Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,165
- Thread starter
- #141
Sehemu ya 51.
Baada ya masaa kadhaa kupita, hatimaye majibu yaliweza kutolewa na daktari, kutokana na ajali aliyoipata Fredrick ilimsababishia matatizo katika kizazi chake pamoja na mshtuko aliyoupata ulimpelekea kupooza hivyo katika maisha yake angeshindwa kuamka na kufanya shughuli zake kama ilivyokuwa kawaida na badala yake maisha yake yalibadilika na kuwa ni ya kitandani.
Fredrick alikuwa amelala kitandani, uso wake ulikuwa umetawaliwa na furaha, alizidi kuonekana kuyafurahia maisha yake.
Alimtazama mke wake ambaye machozi yalikuwa yakimdondoka kwa muda huo, Evelyne kila alipokuwa akimtazama mume wake jinsi alivyokuwa amelala kitandani alihisi maumivu makali mno ndani ya moyo wake.
Alimpenda sana mume wake, hakutaka kumuona akiendelea kuteseka, alipanga kufanya kila awezalo ili aweze kuyaokoa maisha yake lakini alipoyakumbuka majibu ya daktari kuwa asingeweza kupona, alizidi kuumia mno.
Hakuna maumivu makali kama kumuona yule umpendae akiteseka kwa ugonjwa katika dunia hii, ni zaidi ya maumivu makali mno.
Machozi yaliendelea kumbubujika Evelyne pale hospitalini, hakutaka kuamini kama mume wake alikuwa amepooza na kibaya zaidi alipoteza uwezo wa kupata mtoto. Hilo liliendelea kumuumiza sana moyo wake.
Ilikuwa imepita miezi kadhaa tangu walipofunga ndoa yao, kabla ya kufika hata mwaka tayari ndoa hiyo ilikuwa imeingiwa na tatizo.
Ndugu wa mume wake walipozipata taarifa za ajali hiyo hawakutaka kuelewa chochote, waliamini ilikuwa ni ajali ya kupangwa na ilisababishwa na Evelyne ambaye walidai alizitamani mali za ndugu yao.