Nisamehe Mpenzi

Nisamehe Mpenzi

Sehemu ya 41.

“Atokee wapi wakati tayari nipo na wewe.”
“Fredrick niambie ukweli usinidanganye.”
“Niamini upo peke yako katika moyo wangu,” alisema Fredrick.

Kila maneno aliyokuwa akiyasema Fredrick yalizidi kumteka Evelyne, alijikuta akikosa la kusema, alibaki akimtazama mwanaume huyo ambaye alitofautiana mambo mengi sana na Richard. ****

Monalisa hakuishia kumpenda Richard pale chuoni, kila mwanaume mwenye pesa na muonekano mzuri ambaye alijitokeza mbele yake alikuwa akianzisha mahusiano naye na hiyo ndiyo ilikuwa tabia yake. Hakukuwa na watu waliyokuwa wakifahamu hilo zaidi ya marafiki zake Penina, Adela pamoja na Mary.

Tabia yake hiyo ya kuwachanganya wanaume ndiyo iliyosababisha mpaka akapata mimba ambayo hakuwa anamfahamu baba halisi, hakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya msingizia mimba hiyo Richard mwanaume ambaye tayari alikuwa ameshafanya naye mapenzi.

Richard baada ya kupewa taarifa hizo za ujauzito hakutaka kukataa, alikubali huku akiamini ulikuwa ni ujauzito wake.

Hakutaka kuamini kama kweli alikuwa amempa ujauzito msichana huyo ambaye moyo wake haukumpenda, alizidi kujilaumu mno baada ya kukumbuka kuwa msichana huyo ndiye alikuwa sababu ya kumgombanisha na mpenzi wake na kwa wakati huo tayari alikuwa ameanzisha mahusiano na mwanaume mwingine.

Tukio hilo bado liliendelea kumuumiza sana moyo wake, hakutaka kuamini kile kilichokuwa kimetokea, alihisi alikuwa katika ndoto lakini haikuwa hivyo, kila kitu kilichokuwa kimetokea ndiyo ulikuwa ukweli halisi.

Alitamani kuwaeleza ukweli wazazi wake kwa kile kilichokuwa kimetokea kuhusu Monalisa mpaka kufikia hatua ya kumpa ujauzito lakini alipokumbuka maswali ambayo angeweza kuulizwa na Mama yake kuhusu Evelyne alighairi kufanya hivyo.

Alipokuwa akimuona Monalisa chuoni moyo wake ulizidi kumchukia, alimuona kuwa msichana aliyeyaharibu mahusiano yake na mpenzi wake, kitu kibaya zaidi alikuwa ameubeba ujauzito wake na hilo ndilo lilizidi kumchanganya akili yake bila kujua kuwa alisingiziwa ujauzito huo haukuwa ni wake.
 
Sehemu ya 42.

****
Penzi kati ya Fredrick na Evelyne lilizidi kupamba moto, hakukuwa na tatizo lolote kati yao, tangu walipoweza kukutana siku ya kwanza mapenzi yao yalizidi kuongezeka.

Fredrick alikuwa ni mwanaume wa tofauti sana, alifanya kila awezalo ilimradi ahakikishe msichana huyo anapata furaha, hakutaka kuona anakuwa sababu ya kumuumiza bila sababu, hakutaka kuona tukio hilo linatokea hata mara moja, alihakikisha anamtimizia kila kitu alichokuwa akikihitaji katika mapenzi, hata hivyo mbali na yote hayo ndoto yake kubwa ilikuwa ni siku moja kuja kufunga pingu za maisha na msichana huyo pale pindi ambapo angeweza kumaliza chuo na kufanikiwa kupata kazi.

Evelyne alizidi kutekwa na mapenzi ya Fredrick, muda wote furaha ndiyo ilikuwa imemtawala, hakuona sababu ya kuyachukia tena mapenzi, aliyapenda na moyo wake ulikuwa ukimpenda Fredrick tu.

“Una nini wewe mbona unacheka mwenyewe?” aliuliza Happy.
“Hakuna kitu,” alijibu Evelyne.
“Umeanza kuchanganyikiwa?”
“Hapana kuna kitu nimekikumbuka ndiyo kimefanya nimecheka.”

“Kitu gani?”
“Ni kuhusu Fredrick.”
“Mwenzetu ndiyo tayari umeshakolea kiasi hicho?”

“Yeah! nampenda sana na ninaimani hata yeye pia ananipenda.”
“Unajua siku hizi umebadilika sana tofauti na siku zote.”
“Nimekuwaje?”
“Umekuwa ni mtu wa kufurahi tu kila wakati.”

“Nimeipata furaha, nimeipata amani sasa kwanini nisifurahie?”
“Kweli huyo mwanaume amekuteka,” aliniambia Happy. ****

Adela alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha ya Monalisa, hakuipenda tabia ya rafiki yake huyo ambaye kila mwanaume mwenye pesa na muonekano mzuri aliyejitokeza mbele yake alikuwa akianzisha mahusiano naye.

Alikuwa ametembea na wanaume wengi sana na mpaka kufikia wakati huo alikuwa amepata ujauzito na hakujua ulikuwa ni wa nani zaidi alichoamua kukifanya nikumsingizia Richard kwa kuwa tayari alikuwa ameshalala naye, alihitaji kutumia pesa zake.

Alichoamua kukifanya Adela ni kutafuta muda wa kukutana na Richard kisha akahitaji kumueleza kila kitu kilichokuwa kikiendelea.
 
Sehemu ya 43.

“Kuna nini?” aliuliza Richard.
“Nahitaji kuzungumza na wewe,” alijibu Adela.
“Ni mazungumzo ya umuhimu?” aliuliza Richard.

“Ndiyo ni muhimu sana,” alijibu Adela.
Baada ya kujibiwa hivyo Richard hakutaka kupoteza muda alichoamua kukifanya ni kumpa nafasi msichana huyo ya kumsikiliza kile alichokuwa amedhamiria kumwambia kwa wakati huo.
“Ok, nakusikiliza niambie,” alisema Richard.

“Richard najua unatembea na rafiki yangu, hilo sio jambo la siri tena ila kuna kitu kimoja nahisi haukifahamu na kinaniumiza sana,” alisema Adela.
“Kitu gani?” aliuliza Richard.

“Monalisa hakupendi isipokuwa amekutamani, tamaa zake za kimwili ndiyo zimempelekea mpaka akakuharibia mahusiano yako,” alijibu Adela huku akionyesha msisitizo wa maneno yake.

“Mbona sijakuelewa ni nini unachokimaanisha?” aliuliza Richard.
“Monalisa sio msichana sahihi kwako, hastahili kuwa mpenzi wako ni muuaji yule,” alijibu Adela.

“Bado sijakuelewa.”
“Ninachotaka kukuambia ni kwamba ule ujauzito wa Monalisa sio wako,” alisema Adela.

Maneno hayo yalimchanganya sana Richard, alishindwa kuelewa ukweli wa maneno yale, kama ule haukuwa ujauzito wake ulikuwa ni wa nani. Hili ndilo lilikuwa swali pekee lililokuwa linamuumiza kichwa chake, hakujua nyuma ya pazia kama alishiriki mapenzi na msichana ambaye kwake kitendo cha kuwabadilisha wanaume kama nguo kilikuwa ni cha kawaida.

“Unasemaje?” aliuliza kwa mshangao.
“Huo ndiyo ukweli,” alijibu Adela lakini kama haitoshi aliamua kumsimulia kila kitu kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia. ****

Taarifa za ujauzito wa Monalisa zilisambaa chuo kizima, hakukuwa na siri juu ya uhusiano wake na Richard, kila mtu alifahamu kuhusu habari za wawili hao. Waliyomfahamu Richard walimlaumu sana kwa kitendo alichokuwa amekifanya cha kumsaliti mpenzi wake kisha akaanzisha mahusiano na msichana mwingine ambaye tayari alikuwa amembebesha ujauzito. Jambo hilo lilizidi kumfanya achukiwe na baadhi ya watu.
 
Sehemu ya 44.

