masanzakona
JF-Expert Member
- Jan 2, 2014
- 228
- 121
Kwanza na mshukuru Mungu kwa rehema na baraka mbali mbali anazonijalia katika maisha yangu kila iitwapo leo.
Wana-MMU ninakuja kwenu nikihitaji ushauri juu ya hili suala, kiukweli maisha ya upweke yamenichosha, hii ni baada ya kudivorce na aliyekuwa mume wangu 2007. Mimi ni mama nina watoto wawili, 36yrs, mkristo. Nina nyumba yangu mwenyewe na asset kadhaa, baada ya kuchoshwa na upweke nimeona ni wakati muafaka wa kupata mwenzi mwingine. Nayamudu maisha yangu vizuri tu tatizo ni huo upweke tu, so naombeni mnishauri kuhusu hawa watu hapa chini.
1. Huyu ni mkaka 38yrs hajawahi kuoa ila ana mtoto mmoja, ni mafanyabiashara lakini pia ni mwanafunzi wa chuo fulani hapa nchini. Ana kiwanja, hajajenga so anaishi nyumba ya kupanga, ameonesha nia ya dhati ya kutaka kuishi na mimi pamoja na watoto wangu ila atapenda pia nimzalie watoto wawili. Nikifikiria hapo pa kuzaa watoto wawili nachanganyikiwa kabisa
2. Huyu ni mkaka, 36yrs, hajawahi kuoa ila na mtoto mmoja, ni mwajiriwa kwenye NGO na anasoma online chuo kikuu kimoja huko marekani. Ndio kwanza ameanza ujenzi wa nyumba yake, ananipenda mimi na watoto wangu, nae anapenda Mungu akijalia nimzalie watoto wawili. Hapo kwenye kuzaa nachanganyikiwa lkn pia namuona bado ana ujana mwingi
3. Huyu ni baba, 45yrs, ana familia yake, ana mke na watoto 3, ameajiriwa ofisi ya mtu binafsi, ana nyumba kadhaa, ananipenda kwa dhati, anaipenda familia yangu sana na anajitoa kwa hali na mali, kama tukioana anapenda nimzalie mtoto mmoja tu. Naweza kumzalia mtoto mmoja kama Mungu atapenda, tatizo ni hiyo familia na dini, yeye ni muislam, so anataka mimi niwe bi mdogo
Ushauri wako please, ukiona haikuhusu tafadhali potezea