niokoleeni jahazi nakaribia kukolapsi

niokoleeni jahazi nakaribia kukolapsi

Chochote kile utakachofanya hakikisha kwamba hutaharibu confidence ya kijana wako. Hata kama utamsemea mbovu mbele ya walimu kwa ajili ya kulinda asitimuliwe shule, ukirudi home teta nae, na umpongeze. Ila katika pongezi, ni vizuri ukamfundisha pia kuwa na subira na kufuata sheria za shule.
 
Ujue wewe una busara sana!

Basi tu fyatanga wanakuharibu

Heheheheh! Wewe bana LoL

Katika hali ya kawaida toto lako kila siku linakuja linalia limepigwa. Umechukua hatua ya kuripoti kwa walimu na wazazi wa watoto wakorofi lakini halieleweki.

Mzazi bora na mwema kama mimi sitamwambia mtoto apigane kiume tu, bali pia ntamfundisha namna ya kuwatwanga hasa maeneo nyeti. Pia na kumfundisha mbinu ya kuwagongea magelofrendz zao. Shenzy taipu zao na nusu.
 
Dada pole kwa kweli usijilaumu sana kwa sababu ni kweli umekosea na kama ujuavyo mtoto ukimfunza hushika haraka lakini nadhani ile hali ya yeye kuonewa kila mara ndio ilimsukuma kufanbya kama ulivyomshauri. Nina maswali kidogo;
1. Hao walimu ni wale wale ambao wewe ulikuwa unawalalamikia wakati mwanao akija amepigwa?
2. Kama ni ndio kwa nini kabla hawajamsuspend hawakukuita wewe kukujulisha juu ya mabadiliko ya mwanao?( Maana ni wazi kuwa kosa la kwanza kama hilo halimfanyi mtoto kwenda nyumbani na
3. Wakati yeye alipokuwa anapigwa na kuumwizwa hao watoto waliokuwa wanampiga walikuwa nao wanapewa sunspensions?
 
Rekodi zinamtetea
Waambie walimu utaongea na mwanao nyumbani
Afu akifika nyumbani, mpongeze kwa kuweka rekodi ya kiume
Ila asiendelee kuwapiga tena, maana hadi hapo ujue wameshamuogopa
kongosho nashukuru umenitia moyo, namm nitamwambia mamdogo awaambie tutaongea na mtoto nyumbani. sasa kwa kipindi hiki yupo nyumban afanyiwe nini ili asijione mkosa?
 
Jamani hivi self defence sihata mahakamani inaruhusiwa? Mwanao hana kosa bwana alikuwa anajihami alah!
 
Dada pole kwa kweli usijilaumu sana kwa sababu ni kweli umekosea na kama ujuavyo mtoto ukimfunza hushika haraka lakini nadhani ile hali ya yeye kuonewa kila mara ndio ilimsukuma kufanbya kama ulivyomshauri. Nina maswali kidogo;
1. Hao walimu ni wale wale ambao wewe ulikuwa unawalalamikia wakati mwanao akija amepigwa?
2. Kama ni ndio kwa nini kabla hawajamsuspend hawakukuita wewe kukujulisha juu ya mabadiliko ya mwanao?( Maana ni wazi kuwa kosa la kwanza kama hilo halimfanyi mtoto kwenda nyumbani na
3. Wakati yeye alipokuwa anapigwa na kuumwizwa hao watoto waliokuwa wanampiga walikuwa nao wanapewa sunspensions?

jambo ambalo hata mm nimeshindwa kulijua ni kwann amekuwa suspended bila baria ya onyo ama wito tu kwa mzazi?? pia waalim ni wale wale na sikuwah kujua kama waliokuwa wanampiga walikuwa suspended ama vipi ingawa nimeshalalamika zaid ya mara 4 juu ya mwanangu kupigwa na kuumizwa. nimewaza kwamba ni uonevu ama labda kamuumiza sana manake sijamuona aliyeumizwa.
 
Asprin ujue niliwaza nikupigie wewe nikuombe unisaidie kwenda huko shule, manake nataka mwanangu nae awe jasiri na sioni kosa manake nimekuwa nikilalamika sana juu ya watoto kuachwa kupigana hovyo, ingawa waalim wao hawako makin katika hili. pia nimewaza kumuhamisha tu shule manake naona mapaka afike grade 7 nitakufa kwa presha.

Heheheee! Khaa!
Mkwala ambao ningeingia nao, ningewatafuna walimu wote mabinti na kijana angeteuliwa kuwa kiranja mkuu!
 
Last edited by a moderator:
Jamani hivi self defence sihata mahakamani inaruhusiwa? Mwanao hana kosa bwana alikuwa anajihami alah!

Da mkubwa huwez kuamini nataka kumuhamisha shule manake naona nitakufa kwa presha tu.
 
Lazima atambue kupewa suspension sio vizuri
Na sidhani kama anastahili adhabu
Wee ukirudi utaongea naye kwa kirefu

Ha hiyo guility muibebe wote, usiache aibebe peke yake kwa kujiona mkosaji sana
Ila asijione kafanya la maana sana pia

kongosho nashukuru umenitia moyo, namm nitamwambia mamdogo awaambie tutaongea na mtoto nyumbani. sasa kwa kipindi hiki yupo nyumban afanyiwe nini ili asijione mkosa?
 
Naandika uzi huu nikiwa na mawazo sana na hapa nisaidieni kukoa jahazi na kurekebisha makosa yangu chonde jalini hisia zangu.

Mwanagu wa miaka 9 ni mvulana na alikuwa mara kwa mara anapigwa na wenzie shule. hii hali niijaribu kuikemea sana kwa kwenda shule kuongea na waalimu wake lakin ikipita wiki ni bahati lazima atarudi kaumizwa na mwenzie tena kidonda cha kumtia kovu. sikukata tamaa ya kufuatilia kwa waalimu wake na hata kwa baadhi ya wazazi ambao watoto wao walikuwa wanamwonea mwanangu. Simtetei ila katika watoto wangu huyu anaonekana kuwa mtu anayependa sana kazi na pia anapenda kusoma na huwa ananitia moyo kwa perfomance nzuri lkn tatizo ni mpole sana na huwa havunji mwiko alopewa na mwl wake wa sunday school wa kuwapenda wenzie.

kasheshe ilikuja kama mwez wa 10 hivi alitegewa mguu na mwenzie na kuanguka akachubuka usoni eneo la karibu na jicho nilikasirika sana nikamwambia sasa iwe ni mwisho siku ukija hapa nyumban umepigwa ama kuumizwa nakuchapa. Nilinadi sera mwenyewe kwamba hali pamba, hivyo akipigwa na yeye apige ni heri niitwe kwamba kamuumiza mwenzie kuliko yeye kaumizwa. ( nakiri nilikosea hapa usihukumu)

sasa kasheshe imekuja home jana kapewa barua shulen ya suspension ya wiki moja kisha arudi shule na mzazi kosa lake ni kwamba amempiga mwenzie shulen kiasi cha kumuumiza na akamtishia kwamba atamvunja mkono. mm sipo nyumban ili nitatue haya, hapa nilipo nimechanganyikiwa sijui nifanyeje. tatizo lililopo ni hili

1) mtoto si ataona mama nimemtega kutenda kosa lililomtia hatiani??
2) je nitakubalije kwamba mwanangu ni mkosa ilihali mm ndo niliye mtuma??
3)nategemea kumtuma mamdogo aende shuleni ila je itumike busara gani ili mwanangu asiadhibiwe?

wapendwa Kongosho, HorsePower, King'asti, Mtambuzi, platozoom na wengine wote nisaidieni, jamani nakaribia kuzimia. manake mtoto huko nyumban analia tu hanyamazi.

Pole sana mdogo wangu,sasa mimi naomba nikuulize swali kwanza,hivi wale wenzie waliokuwa wanampiga na kumuumiza mwanao walikuwa wanachukuliwa hatua gani??kama hatua ni hiyo hiyo kama aliochukuliwa mwanao cha kufanya kubali hiyo adhabu aliyopewa mwanao,lakini kaa nae chini umueleze ukweli,mwambie alichofanya ni sahihi kabisa maana alikuwa anajitetea,sema alitakiwa asiwatishie wenzie na ajitahidi kuepuka kupigana na kuwaumiza wenzie,yaan mfunze kupima kiwango cha kichapo anachopaswa kuwapa wenzie wanaomchokoza,na pia mwambie kwamba ugomvi huwa hautakiwi kabisa na kila sehemu kuna sheria zake,na kwakuwa alikuwa shule basi hizo ni sheria za shule na ndio zinatekelezwa,mbali ya yote huyo ameshatoa onyo watoto wenzie watamuogopa,na hawata mchezea tena.
 
Heheheee! Khaa!
Mkwala ambao ningeingia nao, ningewatafuna walimu wote mabinti na kijana angeteuliwa kuwa kiranja mkuu!

nenda basi rafiki niokolee jahazi. manake nimeongea nae sasa hivi anasema yeye ndo alichokozwa kwahiyo akajihami.
 
Kwanza pole. pili swali kwa mwanao hana marafiki mabaunsa wa kumtetea cz nahisi yeye 'mayai' sana. Chakufanyika nenda shule ongea na waalimu wake kesi ikiisha mwandae mwanao kikomando nikiwa na maana asiwe mnyonge wanamuonea sana. Ataharibika kisaikolojia n perfomance itashuka taratibu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nakupongeza umempa mwanao somo zuri sana la kujitetea pindi anapoonewa. Na kamwe usirudi nyuma mwambie mwanao ajitetee kwa nguvu zake zote pindi anapoonewa kwani ulimwengu tunaoishi ni wa struggle' The strongs survives through the expences of the weak'. Maana ukimwacha aruhusu hilo kutokea wewe ndo utakuwa m2 wa kununu kalamu na madaftari kila sk mana atakuwa anaibiwa au ht kunyang'anywa. Hivyo mpöngeze kwa kujilinda ila mwambie asiwe mchokz bali ajilinde pindi akionewa. Kuhusu walimu hapo hakuna kesi yoyote, ongea nao kikubwa yataisha tu.
 
Hao walimu walipaswa kuwaita kwa pamoja wazazi na watoto waliohusika kisha wawacondemn kwa kosa la KUPIGANA na kila mtoto apewe nafasi ya kujitetea kwanza kabla ya kususpend mwanao. Labda kama alopigwa ni mtoto wa mwalimu mwenzao so ana hasira au wa mkubwa flani
 
Pole sana mdogo wangu,sasa mimi naomba nikuulize swali kwanza,hivi wale wenzie waliokuwa wanampiga na kumuumiza mwanao walikuwa wanachukuliwa hatua gani??kama hatua ni hiyo hiyo kama aliochukuliwa mwanao cha kufanya kubali hiyo adhabu aliyopewa mwanao,lakini kaa nae chini umueleze ukweli,mwambie alichofanya ni sahihi kabisa maana alikuwa anajitetea,sema alitakiwa asiwatishie wenzie na ajitahidi kuepuka kupigana na kuwaumiza wenzie,yaan mfunze kupima kiwango cha kichapo anachopaswa kuwapa wenzie wanaomchokoza,na pia mwambie kwamba ugomvi huwa hautakiwi kabisa na kila sehemu kuna sheria zake,na kwakuwa alikuwa shule basi hizo ni sheria za shule na ndio zinatekelezwa,mbali ya yote huyo ameshatoa onyo watoto wenzie watamuogopa,na hawata mchezea tena.

kwakweli hilo sina hakika nalo kama walikuwa suspended ama vipi. ila tu simuoni mwanagu kama mkosa ila sasa nashindwa kujua nitumie mbinu gani kumfunza mwanangu kwamba hana makosa katika hili.
 
Asprin ujue niliwaza nikupigie wewe nikuombe unisaidie kwenda huko shule, manake nataka mwanangu nae awe jasiri na sioni kosa manake nimekuwa nikilalamika sana juu ya watoto kuachwa kupigana hovyo, ingawa waalim wao hawako makin katika hili. pia nimewaza kumuhamisha tu shule manake naona mapaka afike grade 7 nitakufa kwa presha.

Shule gani hiyo ulishapeleka malalamiko anaonewa halafu waje wampige suspension? It seems walimu siyo wafwatiliaji hata kidogo, BTW kumuhamisha itakua solution nzuri, tafuta shule ambayo ina record nzuri ya walimu kuwa close na wanafunzi. Ningekua mimi ningeendaje kukoroma huko shuleni? Wangenitambua, mwanangu ameumizwa sikusikia mtu kapewa suspension, angerudi na hiyo barua mkononi,
All the best, malezi yanahitaji busara sana.
 
Last edited by a moderator:
kongosho nashukuru umenitia moyo, namm nitamwambia mamdogo awaambie tutaongea na mtoto nyumbani. sasa kwa kipindi hiki yupo nyumban afanyiwe nini ili asijione mkosa?

Wewe bana. Piga simu ongea naye umpe moyo. Tena mwambie alichofanya ni sahihi ila asirudie tena mpaka utakaporudi umpe tekiniki nyingine ya kiume zaidi.

Ujumbe: Mwambie aangalie tangazo la MWANAUME WA KWELI HUTUMIA DUME.
 
Naandika uzi huu nikiwa na mawazo sana na hapa nisaidieni kukoa jahazi na kurekebisha makosa yangu chonde jalini hisia zangu.

Mwanagu wa miaka 9 ni mvulana na alikuwa mara kwa mara anapigwa na wenzie shule. hii hali niijaribu kuikemea sana kwa kwenda shule kuongea na waalimu wake lakin ikipita wiki ni bahati lazima atarudi kaumizwa na mwenzie tena kidonda cha kumtia kovu. sikukata tamaa ya kufuatilia kwa waalimu wake na hata kwa baadhi ya wazazi ambao watoto wao walikuwa wanamwonea mwanangu. Simtetei ila katika watoto wangu huyu anaonekana kuwa mtu anayependa sana kazi na pia anapenda kusoma na huwa ananitia moyo kwa perfomance nzuri lkn tatizo ni mpole sana na huwa havunji mwiko alopewa na mwl wake wa sunday school wa kuwapenda wenzie.

kasheshe ilikuja kama mwez wa 10 hivi alitegewa mguu na mwenzie na kuanguka akachubuka usoni eneo la karibu na jicho nilikasirika sana nikamwambia sasa iwe ni mwisho siku ukija hapa nyumban umepigwa ama kuumizwa nakuchapa. Nilinadi sera mwenyewe kwamba hali pamba, hivyo akipigwa na yeye apige ni heri niitwe kwamba kamuumiza mwenzie kuliko yeye kaumizwa. ( nakiri nilikosea hapa usihukumu)

sasa kasheshe imekuja home jana kapewa barua shulen ya suspension ya wiki moja kisha arudi shule na mzazi kosa lake ni kwamba amempiga mwenzie shulen kiasi cha kumuumiza na akamtishia kwamba atamvunja mkono. mm sipo nyumban ili nitatue haya, hapa nilipo nimechanganyikiwa sijui nifanyeje. tatizo lililopo ni hili

1) mtoto si ataona mama nimemtega kutenda kosa lililomtia hatiani??
2) je nitakubalije kwamba mwanangu ni mkosa ilihali mm ndo niliye mtuma??
3)nategemea kumtuma mamdogo aende shuleni ila je itumike busara gani ili mwanangu asiadhibiwe?

wapendwa Kongosho, HorsePower, King'asti, Mtambuzi, platozoom na wengine wote nisaidieni, jamani nakaribia kuzimia. manake mtoto huko nyumban analia tu hanyamazi.


Mimi naona huyo mtoto umwamishe shule ili hiyo concept ya kutokukubali kupigwa aende nayo shule mpya. Hapo atapigana kila siku kwa sababu wenzie walishazoea kumwonea na yeye hatakubali tena. Ushauri uliompa ni mzuri sana, mtoto anatakiwa akue akijua kwamba anatakiwa kutetea haki zake. Wewe hautakuwepo wakati wote kumpigania. Mimi wangu tatizo lake lilikuwa opposite, yeye ndio alikuwa anapiga sana wenzie mpaka watoto wote na walimu pia wakawa wanamchukia, ikafika wakati anarudi nyumbani kila siku hajasaishiwa exercise. Eti mwalimu anamkomoa. Mtoto asipopeleka daftari na yeye anamwacha hivohivo. Huyo mtoto atapata taabu sana hapo, mwamishe shule. Wangu alibadilika sana nilipomhamisha. Pole.
 
Hao walimu walipaswa kuwaita kwa pamoja wazazi na watoto waliohusika kisha wawacondemn kwa kosa la KUPIGANA na kila mtoto apewe nafasi ya kujitetea kwanza kabla ya kususpend mwanao. Labda kama alopigwa ni mtoto wa mwalimu mwenzao so ana hasira au wa mkubwa flani

Damkubwa kibaya zaid sipo nyumban, sasa nashindwa kuhandle hali hii nkiwa mbali, manake napata maswali mengi sana juu ya hali hii na mpaka next wk sitokuwepo nifanyeje?
 
Back
Top Bottom