“Jamaa karuka mkoja kakanyaga mavi,” alisema mwanachuo mmoja.
“Hili ndilo tatizo letu sisi wanaume hatuwezi kutulia na mwanaume mmoja,” alisema mwanachuo mwingine.
Hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiwakasirisha watu kama kusikia kuwa msichana huyo aliyelisambaratisha penzi la Evelyne alikuwa amebeba ujauzito.

Baada ya kuzisikia taarifa hizo Happy na yeye alianza kumchukia Richard, hakutaka kuzungumza naye, aliamua kuwa upande wa rafiki yake na kuanzia siku hiyo alimuunga mkono kwa uamuzi aliyokuwa ameuchukua wa kuanzisha mahusiano na Fredrick.

Alifahamu ni maumivu kiasi gani aliyokuwa ameyapata hivyo kwa uamuzi aliyokuwa ameuchukua aliamini uliweza kumpunguzia maumivu hayo.

“Yaani pamoja na uchafu aliyoufanya ameona haitoshi ameamua bora ampe ujauzito kabisa,” alisema Happy.
“Wanaume ndivyo walivyo hawaridhiki,” alisema Evelyne.
“Nimemchukia sana.”

“Sio wewe tu hata mimi sitaki kuzungumza naye,” alisema Evelyne.
Mpaka kufikia hapo hakukuwa na mtu aliyefahamu ni nini kilichokuwa kikiendelea, wanachuo walimchukia sana Richard kwa ujinga aliyokuwa ameufanya wa kumsaliti mpenzi wake.

Ilikuwa imebakia miezi miwili ili waweze kufanya mitihani ya kumaliza degree yao, kila mwanachuo alionekana kuwa bize na kusoma kwa ajili ya kujiandaa na mitihani hiyo.

Kwa upande wa Richard hali ilikuwa tofauti, alijitahidi kujisomea lakini badala ya kuelewa alichokuwa akikisoma ndiyo kwanza mawazo yake yalikuwa yakitafakari ukweli aliyoelezwa na Adela kuhusu ujauzito wa Monalisa.

Alihisi kuchanganyikiwa kila alipokuwa akiyakumbuka maneno ya Adela, alitumia pesa nyingi mno kwa ajili ya Monalisa, hakutaka kuamini kama msichana huyo aliyedai kuwa anaujauzito wake hakuwa muaminifu, alishiriki mapenzi na wanaume wengi na mpaka kufikia wakati huo ujauzito haukuwa ni wake.

Hilo liliendelea kumuumiza sana moyo wake, alijiona kuwa mwanaume mwenye mikosi kila kukicha.
*
*
Je, nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 41.

“Atokee wapi wakati tayari nipo na wewe.”
“Fredrick niambie ukweli usinidanganye.”
“Niamini upo peke yako katika moyo wangu,” alisema Fredrick.

Kila maneno aliyokuwa akiyasema Fredrick yalizidi kumteka Evelyne, alijikuta akikosa la kusema, alibaki akimtazama mwanaume huyo ambaye alitofautiana mambo mengi sana na Richard. ****

Monalisa hakuishia kumpenda Richard pale chuoni, kila mwanaume mwenye pesa na muonekano mzuri ambaye alijitokeza mbele yake alikuwa akianzisha mahusiano naye na hiyo ndiyo ilikuwa tabia yake. Hakukuwa na watu waliyokuwa wakifahamu hilo zaidi ya marafiki zake Penina, Adela pamoja na Mary.

Tabia yake hiyo ya kuwachanganya wanaume ndiyo iliyosababisha mpaka akapata mimba ambayo hakuwa anamfahamu baba halisi, hakuwa na njia nyingine ya kufanya zaidi ya msingizia mimba hiyo Richard mwanaume ambaye tayari alikuwa ameshafanya naye mapenzi.

Richard baada ya kupewa taarifa hizo za ujauzito hakutaka kukataa, alikubali huku akiamini ulikuwa ni ujauzito wake.

Hakutaka kuamini kama kweli alikuwa amempa ujauzito msichana huyo ambaye moyo wake haukumpenda, alizidi kujilaumu mno baada ya kukumbuka kuwa msichana huyo ndiye alikuwa sababu ya kumgombanisha na mpenzi wake na kwa wakati huo tayari alikuwa ameanzisha mahusiano na mwanaume mwingine.

