Nisamehe Mpenzi

Nisamehe Mpenzi

Shunie Katufanyia Utumbo kama wanatufanyiaga wale wapumbavu wa Into the badlands Ndo nn sasa kupotea

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sehemu ya 19.

Evelyne aliendelea kuwa ni mwenye wasiwasi mkubwa baada kuona Richard hapatikani, tukio hilo lilizidi kumnyima furaha kabisa katika moyo wake, alikosa amani muda wote alikuwa akimfikiria Richard.

“Kwanini nakufikiria muda wote Richard utakuwa umepatwa na nini?” alijiuliza kwa sauti mpaka Happy akamsikia.
“Usiwaze hayo kama Richard angekuwa amepatwa na tatizo ni lazima ungepata taarifa.”

“Nani angeniambia?”
“Mama yake,” alijibu Happy kisha akamfanya Evelyne apunguze wasiwasi kidogo, alianza kuyaamini maneno ya rafiki yake baada ya kukumbuka alikuwa akifahamiana na Mama yake Richard, alimuheshimu sana Mama mkwe wake mtarajiwa na hii ndiyo sababu iliyomfanya ashindwe kumpigia simu.

Usiku wa siku hiyo Evelyne alishindwa kulala kabisa, hakutaka kuamini kama siku hiyo alikuwa analala bila kuzungumza wala kuchati na Richard. Japo aliambiwa na Happy apunguze wasiwasi lakini hakutaka kukubaliana na jambo hilo.

Wakati Happy alipokuwa amelala usingizi yeye aliamka kisha akaanza kumpigia simu Richard lakini bado alikuwa hapatikani.

Baada ya kuona ameshindwa kupata usingizi kabisa aliamua kuwasha data simu yake kisha akaingia WhatsApp kwa lengo la kujibu jumbe za watu waliyokuwa wamemtumia kwa siku hiyo, alianza kuzipitia moja baada ya nyingine.

Hakutaka kuamini macho yake baada ya kuona ujumbe kutoka kwa Monalisa, haraka aliufungua na ni hapo ambapo alishikwa na bumbuwazi baada ya kukutana na picha pamoja na video iliyokuwa ikimuonyesha Richard na Monalisa wakiwa kitandani. “YOUR HUSBAND” (MUME WAKO.) aliyasoma maneno haya mara mbilimbili, hakutaka kuamini hata kidogo kile alichokuwa akikiona kwa wakati huo.

Kitendo cha kuziona picha za mpenzi wake akiwa amelala kitandani na Monalisa hakika zilimuumiza mno moyo wake, alihisi kupata maumivu makali asiyoyatarajia kwa wakati huo.
 
Sehemuya 20.

Kila kitu alichokuwa akikiona katika picha hizo kilimfanya abaki katika wakati wa maumivu mno. Machozi yalianza kumbubujika mashavuni mwake, akajaribu kuyafuta lakini huo haukuwa ndiyo mwisho wa kuyamaliza, yalizidi kumbubujika mfululizo bila kukoma.

Hakukuwa na kitu kingine kilichokuwa kikimuumiza moyo wake zaidi ya usaliti, alisalitiwa na mpenzi wake ambaye alikuwa akimpenda sana.

Alikumbuka mambo mengi waliyowahi kuyafanya na Richard katika mapenzi yao lakini mambo yote hayo yalibaki kuwa hayana mashiko yoyote.

Muda huo ambao alikuwa katika maumivu ghafla! simu yake ikawa inaita, alipaitazama mpigaji wa simu hiyo aliliona jina la Mama Richard, hakutaka kupokea, aliamini Richard ndiye aliyekuwa akimpigia. Hakutaka kuzungumza naye lolote hivyo aliamua kuiacha simu iendelee kuita mpaka pale ilipokata. Aliendelea kulia huku akiwa ameukumbatia mto pale kitandani. ****

Monalisa alikuwa katika furaha isiyokuwa na kifani, muda wote alikuwa ni mtu wa kucheka peke yake baada ya kufanikiwa kumtumia picha Evelyne. Aliamini picha hizo lazima zingeweza kuliua penzi kati ya Richard na Evelyne na hiyo ndiyo sababu iliyomfanya azidi kubaki akiwa ni mtu mwenye furaha muda wote.

Aliamini hakuwa na sababu ya kuendelea kulia au kuumia tena kwani mwanaume aliyekuwa akimuhitaji tayari alikuwa ni wake, hilo lilizidi kumfurahisha mno.

“Amekujibu lolote mpaka sasa baada ya kumtumia hizo picha?” aliuliza Adela.
“Hapana bado hajanijibu ila amezipokea tayari,” alijibu Monalisa huku akitabasamu.

“Hivi umejiamini nini mpaka ukaamua kuzipiga hizo picha?”
“Nampenda sana Richard, nimeshindwa kujizuia kwa kweli imenibidi nifanye hivyo,” alijibu Monalisa.

Monalisa aliendelea kuushikilia msimamo wake wa kumpenda Richard, muda mwingine aliamini kwa tukio alilokuwa amelifanya la kumtumia picha za utupu Evelyne ni lazima zingeweza kuwagombanisha wawili hao na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kulifaidi penzi la Richard kwa uhuru.

