Niolewe na yupi - ushauri wako ni muhimu

Niolewe na yupi - ushauri wako ni muhimu

Ahsante! Chanzo cha kuvunjika kwa ndoa nakifahamu, tatizo lilikuwa kwa my x. Ndo ya kikristo inaweza kuvunjika kwa sababu, mtume Paulo ktk kitabu cha Wakoritho amesema sababu ya kuvunja ndoa
Pole bidada!
Kabla hujachagua tafadhari jiulize chanzo cha ku-divorce; ni wewe au x-husband?
Kama ni wewe, umebadilika?
Kama hujabadilika, hao wa3 wako tayari kuvumilia mapungufu yako?
Kama tatizo lilikuwa mmeo, je hao wachumba hawana hizo tabia, kama wanazo uko tayari kuwavumilia?
***Mind you, ndoa ya kikristu haivunjwi ila kwa kifo***
 
Hivi ni wachungaji wa kanisa gani hao waliokuruhusu utafute bwana mwingine wakukuweka ndani wakati yule uliyefunga ndoa naye awali yu ngali hai?

Je hawajakueleza ya kwamba hilo utakalo kufanya mbele za Mungu lahesabika kama zinaa?

Au hata wewe mwenyewe kwa utashi wako huoni kama hilo ni kosa kwa kukiuka kile kiapo cha hadi kifo kiwatenganishe?

Je hao unaotaka wakuoe nao wakigeuka mbogo nako huko utakimbilia kuachika na kutafuta bwana mwingine?

Ndio shida hii ya kukimbilia kuolewa na mtu ambaye huenda Mungu hakupanga awe mumeo isipokuwa kwa kiherehere cha kibinadamu ukafanya ya kufanya.

Mtu yoyote ataye kushauri uolewe tena wakati mumeo wa ndoa ya mwanzo yu ngali hai basi mtu huyo atakuwa kakupotosha na kukufanya ushiriki zinaa.

Mkuu kuachana kupo "usiwasikilize tu viongozi wako wa dini jaribu kufuatilia maandiko"
 
We dada mleta mada ni fisadi wa mapenzi yaani wachumba watatu wote!!! Tena baada ya shortlisting!!! Wakati wenzio hawana hata mmoja. Kuna member anapenda huu msemo,'Wonders shall never end'!!!
 
yupi kati ya hao anatoka masanza kona?
 
Kwanza na mshukuru Mungu kwa rehema na baraka mbali mbali anazonijalia katika maisha yangu kila iitwapo leo.

Wana-MMU ninakuja kwenu nikihitaji ushauri juu ya hili suala, kiukweli maisha ya upweke yamenichosha, hii ni baada ya kudivorce na aliyekuwa mume wangu 2007. Mimi ni mama nina watoto wawili, 36yrs, mkristo. Nina nyumba yangu mwenyewe na asset kadhaa, baada ya kuchoshwa na upweke nimeona ni wakati muafaka wa kupata mwenzi mwingine. Nayamudu maisha yangu vizuri tu tatizo ni huo upweke tu, so naombeni mnishauri kuhusu hawa watu hapa chini.


1. Huyu ni mkaka 38yrs hajawahi kuoa ila ana mtoto mmoja, ni mafanyabiashara lakini pia ni mwanafunzi wa chuo fulani hapa nchini. Ana kiwanja, hajajenga so anaishi nyumba ya kupanga, ameonesha nia ya dhati ya kutaka kuishi na mimi pamoja na watoto wangu ila atapenda pia nimzalie watoto wawili. Nikifikiria hapo pa kuzaa watoto wawili nachanganyikiwa kabisa

2. Huyu ni mkaka, 36yrs, hajawahi kuoa ila na mtoto mmoja, ni mwajiriwa kwenye NGO na anasoma online chuo kikuu kimoja huko marekani. Ndio kwanza ameanza ujenzi wa nyumba yake, ananipenda mimi na watoto wangu, nae anapenda Mungu akijalia nimzalie watoto wawili. Hapo kwenye kuzaa nachanganyikiwa lkn pia namuona bado ana ujana mwingi

3. Huyu ni baba, 45yrs, ana familia yake, ana mke na watoto 3, ameajiriwa ofisi ya mtu binafsi, ana nyumba kadhaa, ananipenda kwa dhati, anaipenda familia yangu sana na anajitoa kwa hali na mali, kama tukioana anapenda nimzalie mtoto mmoja tu. Naweza kumzalia mtoto mmoja kama Mungu atapenda, tatizo ni hiyo familia na dini, yeye ni muislam, so anataka mimi niwe bi mdogo

Ushauri wako please, ukiona haikuhusu tafadhali potezea

Hao watoto wawili ni baba mmoja?
 
Hapo kila mmoja anazani yuko peke yake!! Wote hao wa kazi gani?
USITHUBUTU KUMWAMINI MWANAMKE.
Samahan lakini.
Mkuu acha tu, huyu mleta mada amenichanganya sana. Hao wote amewatenga kimafungu, kazi ipo.
 
Bado ni marafiki tu, tena marafiki wa kawaida, ndo nikimpata mmoja atakuwa mchumba then mume


nakushauri kitu cha muhimu, usiolewe na mume wa mtu. hata kama yeye dini yake inamruhusu, kiukweli mi ni muislamu lkn uke wenza siwezi..kumbuka utakavyomuumiza mwanamke mwenzako, na jiweke wewe kwenye position yake uone kama ungeweza..utavuruga familia ya watu na kuharibu ndoa ya watu, kwa nini wakati kuna option zingine..

ukishaanza kuolewa mke wa pili basi jiandae kwa mambo ya ushirikina na vituko visvoisha, usitegemee kama huyo mke waliyeanza naye maisha na kufika kote huko kama atakubali kirahisi tu..ujue na yeye atahangaika..

ukiolewa na huyu mume wa mtu hutaishi kwa amani japo kuwa mtakuwa na kila kitu..

mimi naona huyu wa 38 years anaweza kukufaa, usiangalie mali wala ana nini, kwani we shida yako mali? si ushasema unazo na ukasema wewe unataka mume..sasa usiangalie ana nini kama unampenda akuoe halafu mjue mnatafuta vipi hizo kwa joint effort..na ndoa yenye baraka ni bora kuliko kuwa na mali nyingi halafu huna amani..
 
Nakuheshimu sana Dr, kwa hili labda uende kwenye maandiko tu, kasome Wakoritho wa kwanza, zipo sababu za kuvunja ndoa

Nipe sababu za kuolewa kwa mara ya pili, maana hiyo ya kuachana tayari naifahamu...

Kwa maana nijuavyo hicho kitabu ulichokitaja kinatamka kama ifuatavyo...

1 Kor 7
10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
 
We dada mleta mada ni fisadi wa mapenzi yaani wachumba watatu wote!!! Tena baada ya shortlisting!!! Wakati wenzio hawana hata mmoja. Kuna member anapenda huu msemo,'Wonders shall never end'!!!
hahahah wonders shall never end!mhh
 
Mhmm! Inaonekana ni tabia yako,kuchepuka. Rudi kwa mumeo. Acha kuchepusha wenzii hasa huyo mkaka mwenye mke.
 
watu8, sijaachana na mume wangu ili niolewe na mwanaume mwingine, naka kuolewa ningeshaolewa siku nyingi tu, kumbuka nimedivorce 2007 hadi leo ni miaka mingapi?

Kuacha kunaruhusiwa pale inapobidi kufanya hivyo, sina sababu ya kusema hapa why tuliachana lakini nikwambie tu tatizo lilikuwa kubwa, wachungaji, hadi askofu aliingilia kati lakini ilishindikana


Sijapinga kuachana bali unaachana na mtu halafu unaenda kuolewa au kuoa mwingine...hiyo sio sawa
 
Last edited by a moderator:
Shangaa na wewe ndugu yangu


Ila watu tumerahisisha sana ngono. Nimesoma baadhi ya majibu naona kuna watu wengi tu wameshamhukumu mleta mada kuwa tayari anagegedwa na hao jamaa watatu. Mimi nimebaki najiuliza tu, hivi ni kwa nini kuna watu wengi wamefikia hitimisho hilo, hivi siku hizi haiwezekani kuwa na uhusiano bila ngono??
 
na wewe unampenda yupi...?naona unayapa kipaumbele mambo ya "ana nyumba" na "anataka nimzalie watoto wawili" kipaumbele kuliko furaha ya moyo wako..
 
na wewe unampenda yupi...?naona unayapa kipaumbele mambo ya "ana nyumba" na "anataka nimzalie watoto wawili" kipaumbele kuliko furaha ya moyo wako..kama ukikosa furaha na amani hivyo vingine vyote havina maana...
 
Nimekuwa fisadi tena, kwani kupendwa na mtu una tuma maombi kakangu, hao ambao hawana wasubiri yu siku itafika nao watapendwa


We dada mleta mada ni fisadi wa mapenzi yaani wachumba watatu wote!!! Tena baada ya shortlisting!!! Wakati wenzio hawana hata mmoja. Kuna member anapenda huu msemo,'Wonders shall never end'!!!
 
Back
Top Bottom