Tukio hilo bado liliendelea kumuumiza sana moyo wake, hakutaka kuamini kile kilichokuwa kimetokea, alihisi alikuwa katika ndoto lakini haikuwa hivyo, kila kitu kilichokuwa kimetokea ndiyo ulikuwa ukweli halisi.

Alitamani kuwaeleza ukweli wazazi wake kwa kile kilichokuwa kimetokea kuhusu Monalisa mpaka kufikia hatua ya kumpa ujauzito lakini alipokumbuka maswali ambayo angeweza kuulizwa na Mama yake kuhusu Evelyne alighairi kufanya hivyo.

Alipokuwa akimuona Monalisa chuoni moyo wake ulizidi kumchukia, alimuona kuwa msichana aliyeyaharibu mahusiano yake na mpenzi wake, kitu kibaya zaidi alikuwa ameubeba ujauzito wake na hilo ndilo lilizidi kumchanganya akili yake bila kujua kuwa alisingiziwa ujauzito huo haukuwa ni wake.
Shunie unantengaa jamani, sikujua kama umeiendeleza

the Legend☆
 
Sehemu ya 44.

“Jamaa karuka mkoja kakanyaga mavi,” alisema mwanachuo mmoja.
“Hili ndilo tatizo letu sisi wanaume hatuwezi kutulia na mwanaume mmoja,” alisema mwanachuo mwingine.
Hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiwakasirisha watu kama kusikia kuwa msichana huyo aliyelisambaratisha penzi la Evelyne alikuwa amebeba ujauzito.

Baada ya kuzisikia taarifa hizo Happy na yeye alianza kumchukia Richard, hakutaka kuzungumza naye, aliamua kuwa upande wa rafiki yake na kuanzia siku hiyo alimuunga mkono kwa uamuzi aliyokuwa ameuchukua wa kuanzisha mahusiano na Fredrick.

Alifahamu ni maumivu kiasi gani aliyokuwa ameyapata hivyo kwa uamuzi aliyokuwa ameuchukua aliamini uliweza kumpunguzia maumivu hayo.

“Yaani pamoja na uchafu aliyoufanya ameona haitoshi ameamua bora ampe ujauzito kabisa,” alisema Happy.
“Wanaume ndivyo walivyo hawaridhiki,” alisema Evelyne.
“Nimemchukia sana.”

“Sio wewe tu hata mimi sitaki kuzungumza naye,” alisema Evelyne.
Mpaka kufikia hapo hakukuwa na mtu aliyefahamu ni nini kilichokuwa kikiendelea, wanachuo walimchukia sana Richard kwa ujinga aliyokuwa ameufanya wa kumsaliti mpenzi wake.

Ilikuwa imebakia miezi miwili ili waweze kufanya mitihani ya kumaliza degree yao, kila mwanachuo alionekana kuwa bize na kusoma kwa ajili ya kujiandaa na mitihani hiyo.

Kwa upande wa Richard hali ilikuwa tofauti, alijitahidi kujisomea lakini badala ya kuelewa alichokuwa akikisoma ndiyo kwanza mawazo yake yalikuwa yakitafakari ukweli aliyoelezwa na Adela kuhusu ujauzito wa Monalisa.

Alihisi kuchanganyikiwa kila alipokuwa akiyakumbuka maneno ya Adela, alitumia pesa nyingi mno kwa ajili ya Monalisa, hakutaka kuamini kama msichana huyo aliyedai kuwa anaujauzito wake hakuwa muaminifu, alishiriki mapenzi na wanaume wengi na mpaka kufikia wakati huo ujauzito haukuwa ni wake.

Hilo liliendelea kumuumiza sana moyo wake, alijiona kuwa mwanaume mwenye mikosi kila kukicha.
*
*
Je, nini kitaendelea?
Daah, sijui nini kitatokea. Richard alibugi sana kukubali kutembea na Monalisa, angebaki na msimamo wake yote yasingetokea. Asante Shunie

the Legend☆
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom