gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,720
Naandika uzi huu nikiwa na mawazo sana na hapa nisaidieni kukoa jahazi na kurekebisha makosa yangu chonde jalini hisia zangu.
Mwanagu wa miaka 9 ni mvulana na alikuwa mara kwa mara anapigwa na wenzie shule. hii hali niijaribu kuikemea sana kwa kwenda shule kuongea na waalimu wake lakin ikipita wiki ni bahati lazima atarudi kaumizwa na mwenzie tena kidonda cha kumtia kovu. sikukata tamaa ya kufuatilia kwa waalimu wake na hata kwa baadhi ya wazazi ambao watoto wao walikuwa wanamwonea mwanangu. Simtetei ila katika watoto wangu huyu anaonekana kuwa mtu anayependa sana kazi na pia anapenda kusoma na huwa ananitia moyo kwa perfomance nzuri lkn tatizo ni mpole sana na huwa havunji mwiko alopewa na mwl wake wa sunday school wa kuwapenda wenzie.
kasheshe ilikuja kama mwez wa 10 hivi alitegewa mguu na mwenzie na kuanguka akachubuka usoni eneo la karibu na jicho nilikasirika sana nikamwambia sasa iwe ni mwisho siku ukija hapa nyumban umepigwa ama kuumizwa nakuchapa. Nilinadi sera mwenyewe kwamba hali pamba, hivyo akipigwa na yeye apige ni heri niitwe kwamba kamuumiza mwenzie kuliko yeye kaumizwa. ( nakiri nilikosea hapa usihukumu)
sasa kasheshe imekuja home jana kapewa barua shulen ya suspension ya wiki moja kisha arudi shule na mzazi kosa lake ni kwamba amempiga mwenzie shulen kiasi cha kumuumiza na akamtishia kwamba atamvunja mkono. mm sipo nyumban ili nitatue haya, hapa nilipo nimechanganyikiwa sijui nifanyeje. tatizo lililopo ni hili
1) mtoto si ataona mama nimemtega kutenda kosa lililomtia hatiani??
2) je nitakubalije kwamba mwanangu ni mkosa ilihali mm ndo niliye mtuma??
3)nategemea kumtuma mamdogo aende shuleni ila je itumike busara gani ili mwanangu asiadhibiwe?
wapendwa Kongosho, HorsePower, King'asti, Mtambuzi, platozoom na wengine wote nisaidieni, jamani nakaribia kuzimia. manake mtoto huko nyumban analia tu hanyamazi.

Last edited by a moderator: