niokoleeni jahazi nakaribia kukolapsi

niokoleeni jahazi nakaribia kukolapsi

Rekodi zinamtetea
Waambie walimu utaongea na mwanao nyumbani
Afu akifika nyumbani, mpongeze kwa kuweka rekodi ya kiume
Ila asiendelee kuwapiga tena, maana hadi hapo ujue wameshamuogopa

Mimi nafikiri hii imekaa vizuri, ila na walimu nao usisahau kuwapongeza kuwa inaonekana sasa wameanza kuchukua hatua kwa watoto wanaopigana shule (nia ni kuwasuta tu coz huchelewi kukuta kuwa wakwako ni wa kwanza kuadhibiwa).

Nakumbuka nilikuwa namuasa sana mwanangu kuwa asipigane shule, na kama kuna uonevu wowote basi amuambie mwalimu wake. Kumbe behind my back, mama mkwe alikuwa anamuambia..wakikupiga na wewe piga tu, mtoto wa kiume hamna kuonewa onewa! Nilichokaje?
 
Hahah Babu kwa hiyo kwenye ndoa na wewe ukiambiwa geuka kidole utatii?? LOL

Unakorofisha ujue. Anayetakiwa kujidefend kwenye ndoa na tendo lake ni mwanamke.

Kumbe bado hujakua eh? we unafikiri nazungumzia "ngumi" kwenye ndoa? Hapa nazungumzia naniliyu bana, hakuna kujidefend ni kukubali tu naniliyu ifanye kazi yake...

Ushanfahamu?
 
HII NIMEIPENDA Asprin inafaa avae ubaba halisi, aende kama mzazi, nitakuwa pembeni kama mama mdogo!! kama umempa Asprin hii kesi, basi imekwisha!! hubby usituangushe, mtoto arudi shule, busara zako tunaziamini.

mwali usininagushe manake nataman kumtoa mtu korodani kwa kumnyanyasa mwanagu.
 
HII NIMEIPENDA Asprin inafaa avae ubaba halisi, aende kama mzazi, nitakuwa pembeni kama mama mdogo!! kama umempa Asprin hii kesi, basi imekwisha!! hubby usituangushe, mtoto arudi shule, busara zako tunaziamini.

Hahahahha! wifey bana. Umeona eh? Chezeya ODM? Hebu nunua hii kesi tuongozane asee.

Afu unajua nakumisije?
 
Last edited by a moderator:
Usimhamishe, atahama shule ngapi?
Na maishani akikutana na masahibu ahame mtaa ama akabiliane nayo?
Hii pia inamjenga kukabiliana na makashkash hata akiwa mtu mzima
Nsio mchakato wa kujifunza huo

duh! na hili ndo nililokuwa nimelisahau. ila jaman mtoto akionewa inauma sana na sijui kama kuna mzazi anaweza vumilia aisee. khaaa! sijui nikutafute aje kwako likizo umfundishe karate lol!
 
Yaani mpenzi haukukosea kabisaa. Na kwa sababu mwanao akipigwa waalimu hawakuwahi kuwa bothered, basi afadhali mtoo kajitetea. Muambie mwanao violence is the last solution to bullying. Akiweza kusema kwa mwalimu. Ila kama alivyosema Asprin, angenyofoa mtu jino wangemuheshimu.

Sijui kama naweza kutolerate bullying kwa mwanangu aisee!
king'asti nilishindwa kuvumilia mwanangu kuonewa na mpaka namfunza kuwa na self defense nilichoka kuumia moyo. na kiukweli nilimpa njia ambayo sasa inanitokea puani. am proud of him ila tu nataka sasa ajue wapi pa kutumia nguvu kubwa na wapi pa kupiga kibao tu.
 
an eye for an eye makes the world blind dada gfsonwin. jaribu kujua kwa nini mwanao anakuwa bullied. ukijua chanzo u may find a solution. does he have friends who he 'clicks' with, is he socialable kid? find out. i was bullied till 3rd grade when it stopped and i wasn't even into many of the 'boy' stuffs so give it time and avoid violence.
 
Last edited by a moderator:
kwani hao waliokuwa wanampiga yeye walikuwa suspended? Au ni yeye tu ndo imekuwa inshu?

Kwanza nakupongeza kwa ushauri uliompa mwanao. Sasa nae atakuwa huru, watamheshimu na performance yake itaongezeka zaidi nakushauri ondoa wazo la kumhamisha shule.

Note kwamba; kama wewe ilikuwa inakuuma akipigwa basi yeye mwenyewe ilikuwa inamuuma sana na kumuondolea kujiamini.

mkuu jf naipenda kwasababu ya watu kama wewe, asante sana
 
Hii mbona kawaida sana nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 80 mdogo wangu alikua anchezea kichapo kwa wenzake siku hiyo karudi kapigwa baba akamwmbia kesho wakikuchokoza tena kamata mmoja ngata! Aisee baada ya siku mbili tu kudagadeki aling'ata mtoto wa watu mkono nusuru atoe nyama! Tolkea siku hiyo hakuna tena kuja analia! Mtoto yoyote anachosikia kwa baba anakiamini kuliko maelezo! Sasa hiyo kesi ikiisha we mwambie msimamo ni huo huo ukichokozwa dunda then nenda kaseme kwa mwalimu
 
an eye for an eye makes the world blind dada gfsonwin. jaribu kujua kwa nini mwanao anakuwa bullied. ukijua chanzo u may find a solution. does he have friends who he 'clicks' with, is he socialable kid? find out. i was bullied till 3rd grade when it stopped and i wasn't even into many of the 'boy' stuffs so give it time and avoid violence.
mmh! hapa unanifanya nijichukie..........but havivumiliki bana. niliwah kujua ni kwann anaonewa na sababu ilikuwa nje ya uwezo wetu, mwanangu darasani ni mzuri sana, na ukweli baba yake hujitahd sana na vijizawadi vya shule ambavyo ni unique hasa begi la shule ruler nk unajua kuna viitu ambavyo unaweza ukampa mtoto kwa nia njema ila sasa vikamsabishia mtoto madhara kwamfano wenzie kumchukia, so wenzake waliona kama anaringa na vitu vyake hivyo so baadhi ya wavulana mle darasan wakawa na -ve attitude. nilipogundua haya nilimwambia aanze kujitetea manake hata kucheza nae walikataa.
 
Mm sijaona kama umekosea kumfundisha mwanao awe na SELF DEFENCE! tena anza leo kumwambia yeye ni mwanaume, na anatakiwa asimame na ajiamini kwa sababu baadaye atakwenda kuwa baba wa nyumba. so akilegea hata mkewe anakuwa anampiga, sasa hapo wewe mama yake utakubali??? si ndiyo utakwenda kupigana na mkweo.So mfundishe kupigania haki yake, na asikubali kuonewa. YAANI NI MARUFUKU KUONEWA AKIWA MWANAUME!!!
 
Hii mbona kawaida sana nakumbuka mwanzoni mwa miaka ya 80 mdogo wangu alikua anchezea kichapo kwa wenzake siku hiyo karudi kapigwa baba akamwmbia kesho wakikuchokoza tena kamata mmoja ngata! Aisee baada ya siku mbili tu kudagadeki aling'ata mtoto wa watu mkono nusuru atoe nyama! Tolkea siku hiyo hakuna tena kuja analia! Mtoto yoyote anachosikia kwa baba anakiamini kuliko maelezo! Sasa hiyo kesi ikiisha we mwambie msimamo ni huo huo ukichokozwa dunda then nenda kaseme kwa mwalimu
asante sana Zanta. malezi kazi
 
Last edited by a moderator:
Mm sijaona kama umekosea kumfundisha mwanao awe na SELF DEFENCE! tena anza leo kumwambia yeye ni mwanaume, na anatakiwa asimame na ajiamini kwa sababu baadaye atakwenda kuwa baba wa nyumba. so akilegea hata mkewe anakuwa anampiga, sasa hapo wewe mama yake utakubali??? si ndiyo utakwenda kupigana na mkweo.So mfundishe kupigania haki yake, na asikubali kuonewa. YAANI NI MARUFUKU KUONEWA AKIWA MWANAUME!!!
aisee mwanaume kumjengea kujiamini ni kazi sana, manake lazima ubabe umwekee ndani yake.
 
mkuu mbona kawaida tu!?. je hiyo hali inakuuma zaidi ya ilivyo kuwa inakuuma baada ya mwanao kupigwa?. mi nikajua ameua mtu kumbe kamtishia kwa maneno kumvunja!. alikua anajihami. sasa hivi watoto wanaanza kwenda likizo. so hamna noumer. Hakikisha unakua upande wa mwanao. Shule ndo inafundisha kupigana sababu hiyo tabia kaitoa shuleni. mara ngapi umewalalamikia mbona hakuna aliye simamishwa masomo?. Mi naona wanakuoneeni tu.NOTE: Wakati wa kumrudisha jifanye mjinga siku ipite. wasikilize. mia
 
aisee mwanaume kumjengea kujiamini ni kazi sana, manake lazima ubabe umwekee ndani yake.

Yaani hata mm wangu alikuwa anaonewa sana, siku hiyo nilikaa naye nikamfundisha kuwa ukimwona anayekupiga ni mkubwa mvizie mng'ate sikio, ukiona unamweza mpige roba ya nguvu ,akamngata sikio mtoto wa watu nikaitwa shule nikaomba msamaha, niliporudi home nikamnunulia ICe cream ya Azam na Kumwambia Kuwa HUO NDIYO UANAUME , USIKUBALI KUONEWA.tangia hapo mpka leo yupo darasa la nne ahaonewa na anajisikia huru kuwa mwanaume.
 
wazazi wa kike tuna kazi lol!
 
unajua gfsonwin hata viongozi wanaandaliwa, tena penda kumpa mwanao challenge za kujieleza mbele yako, asimame kama vile anafanya presentation , hapo unakuwa unamjengea uwezo wa kujiamini kwamba yeye ni mwanaume na kujitetea kama kuna tatizo maana anakuwa hana hofu. mjenge mwanao leo usingoje kesho.
 
mi too hun! ila niliongea na KARIA, Najua wajua kuwa nasi twajua vile wajuavyo!

Hahahahaha wife bana.... Mafumbo mengine mi hoi lol

Kaniambia kuna mpango mkakati weekend hii maeneo na muda kama ule. Eti ni kweli nianze mazoezi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom