hesabu yao pale ndani, walikuwa wanne.
“Lakini lazima nitampata tu,” alisema Monalisa huku akijiapiza kumpata kwa vyovyote iwezekanavyo.

“Utatumia njia gani?” aliuliza Mary huku akimtazama Monalisa.
“Nitajua tu lakini lazima nimpate, nitahakikisha Richard anakuwa mali yangu,” alisema Monalisa.
 
Sehemu ya 05.

Hakukuwa kuna kitu kingine alichokuwa akikihitaji Monalisa zaidi ya kuona anafanikiwa kummiliki Richard mvulana ambaye alitokea kuuteka moyo wake. Kila kitu alichokuwa akikifanya, aliamua kukifanya huku malengo yake makubwa yakiwa ni siku moja atafanikiwa kummiliki Richard.

Miongoni mwa wasichana ambao waliwahi kumtamani Richard kimapenzi kutokana na muonekano wake kuwa mzuri alikuwa ni Adela, Mary pamoja na Penina.

Wasichana hawa wote mioyo yao iliwahi kufa na kuoza kwa Richard lakini kutokana na msimamo aliyokuwa nao mvulana huyo hawakuweza kuambulia hata busu bandia.

Kila mmoja alishaanza kukata tamaa ya kufanikiwa kulipata penzi la mvulana huyo, walitumia kila aina ya njia walizoziona zinafaa kumteka Richard kimapenzi lakini hakukuwa na njia hata moja iliyomkamata mtegoni.

Hilo lilizidi kuwasononesha mioyo yao mno, ilifikia kipindi hata wakati wa kula chakula kila mmoja alishindwa kula kwa nafasi yake, moyo wake ulikuwa ukiumia kwa sababu ya kulikosa penzi la Richard.
“Sitaki kuamini na sitaamini kama nimelikosa penzi la Richard,” alisema Monalisa.

“Hutaki kuamini nini sasa wakati mwenzako ameshapendwa,” alisema Penina huku akimcheka Monalisa wakati huo walikuwa darasani, tukio hilo lilizidi kumuumiza mno moyo wa Monalisa, hakutaka kuamini licha ya kuupoteza muda wake wote katika kumfukuzia Richard lakini mwisho wa siku aliambulia patupu.

“Nadhani kuna kitu natakiwa kufanya,” alisema Monalisa.
“Kitu gani?” aliuliza Penina.
“Ni mapema mno kukuambia.”
“Niambie usinifiche.”

“Usijali nitakuambia,” alisema Monalisa huku akionekana kutawaliwa na mawazo.
Kichwani mwake lilimjia wazo, lilikuwa ni wazo la kufanya kitu maalumu kwa ajili ya Richard ili afanikiwe kumpata kimapenzi na ni katika wazo hilo hakutaka kuyawaza au kuyapima maumivu ambayo angeweza kumpa Evelyne msichana ambaye tayari alikuwa akijihusisha kimapenzi na Richard.
 
Sehemu ya 06.

Moyo wake bado uliendelea kumuuma mno, kila alipokuwa akimuona Richard darasani alijihisi kuwa na sababu milioni mia moja za kuwa naye kimapenzi.

Kuna kipindi alipokuwa akimtazama Richard pamoja na muonekano wake mzuri alijaribu kumlinganisha na Evelyne msichana ambaye alimuona kuwa na uzuri wa kawaida sana, hakustahili kabisa kuwa na Richard kimapenzi.

Lilipokuja suala la uzuri kati yake na Evelyne alipokuwa akijiremba kwenye kioo alikiri fika alimzidi msichana huyo kwa uzuri wala hakukuwa na upinzani katika hilo.

“Sasa kwanini Richard asinipende mimi?” alijiuliza swali ambalo lilizidi kumfanya ajione kuwa na mapungufu mengi katika mwili wake, kuna muda pia alijiona kuwa miongoni mwa wajinga na wapumbavu wa kumkosa Richard.

“Lazima nifanye kitu kwa ajili yako Richard, sitokubali na siwezi kamwe kukubali kuona ukiendelea kuutesa moyo wangu kila siku, nakupenda sana na ninahitaji ulifahamu hilo,” alisema Monalisa siku moja usiku alipokuwa amelala hostel, usiku wa siku hiyo ulikuwa mrefu sana kwake na aliutumia katika kumfikiria Richard tu, kichwani mwake jina la Richard lilitawala sehemu kubwa sana.

Alichokuwa amepanga kukifanya Monalisa ni kutengeneza mazingira ambayo yangeweza kumuonyesha kuwa yeye na Richard kuwa ni wapenzi, alilifikiria wazo hilo huku akiamini kama kweli angeweza kufanikiwa kuyatengeneza mazingira hayo basi ni lazima Evelyne angeingiwa na wivu kiasi cha kuumia sana moyoni mwake, hilo ndilo alilokuwa anahitaji kuliona likitokea kwa msichana huyo, hakumpenda wala hakutaka kumuona akiendelea kuwa karibu na Richard mvulana ambaye tayari alikuwa ameshauteka moyo wake wa kimapenzi.

“You must be mine,” (Lazima utakuwa wangu,) alijisemea Monalisa huku akitabasamu, ulikuwa ni wakati ambao wazo hilo lilimjia kichwani mwake.
 
Sehemu ya 07.

Maisha ya chuo yaliendelea huku Monalisa kila siku akizidi kuumia, kuna kipindi alitamani kutengeneza mazingira ya kumfanya Evelyne afukuzwe chuo na yote hayo aliwaza ilimradi afanikiwe kumpata Richard.

Siku moja Monalisa alijaribu kutafuta nafasi ya kuzungumza na Richard mpaka akafanikiwa kuipata.

“Kwanini hutaki kuwa na mimi?”
“Hapana siwezi.”
“Kwanini?”
“Nipo katika mapenzi tayari.”
“Richard mbona unapenda kunifanyia hivyo, kwanini unautesa moyo wangu kiasi hiki?”

“Sio kama nakutesa ila tatizo tayari moyo wangu upo kwa msichana mwingine.”
“Hunipendi?” aliuliza Monalisa.

Lilikuwa ni swali gumu mno lililomfanya Richard ashindwe kutoa jibu la haraka, alibaki akimtazama Monalisa huku asijue ni nini alitakiwa kumjibu kwa wakati huo.

Macho yake yalipotazamana na ya Monalisa kuna kitu alikigundua kilikuwa kikiendelea kwa wakati huo, aliyashuhudia machozi yakianza kumbubujika Monalisa mashavuni mwake, hakutaka kuamini kile alichokuwa akikishuhudia, kitendo cha kumuona msichana mrembo kama yule akiyadondosha machozi mbele yake hakika kilimuumiza mno, kuna muda alianza kujiona kuwa na makosa makubwa mno kwa kuendelea kuutesa moyo wa msichana ambaye alionekana kumpenda kuliko kitu chochote kile.

Alichoamua kukifanya alikitoa kitambaa katika mfuko wa suruali yake kisha akamfuta machozi Monalisa, kitendo hicho kilimfanya Monalisa ashangae, hakutaka kuamini kama machozi yake yalimgusa Richard kiasi kwamba akafikia hatua ya kumfuta.
“Richard,” alimuita.
“Niambie,” alisema Richard.

“Unaweza kweli kuendelea kuishuhudia nafsi ambayo inateseka, inasononeka, inaumia kila siku kwa sababu yako?” aliuliza Monalisa.
“Hapana siwezi,” alijibu Richard.
 
Sehemu ya 08.

“Sasa kwanini hutaki kunifikiria hata mara moja, nimekusumbua sana, nimetumia kila njia ilimradi niwe na wewe lakini imeshindikana basi naomba unisaidie kitu kimoja tu kama hutojali,” alisema Monalisa kwa sauti ya utulivu.
“Kitu gani hicho?” aliuliza Richard huku akimtazama Monalisa.

“Nalihitaji penzi lako, naomba nitumie kuwa na wewe ndani ya usiku mmoja nahisi nitakuwa nimeuridhisha moyo wangu maana kila siku unaishi kwa kuteseka kwa sababu yako,” alisema Monalisa.

Maneno ya Monalisa yalimuweka Richard kuwa katika wakati mgumu sana, hakutaka kuamini kile alichokuwa akikisikia kutoka kwa msichana huyo ambaye alikuwa na kila sifa za kumteka mwanaume rijali, bado hakutaka kuamini kile alichokuwa amekisikia kutoka kwa msichana huyo, ilibidi amuulize ni nini alichokuwa amefikiria lakini kabla hajafanya hivyo ghafla! Monalisa aliweza kumzuia asizungumze lolote kwa kumuwekea kidole katika lips zake.

“Don’t say no please say yes,” (Usiseme hapana tafadhali sema ndiyo,) alitamka maneno haya Monalisa wakati ambao alikuwa amemuwekea kidole kwenye lips Richard.

Richard alishindwa la kufanya, alikosa la kuamua kwa wakati huo. Ni kweli Monalisa alikuwa na sifa zote za kumchanganya mwanaume rijali na kupitia udhaifu huo aliweza kumchanganya Richard mwisho akajikuta akili yake ikianza kumfikiria.

“Ok right but let’s make it a secret between us,” (Sawa ila naomba tufanye iwe ni siri kati yetu,) alisema Richard huku akionekana kukosa uvumilivu kabisa.
“Don’t worry about it I will keep that secret,” (Usijali kuhusu hilo nitaitunza siri hiyo,) alisema Monalisa huku akimtoa hofu Richard.
 
Sehemu ya 09.

“Don’t go against our agreement,” (Usiende kinyume na makubaliano yetu,) alisema Richard.
“Don’t worry,” (Usijali,) alisema Monalisa huku akitabasamu.

Monalisa hakutaka kuamini kama kweli alifanikiwa kwa asilimia zote mpango wake, aliamini huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kumpa maumivu Evelyne, maumivu ambayo alikuwa akiyapitia kila siku.

Siku hiyo aliporudi hostel hakukuwa na kazi nyingine aliyoifanya zaidi ya kuwasiliana na Richard, alisahau mpaka kusoma kwasababu ya Richard mvulana aliyeutesa sana moyo wake lakini mwisho wa siku alifanikiwa kuwa naye.

“Mbona unafuraha sana leo?” aliuliza Penina wakati huo alikuwa akisoma kitabu.

“We acha tu shosti yani huwezi kuamini,” alisema Monalisa huku furaha ikionekana kumtawala.

“Kuhusu nini?” aliuliza Penina.
“Kuhusu Richard,” alijibu Monalisa.
“Amefanyaje?”
“Amekubali kuwa na mimi.”
“Unasemaje?”

“Ndiyo amekubali kuwa na mimi,” alijibu Monalisa jibu lililowashangaza wasichana wote pale ndani, kila mmoja hakutaka kuamini kama kweli Monalisa aliweza kukubaliwa na mvulana huyo. ****

Yalikuwa ni majira ya saa tatu za usiku, Richard alikuwa nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni B, wakati huo alikuwa chumbani kwake amejilaza kitandani.

Akili yake bado iliendelea kumfikiria Monalisa, hakujua ni kwanini msichana huyo alianza kumuingia kwa kasi katika kichwa chake, kuna kipindi alianza kujilaumu kwa kumkubalia ombi lake lakini alipotaka kuchukua simu yake na kutaka kumuandikia ujumbe wenye lengo la kughairi uamuzi huo alishindwa, alijikuta vidole vyake vikiwa vizito kuandika ujumbe wa aina hiyo mwisho akajikuta akimtumia ujumbe wa salamu na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuchat na msichana huyo.

Alisahau kumjulia hata hali Evelyne msichana ambaye alikuwa katika mahusiano naye, alichokuwa amekiona ni cha umuhimu kwa wakati huo ni kuwasiliana na Monalisa ili aweze kuzikidhi haja za moyo wake, alipanga kushiriki kufanya mapenzi naye halafu huo ndiyo uwe mwisho wa uhusiano wao, hakupanga kumuumiza Evelyne na ndiyo sababu aliomba iwe siri ili msichana wake huyo asiweze kugundua lolote.
*
*
Je, nini kitaendelea?
Usikose sehemu ijayo.
 
Sehemu ya 10.

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika moyo wa Richard aliamini ilikuwa ni siri nzito mno na hakukuwa na mtu mwingine ambaye alikuwa akikifahamu zaidi yake na Monalisa.

Wakati alipokuwa akiendelea kuwasiliana na msichana huyo ndivyo ambavyo Monalisa na yeye alizidi kuwatambia wasichana wenzake mule hostel jinsi ambavyo alikuwa msichana shupavu ambaye hakukubali kushindwa kirahisi kwa kumkosa Richard.

Hilo lilizidi kuwaumiza wasichana wenzake mno, walianza kuingiwa na wivu baada ya kusikia kuwa Richard na Monalisa walikuwa ni wapenzi kwa wakati ule, kuna kipindi hawakutaka kukubali kabisa lakini huo ulibaki kuwa ni ukweli. Richard na Monalisa walikuwa katika mapenzi.

“Unafikiri nitakubali kirahisi kuachana naye, nitahakikisha anabaki kuwa wangu tu,” alisema Monalisa huku akiwaambia Penina, Mary na Adela, walionekana kuingiwa na wivu mno, hawakutaka kuamini kabisa.

“Sijui Evelyne atakuwa katika hali gani akisikia kuwa wewe na Richard ni wapenzi?” aliuliza Mary swali la kinafki ambalo jibu lake lilikuwa wazi kabisa, swali hilo likawafanya wote watokwe na kicheko halafu wakagongeana kama ilivyokuwa kawaida yao.

“Evelyne ndiyo mdudu gani?” aliuliza Monalisa huku akiendelea kucheka.

Hakutaka kuona msichana huyo akiendelea kuyafurahia mapenzi na Richard, kitu pekee alichokuwa amepanga kukifanya ni kuhakikisha anafanikiwa kumpokonya Richard mikononi mwake na kisha anakuwa mali yake peke yake tu.

Hakuacha kuendelea kuwasiliana na Richard, walikuwa wakifanya mawasiliano kila siku huku moyoni akizidi kujiapiza kumteka mvulana huyo kimapenzi. “Nahitaji kukuona Richard.”
“Lini?”
“Leo.”
“Usiku huu?”

“Ndiyo, Kwani kuna tatizo gani mpenzi?”
“Hapana, hakuna tatizo.”
“Sasa kwanini hutaki?”
“Sio sitaki ila si upo hostel na kesho tunakipindi asubuhi?”
“Ndiyo najua hilo.”

“Sasa huoni hilo ni tatizo?”
“Richard mimi siwezi kusoma ukweli bila kuonana na wewe usiku wa leo, kama ni kipindi kuingia tutaingia tu kwanza kipindi chenyewe hakina umuhimu zaidi yako, tafadhali naomba kukuona japo sekunde moja, nitauridhisha moyo wangu.”
 
Sehemu ya 11.

“Sawa nakuja kukufuata muda huu hostel ila tafadhali naomba kila kitu kinachoendelea kibaki kuwa ni siri kati yetu.”

“Nilikuahidi na ninarudia kukuahidi, siwezi kuitoa siri hii, shida yangu kubwa ni kuwa na wewe tu basi.”
“Sawa nakuja.”

Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Monalisa na Richard waliyokuwa wakizungumza kwenye simu majira ya jioni, baada ya kumaliza kuzungumza Richard alijiandaa, alipomaliza aliwaaga wazazi wake kuwa anakwenda chuoni kwenye kipindi, wazazi wake walimkubalia kisha akaondoka kwa usafiri binafsi kama ilivyokuwa kawaida yake, siku hiyo aliamua kutembelea gari aina ya Toyota prado new model lenye thamani ya shilingi milioni 65.

Safari yake iliishia nje ya chuo cha IFM ambapo ndipo zilipokuwa hostel za chuo hiko, aliposimamisha gari aliamua kumtumia ujumbe mfupi Monalisa wa kumtaarifu kuwa tayari alikuwa eneo lile la chuo na kwa wakati huo alikuwa akimsubiria nje.

Haikuchukua dakika nyingi Monalisa aliweza kutoka nje ya chuo hiko na kuanza kuyaangaza macho yake huku na kule, Richard aliamua kupiga honi baada ya kumuona Monalisa akiwa katika hali hiyo, tabasamu mwanana lilichanua katika uso wa Monalisa ambaye alikuwa amevalia mavazi yaliyompendezesha kupita kawaida, baada ya kumuona Richard akiwa ndani ya gari alilifuata gari lile, alipolifikia Richard alimpa ishara ya kukaa kiti cha mbele, akafungua mlango wa gari hilo na kuingia.
“Umependeza sana,”alisema Richard huku akimtazama Monalisa.

“Asante Mpenzi na uzuri nao unachangia,” alisema Monalisa maneno yaliyowafanya wote wakatokwa na kicheko.
“Kwahiyo tunaenda wapi?” aliuliza Richard.

“Popote pale mpenzi utakapopapenda wewe,” alijibu Monalisa.
“Sehemu gani itakuwa na utulivu,” alisema Richard huku akionekana kutafakari jambo.

“Pale Serena vipi hapafai kwani?” aliuliza Monalisa swali lililomtoa Richard katika ile hali ya kutafakari.

“Yeah! pako vizuri sana, twende huko,” alijibu Richard kisha akawasha gari na kuondoka eneo hilo.
 
Sehemu ya 12.

Walifika katika hoteli hiyo ya kifahari ya Serena kisha wakachukua chumba, Monalisa bado alikuwa haamini kama kweli siku hiyo alikuwa anafanikiwa kulala na Richard kitanda kimoja, alionekana kuwa mwenye furaha mno.

Walipoingia ndani ya chumba cha hoteli hiyo Richard bado aliendelea kuisisitiza siri ambayo ilitakiwa kuendelea kubaki kati yao, moyoni mwake alimpenda sana Evelyne na hakupanga kumsaliti wala kumpa maumivu yoyote ya kimapenzi, aliamini baada ya kumaliza kufanya mapenzi na Monalisa basi huo ndiyo ulikuwa mwanzo na mwisho wa penzi hilo la dharura.

Waliagiza chakula na baada ya kuletewa na muhudumu wa hoteli hiyo walianza kula taratibu huku wakitazamana kwa macho ya kuibiana.

Baada ya kumaliza kula chakula hakukuwa na tukio lingine ambalo lilitakiwa kuendelea kati yao zaidi ya kuanza kushikanashikana huku midomo yao ikiwa imekutana na kuanza kubadilishana mate, walitumia muda kama wa dakika kumi na tano katika kuchezeana miili yao na baada ya hapo kitendo kilichofuata waliamua kuvunja amri ya sita. ****

Evelyne aliendelea kuishi na matumaini ya kumpenda Richard siku zote, aliamini alikuwa ni mwanaume wa maisha yake hivyo hakukuwa na udanganyifu wowote uliyokuwa ukiendelea.

Kipindi hicho ambapo Monalisa alikuwa amefanikiwa kuwa na Richard kimapenzi zilianza kuvuma tetesi za chinichini pale chuoni kuwa wawili hao walikuwa wakitoka kimapenzi, Evelyne baada ya kuzisikia tetesi hizo aliamua kuzipuuzia, alimuamini sana Richard hivyo kila kitu ambacho alikuwa akiambiwa kibaya kilichomuhusu mwanaume wake huyo aliweza kukikanusha, hakutaka kuishi na wasiwasi.
“Kwanini hutaki kuamini kila kitu kibaya unachoambiwa kuhusu Richard?" aliuliza Happy.

“Hapana, ninampenda sana, ananipenda pia hata hivyo najua hawezi kunifanyia ukatili wowote," alijibu Evelyne.
*
*
*
Je, nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 13.

Evelyne alizidi kuishi na imani hiyo ya kumpenda sana Richard kuliko mwanaume yoyote chuoni pale, aliwakataa wanaume wengi sana, kila kitu alichokuwa anakifanya alikifanya kwa ajili ya Richard.

Kipindi ambapo zilianza kuvuma tetesi chuoni kuwa Richard na Monalisa walikuwa wakitoka kimapenzi alizikataa, hakutaka kuamini kirahisi bila kujua kuwa huo ndiyo ukweli uliyokuwa ukiendelea nyuma ya pazia. ****

Katika mapenzi hakuna kitu kibaya kama kumpenda mtu ambaye hakupendi, kumthamini mtu ambaye hakuthamini, Kumjali mtu ambaye hakujali, hatambui thamani yako kwake baada ya kukutumia.
Hakuna maumivu makali ya moyo kama kuwa na mapenzi ya dhati na mtu ambaye nyuma ya pazia anakusaliti.

Huo ndiyo huwa mwanzo wa maumivu ya mapenzi, kuna muda unaweza ukafikia mtu usitamani kabisa kupenda, moyo ukajenga chuki ukamuona kila mwanaume au mwanamke ni adui yako.

Waliyosema mapenzi ni upofu hawakukosea na hivi ndivyo ambavyo ilikuwa kwa Evelyne, licha ya kuzisikia tetesi juu ya Richard lakini hakutaka kuziamini, alimuamini mno mwanaume huyo.

Adela, Mary pamoja na Penina hawa ndiyo walikuwa wasichana wa kwanza kumpa taarifika hizo Evelyne, walitumia kila njia ya kumueleza ukweli uliyokuwa ukiendelea kati ya Richard na Monalisa lakini Evelyne hakuwaamini.

“Huo ndiyo ukweli shosti Richard sasa hivi sio wako tena,” alisema Mary, wakati huo walikuwa kwenye kimbweta, ulikuwa ni muda ambao hawakuwa na kipindi darasani.

“Umemaliza?” aliuliza Evelyne huku akionekana kuyapuuzia maneno ya Mary, hakutaka kuyaamini.
 
Sehemu ya 14.

“Monalisa sasa hivi ndiyo ameichukua nafasi yako, huna chako tena,” alisema Penina kwa sauti ya juu kidogo.

“Lakini mimi naona tumuache, tusiendelee kumlazimisha auamini ukweli ambao siku si nyingi utakuwa wazi,” alisema Adela huku akionekana kumkomoa Evelyne.

Kila neno alilokuwa akiambiwa Evelyne hakutaka kuliamini, alipuuzia na mwisho wa siku aliendelea kusoma kama ilivyokuwa kawaida yake. Alikuwa ni msichana mwenye mapenzi ya dhati mno kwa mpenzi wake huyo ambaye tayari alikuwa ameshamsaliti.

“Siwezi kuamini kama Richard anaweza akanisaliti, siamini,” alisema Evelyne alipokuwa ndani ya chumba chake, wakati huo Happy alikuwa akimtazama.

“Evelyne hivi unajua kuwa lisemwalo lipo na kama halipo basi jua linakuja,” alisema Happy huku akiendelea kumtazama Evelyne ambaye alionekana kuwa amekufa ameoza kwa Richard.

“Happy nafikiri unamfahamu Richard vizuri, sio mgeni kwako, nadhani unajua ni wapi nilipotoka naye hivi unaweza ukaamini hiki ninachokisikia kuwa ananisaliti?”

“Lakini wanaume sio watu wa kuwaamini kiasi hiko.”
“Sio kwa Richard lakini.”
“Umemuuliza?”
“Kuhusu nini?”
“Kuhusu hizi habari?”
“Hapana.”

“Halafu mbona yeye na Monalisa leo hawajaingia chuo?”
“Aliniambia anajisikia vibaya hivyo ameshindwa kuja.”
“Na Monalisa?”
“Sijui kuhusu habari zake.”
“Mmh!” aliguna Happy.

Alichoamua kukifanya Evelyne ni kuichukua simu yake ya mkononi kisha akampigia Richard, alihitaji kufahamu hali yake kwa wakati huo lakini kitu cha kushangaza simu ya Richard ilikuwa ikiita bila kupokelewa, alianza kuingiwa na hofu kubwa moyoni, hakujua ni nini kilichokuwa kimemkuta mpenzi wake ambaye alimuambia kuwa anaumwa.
“Mungu wangu.”

“Nini?”
“Richard hapokei simu.”
“Umejaribu kupiga namba zake zote?”
“Ndiyo nimepiga lakini hapokei,” alijibu Evelyne huku hofu ikiwa tayari imemuingia, alianza kujiwa na hisia mbaya kwa mpenzi wake huyo kuwa pengine alikuwa amezidiwa kiasi cha kulazwa hospitalini. Kichwani mwake wazo la kuwa pengine Richard alikuwa na mwanamke mwingine na hiyo ndiyo sababu ya yeye kutopokea simu hakutaka kuliwazia. ****
 
Sehemu ya 15.

Moyo wa Richard ulikuwa katika hofu kubwa mno, hakutaka kuamini kama kweli alikuwa amemsaliti Evelyne tena katika mazingira ambayo hakuyategemea.

“Nadhani biashara yetu imeishia hapa,” alisema Richard alipoamka asubuhi na kumkuta Monalisa akiwa tayari ameshajiandaa na kwa wakati huo alikuwa ameketi kitandani huku akiiperuzi simu yake.

“Itaisha vipi wakati mimi na wewe tayari ni wapenzi?” aliuliza Monalisa huku akijibebisha.

“Monalisa unajua unanichanganya kwani haya ndiyo yalikuwa makubaliano yetu?”
“Mimi sijui ila fahamu kuwa sisi tumeshakuwa wapenzi.”
“Acha utani Monalisa.”

“Tangu lini nimeanza utani na wewe?”
“Monalisa lakini si unajua kuwa mimi nina mpenzi wangu na ninampenda sana.”
“Hilo silijui kama kweli ulikuwa unampenzi na unampenda kwanini umekubali kumsaliti, kwanini umekubali kunikubaliana ombi langu.”
“Unasemaje?”

“Tayari umeshakuwa mpenzi wangu,” alijibu Monalisa huku akitabasamu.
Richard alikurupuka pale kitandani kisha akaanza kuitafuta simu yake, hakuiona ilibidi amuulize Monalisa.
“Simu yangu iko wapi?”
“Ninayo.”
“Naiomba.”

“Siwezi kukupa,” alijibu Monalisa kisha akaamka pale kitandani akatoka nje huku akiwa anakimbia, Richard alishindwa kumfuata Monalisa kwani kwa wakati huo alikuwa uchi wa mnyama, alibaki pale kitandani huku akilalamika, alijilaumu mno kwa kufanya kosa la kumsaliti mpenzi wake ambaye aliamini kwa vyovyote alikuwa anaenda kumpoteza katika maisha yake huku sababu kubwa ikiwa ni Monalisa msichana ambaye tayari alionekana kuwa sumu ya penzi hilo.

Muda ambao Evelyne alikuwa akimpigia simu Richard ndiyo muda huohuo ambao Monalisa alikuwa na simu ya Richard. Hakutaka kuipokea simu baada ya kuona mpigaji alikuwa ni Evelyne, alipokuwa hostel kuna muda alitamani kuipokea lakini alisita kufanya hivyo, hakutaka kuwa na haraka ya kumpa maumivu Evelyne katika moyo wake mwisho aliamua kuizima kabisa.
*
*
Je, nini kitaendelea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom