Niolewe na yupi - ushauri wako ni muhimu

Kwanza na mshukuru Mungu kwa rehema na baraka mbali mbali anazonijalia katika maisha yangu kila iitwapo leo.

Wana-MMU ninakuja kwenu nikihitaji ushauri juu ya hili suala, kiukweli maisha ya upweke yamenichosha, hii ni baada ya kudivorce na aliyekuwa mume wangu 2007. Mimi ni mama nina watoto wawili, 36yrs, mkristo. Nina nyumba yangu mwenyewe na asset kadhaa, baada ya kuchoshwa na upweke nimeona ni wakati muafaka wa kupata mwenzi mwingine. Nayamudu maisha yangu vizuri tu tatizo ni huo upweke tu, so naombeni mnishauri kuhusu hawa watu hapa chini.

1. Huyu ni mkaka 38yrs hajawahi kuoa ila ana mtoto mmoja, ni mafanyabiashara lakini pia ni mwanafunzi wa chuo fulani hapa nchini. Ana kiwanja, hajajenga so anaishi nyumba ya kupanga, ameonesha nia ya dhati ya kutaka kuishi na mimi pamoja na watoto wangu ila atapenda pia nimzalie watoto wawili. Nikifikiria hapo pa kuzaa watoto wawili nachanganyikiwa kabisa

2. Huyu ni mkaka, 36yrs, hajawahi kuoa ila na mtoto mmoja, ni mwajiriwa kwenye NGO na anasoma online chuo kikuu kimoja huko marekani. Ndio kwanza ameanza ujenzi wa nyumba yake, ananipenda mimi na watoto wangu, nae anapenda Mungu akijalia nimzalie watoto wawili. Hapo kwenye kuzaa nachanganyikiwa lkn pia namuona bado ana ujana mwingi

3. Huyu ni baba, 45yrs, ana familia yake, ana mke na watoto 3, ameajiriwa ofisi ya mtu binafsi, ana nyumba kadhaa, ananipenda kwa dhati, anaipenda familia yangu sana na anajitoa kwa hali na mali, kama tukioana anapenda nimzalie mtoto mmoja tu. Naweza kumzalia mtoto mmoja kama Mungu atapenda, tatizo ni hiyo familia na dini, yeye ni muislam, so anataka mimi niwe bi mdogo

Ushauri wako please, ukiona haikuhusu tafadhali potezea

Kabla sijatoa ushauri. Je hao wote watatu huwa unafanya nao tendo la ndoa simultaneously?
 
watu8, sijaachana na mume wangu ili niolewe na mwanaume mwingine, naka kuolewa ningeshaolewa siku nyingi tu, kumbuka nimedivorce 2007 hadi leo ni miaka mingapi?

Hakuna mahali nilipokushutumu kuwa umeachana na aliyekuwa mumeo ili ufunge ndoa na mwanaume mwingine...

Ninachojaribu kuweka sawa hapa ni kuwa kwa mkristo, haijalishi umeachana lini na mumeo suala la kuolewa au kuoa tena na mtu mwingine linakatazwa na ndio maana nilikupa nukuu ya maandiko...

Narudia tena kuweka nukuu ile ile ya mwanzo:
1 Kor 7
10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.

Hayo maandiko yanaagiza ukae na usiolewe tena maana option namba mbili ya kupatana kwenu imeshashindikana...

Kuacha kunaruhusiwa pale inapobidi kufanya hivyo, sina sababu ya kusema hapa why tuliachana lakini nikwambie tu tatizo lilikuwa kubwa, wachungaji, hadi askofu aliingilia kati lakini ilishindikana

Biblia inaelezea sababu moja tu ambayo ni halali kwa wanandoa kutengana kwa talaka (tamko la kuachana), na sababu hiyo ni zinaa au uasherati pekee.
 
je hao wate kwanza unawapangiaje ratiba ya kukutana nao bila ya kuonana .....?
 
Nilichogundua hapa kwenye uzi wa dada yetu,ni kuwa kuwa na nyumba ni principal qualification then vinafuata vingine. Soma maandiko yake vizuri utaona.
 
Ila nina swali moja tu kwako mleta mada. Hivi wakati unaolewa kwa mara ya kwanza tayari ulishajenga hiyo nyumba yako?
 
Asset nilizonazo ikiwemo na nyumba, nimezipata baada ya kuwa nimeachana na mume wangu. Na tulivyoachana sikuchukua chochote ktk tulivyopata wakati wa ndoa yetu, nilimwachia kila kitu niliondoka na watoto wangu tu

Ila nina swali moja tu kwako mleta mada. Hivi wakati unaolewa kwa mara ya kwanza tayari ulishajenga hiyo nyumba yako?
 
Nyumba sio principle, kuna wanaume wengine hawapendi kwenda kuishi katika nyumba iliyojengwa na mwanamke

Nilichogundua hapa kwenye uzi wa dada yetu,ni kuwa kuwa na nyumba ni principal qualification then vinafuata vingine. Soma maandiko yake vizuri utaona.
 
Tatizo gani hilo la mumeo lililowashinda maaskofu na mahakimu. Alitaka 0713 nn..just kiding. Hapo dd kuwa makin mana pretenders ni wengi. Utapiga hesabu za yupi awe mume mwenzio anapiga hesabu agegede asepe.
 
Kwanza na mshukuru Mungu kwa rehema na baraka mbali mbali anazonijalia katika maisha yangu kila iitwapo leo.

Wana-MMU ninakuja kwenu nikihitaji ushauri juu ya hili suala, kiukweli maisha ya upweke yamenichosha, hii ni baada ya kudivorce na aliyekuwa mume wangu 2007. Mimi ni mama nina watoto wawili, 36yrs, mkristo. Nina nyumba yangu mwenyewe na asset kadhaa, baada ya kuchoshwa na upweke nimeona ni wakati muafaka wa kupata mwenzi mwingine. Nayamudu maisha yangu vizuri tu tatizo ni huo upweke tu, so naombeni mnishauri kuhusu hawa watu hapa chini.

1. Huyu ni mkaka 38yrs hajawahi kuoa ila ana mtoto mmoja, ni mafanyabiashara lakini pia ni mwanafunzi wa chuo fulani hapa nchini. Ana kiwanja, hajajenga so anaishi nyumba ya kupanga, ameonesha nia ya dhati ya kutaka kuishi na mimi pamoja na watoto wangu ila atapenda pia nimzalie watoto wawili. Nikifikiria hapo pa kuzaa watoto wawili nachanganyikiwa kabisa

2. Huyu ni mkaka, 36yrs, hajawahi kuoa ila na mtoto mmoja, ni mwajiriwa kwenye NGO na anasoma online chuo kikuu kimoja huko marekani. Ndio kwanza ameanza ujenzi wa nyumba yake, ananipenda mimi na watoto wangu, nae anapenda Mungu akijalia nimzalie watoto wawili. Hapo kwenye kuzaa nachanganyikiwa lkn pia namuona bado ana ujana mwingi

3. Huyu ni baba, 45yrs, ana familia yake, ana mke na watoto 3, ameajiriwa ofisi ya mtu binafsi, ana nyumba kadhaa, ananipenda kwa dhati, anaipenda familia yangu sana na anajitoa kwa hali na mali, kama tukioana anapenda nimzalie mtoto mmoja tu. Naweza kumzalia mtoto mmoja kama Mungu atapenda, tatizo ni hiyo familia na dini, yeye ni muislam, so anataka mimi niwe bi mdogo

Ushauri wako please, ukiona haikuhusu tafadhali potezea
olewa na wote....tena ukitaka ongeza wengne wawili
 
Wa 3 NDO MPANGO MZIMA!

We 36yrs uanze tena uendekeza stress! Mie umenizidi zaidi ya miak 10 ila stress navoziogopa???????????? Akuuuuuuuu! We mtu 38 HAJAJENGA? SERIOUSLY????????????? NA ANA KAZI????????????????/ HATA MABWE PANDE??????????

Mxiuuuuuuuuu! Utajikuta UNAFUGA JITU ZIMAAA wakati hata paka tu umeshindwakumfuga! Olewa na Zee hilo, ujipumzishe majukumu,na stress, mzeeke kwa amai. Vijana hao watakufuja fuja uache kuwalea wanao kibili gates buree ujitwishe misalab yao.

shost atapumzika kweli na mke mkubwa na wanaze
 
Ni kweli kabisa

Tatizo gani hilo la mumeo lililowashinda maaskofu na mahakimu. Alitaka 0713 nn..just kiding. Hapo dd kuwa makin mana pretenders ni wengi. Utapiga hesabu za yupi awe mume mwenzio anapiga hesabu agegede asepe.
 
Namba moja anakufaa, mchunguze kama unaona anakizi vigezo vyako tulia naye huyo. Kuwa mke wa pili sikushauri, kuolewa na huyo mwenye ujana mwingi atakusumbua. Mwisho wa siku uamuzi ni wako kuona nani anakufaa kwa matakwa yako.
 
Olewa na wa kwanza..kwani kuzaa watoto wawili kitu gani? ujue u cant eat ur cake and have it
 
Back
Top Bottom