Alichokuwa anakihitaji ni kuwa na Richard bila kujali maumivu ambayo alikuwa anaenda kuwapa wawili hao waliyokuwa wanapendana kwa dhati.
 
Sehemu ya 21.

Adela ndiye alikuwa msichana pekee ambaye alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea kuhusiana na picha ambazo alikuwa amezipiga Monalisa na Richard.

Monalisa aliamua kumuonyesha Adela picha hizo huku akiwaficha Penina na Mary, hakutaka wafahamu lolote zaidi ya uhusiano wake na Richard tu.
“Kwanini nisiwaambie?” aliuliza Adela huku akionekana kushangazwa mno.

“Sitaki uwaambie lolote kuhusiana na hizi picha nilizozipiga,”alijibu Monalisa huku akimtazama kwa macho ya msisitizo Adela.
“Kuna kitu gani kinachoendelea kati yenu?”

“Hakuna.”
“Sasa kwanini hutaki niwaambie?”
“Nimeamua tu kwani picha ni zangu au za kwao?” “Una uhakika hakuna tatizo?”
“Ndiyo hakuna,” alijibu Monalisa.

Waliendelea kuzungumza wakati huo Penina na Mary hawakuwepo hostel, mpaka kufikia muda huo Adela hakujua ni nini kilichokuwa kikiendelea mpaka Monalisa aamue kuwaficha Penina na Mary na wakati wote walikuwa ni marafiki na kila jambo ambalo alikuwa akilifanya ilikuwa ni lazima awaambie, hilo lilizidi kumchanganya kichwa chake. ****
Siku iliyofuata ndiyo ilikuwa ile siku ambayo Evelyne alishindwa kuendelea kubaki darasani baada ya kumuona Richard akiwa ameingia, alishindwa kuyavumilia maumivu ambayo moyo wake tayari ulikuwa umshayapata, alimchukia mno Richard na hakutaka kuendelea kumtazama katika mboni za macho yake.

Alichoamua kukifanya ni kuondoka kabisa eneo hilo la chuo huku akiamini kwa kufanya hivyo angeweza kuyapooza maumivu na machungu ambayo moyo wake ulikuwa ukipitia..

Rafiki yake Happy hakuwa anafahamu lolote lile lililokuwa limetokea, alibaki katika wakati mgumu baada ya Evelyne kushindwa kumuelezea ni nini kilichokuwa kimetokea na kwa wakati huo aliamua kuondoka zake.

Alitamani sana kufahamu ni nini kilichokuwa kimetokea na mtu pekee ambaye aliamini angeweza kumueleza ukweli wa mambo yote hayo alikuwa ni Richard lakini na yeye alishindwa kumueleza ukweli, alibaki akiwa haelewi ni nini kilichokuwa kimetokea baada ya kumuona mpenzi wake akiwa ameondoka.
*
*
Je, nini kitaendelea?
 
[emoji8] [emoji8] [emoji8]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu ya 22.

“Unasema amerudi nyumbani?” aliuliza Richard huku akionekana kuwa mwenye wasiwasi.
“Ndiyo,” alijibu Happy.

“Kigamboni au?” aliuliza Richard.
“Richard inamaana hujui Evelyne anapoishi?” aliuliza Happy huku akionekana kumshangaa Richard kwa wakati huo.

“Hapana, nafahamu ila nimechanganyikiwa,” alijibu Richard.
“Halafu mbona jana ulikuwa unapigiwa simu hupatikani?” aliuliza Happy.

Richard alianza kukumbuka tukio la Monalisa kuichukua simu yake, alishindwa kutoa jibu la haraka, alibaki mithili ya mtu ambaye alikuwa akitafakari jambo na mwisho lilimjia jibu la kudanganya.
“Nimeibiwa,” alijibu.

Happy alianza kuingiwa na wasiwasi baada ya kumuona Richard akionekana kuficha ukweli wa jambo ambalo alihitaji kulifahamu, aliamini Richard alikuwa akifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea lakini alishindwa kujua alitakiwa aanzie wapi kumuhoji ili aweze kumwambia.

“Una uhakika na unayonieleza?”
“Ndiyo nina uhakika,” alijibu Richard huku kijasho chembamba kikianza kumtoka mwilini.

Richard alishindwa kuzungumza ukweli kwasababu mpaka kufikia wakati huo hakujua ni nini kilichokuwa kimetokea, kuna muda alianza kuhisi labda Monalisa aliamua kumueleza ukweli Evelyne wa kile kilichokuwa kimetokea kati yao na hiyo ndiyo ilikuwa sababu iliyomfanya mpaka abadilike.

Lilipomtoka wazo hilo liliingiwa wazo lingine hivyo alishindwa kabisa kuelewa ni nini ambacho alitakiwa kuzungumza.

“Unajua Richard sikuelewi unachokizungumza?”
“Hunielewi nini?”

“Mimi nahisi utakuwa unafahamu kila kitu kwasababu haiwezekani Evelyne halafu abadilike bila sababu.”
“Kama ningekuwa ninafahamu ukweli ningekueleza sasa kwanini nikufiche na kwanini nikufiche?”

“Namfahamu sana Evelyne mimi naamini kuna kitu kati yenu kimetokea.”
“Kitu gani?”
“Sikifahamu,” alijibu Happy.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom