niokoleeni jahazi nakaribia kukolapsi

niokoleeni jahazi nakaribia kukolapsi

Mimi naona huyo mtoto umwamishe shule ili hiyo concept ya kutokukubali kupigwa aende nayo shule mpya. Hapo atapigana kila siku kwa sababu wenzie walishazoea kumwonea na yeye hatakubali tena. Ushauri uliompa ni mzuri sana, mtoto anatakiwa akue akijua kwamba anatakiwa kutetea haki zake. Wewe hautakuwepo wakati wote kumpigania. Mimi wangu tatizo lake lilikuwa opposite, yeye ndio alikuwa anapiga sana wenzie mpaka watoto wote na walimu pia wakawa wanamchukia, ikafika wakati anarudi nyumbani kila siku hajasaishiwa exercise. Eti mwalimu anamkomoa. Mtoto asipopeleka daftari na yeye anamwacha hivohivo. Huyo mtoto atapata taabu sana hapo, mwamishe shule. Wangu alibadilika sana nilipomhamisha. Pole.

dah! ndugu umenifunza jambo. nikirudi namuhamisha shule.
 
Wewe bana. Piga simu ongea naye umpe moyo. Tena mwambie alichofanya ni sahihi ila asirudie tena mpaka utakaporudi umpe tekiniki nyingine ya kiume zaidi.

Ujumbe: Mwambie aangalie tangazo la MWANAUME WA KWELI HUTUMIA DUME.

hahahahah! asprin unavituko sana kwahiyo nianze kumfundisha kuwa mwanaume wa kweli siyo? mmh! asije akatushkia chini mm na baba yake lol!
 
Jamani hivi self defence sihata mahakamani inaruhusiwa? Mwanao hana kosa bwana alikuwa anajihami alah!

Mjukuu mtiifu sasa naona umekua.

Self defence ndio mpango mzima. Utaonewa mpaka lini wakati maisha yenyewe mafupi. Likionewa sana itafika kipindi watalila tigo na lenyewe litakubali kwa woga tu.

NB: Self defence kwenye tendo la ndoa na ndoa yenyewe, haikubaliki!
 
Shule gani hiyo ulishapeleka malalamiko anaonewa halafu waje wampige suspension? It seems walimu siyo wafwatiliaji hata kidogo, BTW kumuhamisha itakua solution nzuri, tafuta shule ambayo ina record nzuri ya walimu kuwa close na wanafunzi. Ningekua mimi ningeendaje kukoroma huko shuleni? Wangenitambua, mwanangu ameumizwa sikusikia mtu kapewa suspension, angerudi na hiyo barua mkononi,
All the best, malezi yanahitaji busara sana.

mmh! nataka nitafute tu shule nyingine aende basi ila haya mashule haya, mtu anajali pesa yake basi mtoto anaachwa ajilee mwenyewe.
 
Mjukuu mtiifu sasa naona umekua.

Self defence ndio mpango mzima. Utaonewa mpaka lini wakati maisha yenyewe mafupi. Likionewa sana itafika kipindi watalila tigo na lenyewe litakubali kwa woga tu.

NB: Self defence kwenye tendo la ndoa na ndoa yenyewe, haikubaliki!
mmmh! hii foot note mie mbavu sina lolest!
 
Damkubwa kibaya zaid sipo nyumban, sasa nashindwa kuhandle hali hii nkiwa mbali, manake napata maswali mengi sana juu ya hali hii na mpaka next wk sitokuwepo nifanyeje?

Please mweleze kila kitu Mdogo wako akaihandle hii issue na awaambie kuwa utakwenda kuonana nao ukirudi. Ila wapigie simu hao walimu waulize kiini cha suspension na uwatwange maswali ya liko wapi onyo au wito wa mzzi kabla ya kutoa adhabu ya suspension. Yaani ikiwezekama waisuspend hiyo suspension yao hadi utakapoongea nao wewe mzazi face to face na kukubaliana.
 
Hukukosea hata kidogo kumwambia huyo dogo ungetia mikwaju endapo angekuja tena kwako analia kwa kuonewa!! Haikuwa ishara njema hata kidogo kwa mtoto wa kiume kila wakati anarudi nyumbani analia!! Kama usingefanya hivyo, basi ukubwani angekuja kupigwa hata na mademu zake achilia mbali mke..!!! Na hapo kosa kubwa kwake halikuwa kuonewa, bali kurudi nyumbani kushitaki kwamba ameonewa!! Kidume cha kweli, hata kama kweli hakiwezi kupigana, kinalia huko huko na kinarudi nyumbani kimenyamaza kama hakuna ambacho kilimkuta kabla! Na hata ikitokea amekula kichapo hadi kuumia, atadanganya alianguka au alijigonga. So, huo mkwara ambao ulimpa ilikuwa ni kumfundisha mwanao kuwa a real dude!! Hapo umempa bonge la msingi wa kutatua matatizo yake binafsi yeye mwenyewe, otherwise hapo ukubwani ingekuwa kila siku kesi zake na mke wake anazipeleka kwa wazee!!

Tukirudi kuhusu wht u need to do kutokana na hiyo issue, kwanza mweleze mwanao asije akaja kuropoka kwamba "mama aliniambia nikionewa nisikubali!" Mtoto ni mtoto tu, anaweza kusema chochote akiona ametaitiwa! Mwambie aseme alikuwa anajitetea kwavile kila mara alikuwa anampiga. Na kwavile ulishawahi mara kadhaa kwenda hapo shule kulalamika kuhusu kuonewa kwa mwanao, then i hope waalimu watakuwa fair....!! Na kwavile ameshatoa displini, basi huenda scenario hiyo huenda isitokee tena coz' watamuogopa!
 
Hapo ni kumwambia mtoto endelea hivyo hivyo
wakikugusa tu wadunde....full stop...
 
Mjukuu mtiifu sasa naona umekua.

Self defence ndio mpango mzima. Utaonewa mpaka lini wakati maisha yenyewe mafupi. Likionewa sana itafika kipindi watalila tigo na lenyewe litakubali kwa woga tu.

NB: Self defence kwenye tendo la ndoa na ndoa yenyewe, haikubaliki!

Hahah Babu kwa hiyo kwenye ndoa na wewe ukiambiwa geuka kidole utatii?? LOL
 
Damkubwa kibaya zaid sipo nyumban, sasa nashindwa kuhandle hali hii nkiwa mbali, manake napata maswali mengi sana juu ya hali hii na mpaka next wk sitokuwepo nifanyeje?

Mi nlifikiri unarudi mwaka ujao, kumbe nekst wiik? Mwambie dada amtengenezee ugali wa muhogo kwa wingi, na yeye apige zoezi la kutosha kwakuwa kocha mkuu unakuja na teknik mpya ya self defence.

BTW baba yake amechukua hatua gani?
 
Ase umenikumbusha my mamushka she did the same, nkamtoa mtoto mwenzangu jino lilikuwa limelegea tena nakumbuka yale ya utotoni, nkapewa suspaa maza akaenda wasuta akanihamisha, so kama wewe ulishawalalamikia hawakuchukua hatua yoyote ila mwanao kafanya the same wame react it seems wamefanya kusudi kukukomesha wamesema huyu mama ake si ndo huwa mlalamikaji mkuu hapa kumbe mwanae kakorofi ngoja tumwadhibu naye ajue mwanae mkorofi, ongea nao kwanza lkn na ni bora uende wewe kama utarudi sijui ni safarini au kazini upo, uende ongea nao kiutu uzima tu kama wakionekana wana jeuri basi just accept the punishment mpeleke tuition hadi mtihani utapoanza afanye salama afaulu umwamishe shule mbona zipo nyingi tu bana, wasikuchoshe kabisa, sasa walitaka umshaurije mwanao? akipigwa shavu la kulia ageuze la kushoto, wala usipatwe na mawazo dada u have real son, mpeleke popote pale hatokuangusha, All the best.
 
Asprin ujue niliwaza nikupigie wewe nikuombe unisaidie kwenda huko shule, manake nataka mwanangu nae awe jasiri na sioni kosa manake nimekuwa nikilalamika sana juu ya watoto kuachwa kupigana hovyo, ingawa waalim wao hawako makin katika hili. pia nimewaza kumuhamisha tu shule manake naona mapaka afike grade 7 nitakufa kwa presha.
HII NIMEIPENDA Asprin inafaa avae ubaba halisi, aende kama mzazi, nitakuwa pembeni kama mama mdogo!! kama umempa Asprin hii kesi, basi imekwisha!! hubby usituangushe, mtoto arudi shule, busara zako tunaziamini.
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na hayo, inabidi ufikirie kumuhamisha hiyo shule.

Haionekani kama ni shule nzuri katika kuwafundisha watoto kuheshimiana na usimamizi wa nidhamu kwa ujumla.

Kwa hapo hali ilipofikia inabidi tu uende mwenyewe shuleni ukawaulize maswali kadhaa hao walimu wa watoto je mtoto wako alipofanyiwa vibaya pia walichukua hatua kama wanazotaka kumchukulia dogo?

Pia kama ni kosa la kwanza, hamna hata onyo jamani?

Otherwise kuna ubabaishaji hiyo sio shule nzuri, sijui upo mji gani ila siku hizi kuna shule nyingi sana nzuri na watoto wana adabu na wanasimamiwa vizuri.

Pole kwa mshtuko!

asante sana mkuu. ila haya mashule ambayo pia yanaangalia sura za watu ni matatizo matupu.
 
Hapo ni kumwambia mtoto endelea hivyo hivyo
wakikugusa tu wadunde....full stop...

wiki sio ishu kabisa

The Boss uko right but ni muhimu pia walimu wakauelewa msimamo wa mzazi. Aigomee hiyo suspension ya kionevu na hao walimu waelewe kuwa kuna wazazi wanaojua haki zao katika shule zao.
 
Mi nlifikiri unarudi mwaka ujao, kumbe nekst wiik? Mwambie dada amtengenezee ugali wa muhogo kwa wingi, na yeye apige zoezi la kutosha kwakuwa kocha mkuu unakuja na teknik mpya ya self defence.

BTW baba yake amechukua hatua gani?
baba yake amesema simple tu ahame shule na tena anataka apelekwe hata darasa la karate. nikimsikiliza huyu lol! nitapoteza mtt
 
Yaani mpenzi haukukosea kabisaa. Na kwa sababu mwanao akipigwa waalimu hawakuwahi kuwa bothered, basi afadhali mtoo kajitetea. Muambie mwanao violence is the last solution to bullying. Akiweza kusema kwa mwalimu. Ila kama alivyosema Asprin, angenyofoa mtu jino wangemuheshimu.

Sijui kama naweza kutolerate bullying kwa mwanangu aisee!
 
Last edited by a moderator:
kwani hao waliokuwa wanampiga yeye walikuwa suspended? Au ni yeye tu ndo imekuwa inshu?

Kwanza nakupongeza kwa ushauri uliompa mwanao. Sasa nae atakuwa huru, watamheshimu na performance yake itaongezeka zaidi nakushauri ondoa wazo la kumhamisha shule.

Note kwamba; kama wewe ilikuwa inakuuma akipigwa basi yeye mwenyewe ilikuwa inamuuma sana na kumuondolea kujiamini.
 
Back
Top Bottom