niokoleeni jahazi nakaribia kukolapsi

niokoleeni jahazi nakaribia kukolapsi

...hahahah gfsonwin kidume hicho kimepambana..........

Ila seriously, kama mtoto anapigwa mara kwa mara, walimu hawachukui hatua (hapa inakua ya kinidhamu zaidi)
Unadhani ni shuke inayomfaa mtoto? Unadhani hali hiyo naitimuathiri mtoto?

Upande wangu naomba zungumza na mtoto kwa lugha ya upole na kwa utaratibu.....ila hebu mtafutie mtoto shule ambayo walimu wapo macho na watoto wote.....inayowafundisha kupendana na disciplin kiasi kuwa watoto wanajua kuwa ni
vibaya kupigana shuleni,itamsaidia mtoto kufurahia maisha yake ya shuleni

ila kwa wakati huu zungumza tu na walimu, na ukizungumza nao usisahau kuwauliza je mtoto aliyemuumiza mwanao last time alipewa adhabu gani? Kusije kukawa na double standards, wape malalamiko yako, waulize toka uwalalamikie kupigwa na kuumizwa kwa mwanao walichukua hatua gani?
 
Last edited by a moderator:

Mafundisho potofu haya. Mwanaume hafundishwi kung'ata bali makonde! Kung'ata kazi ya mabinti.

Akija kumng'ata mkewe utajibu kwa Mungu.
Hahahahaha lol. Na akija kumtia makonde mkewe utajibu wewe kwa Mungu
 
hao watoto walikuwa wakimfanyia bullying.na bullying ikizidi kiu kweli mtoto anaweza akaichukia shule au maendeleo yake yakashuka darasani.tatizo ni hao walimu wameshindwa vipi kulitatua hilo tatizo likawa bado linaendelea?hao watoto wanaomfanyia hivyo lipo jambo ambalo kwa wao ni thretened{maybe mtoto wako amewazidi kiakili}kwa hio wao wanalipiza kwa kufanya hivyo.ki ukweli kama mzazi unaumia ukiona mtoto wako kama anapigwa na hakuna kinachotendeka.mimi nafanya kazi shule naona hayo matukio sana tu,na wapo wanafunzi wanasema kabisa mama ameniambia mtu akinipiga na mimi nipige.ingawa unawaambia is an acceptable behaviour hutakiwi kufanya hivyo.ki ukweli kama mzazi sikulaumu kwa uamuzi wako,lakini na hao walimu wana makosa yao.kwa nini usiombe ufanyike mkutano baina ya hao walimu na hao wazazi,uelezee malalamiko yako,na wajaribu kuweka adhabu kali kwa wanafunzi wanaowanyanyasa wanafunzi wenzao.na hao hao walimu wanatakiwa kuwapa funzo wanafunzi kuhusu bullying
 
pole mwali wangu!
hii huwatokea wazazi wengi!hata mi kuna siku nilimwambia kadada kangu wakiingiia anga zake awape nakozi!
walikuwa wanamwonea balaa!mara wamlie vitu vyake mara arudi kafumuliwa nywele,mara wamemnyang'anya juice!nikaona huu ujinga!nikampa maujanja thanks God sijapata kesi mpaka leo,hapo kalikuwa nursery,sa hivi grade II.sisikii maonevu yoyote na yuko shule nyingne!
ah wakati mwingie watoto wanaonewa sana shuleni jamani!lol
hapa niliweka ualimu pembeni nikawa mama mwingine tu aliyeumia kwa mwanae kudundwa kila siku shuleni!
 
kwakweli hilo sina hakika nalo kama walikuwa suspended ama vipi. ila tu simuoni mwanagu kama mkosa ila sasa nashindwa kujua nitumie mbinu gani kumfunza mwanangu kwamba hana makosa katika hili.

Naomba usome tena post yangu utanielewa vizuri,ila poa kwanza.
 
Pole sana gfswonin! Nimefurahi ulivyo jaribu kumjengea ujasiri mtoto wako hasa ukizingatia ni wa kiume!

Mimi binafsi nilisha kutana na mtihani kama huo kuna mdogo wangu alikuwa ana pigwa shuleni akiwa form one na alikuwa akirudi ana niambia kuna watu wanamuonea nikamwambia aseme kwa walimu lakini akarudi anasema bado wanaendelea kumsumbua, nilichomwambia ni kwamba kama yeye ana ona ni vizuri kuendelea kuonewa aendelee na sitaki aje kunishitakia.Tangia hapo kwakweli siku sikia mashitaka.

Kwanza hao walimu ni waajabu kwani kipindi mtoto ana umizwa na wanapewa taarifa walikuwa hawazifanyii kazi?! Mwambie huyo mamdogo wako aende aongee nao walimu na awaeleze kabisa na awaulize kwa nini mwanao anarudi ameumizwa na hakuna wanalo fanya?

Hila kusema ukweli hiyo shule hawajui kuwaangalia watoto na matunzo hawajui, maana hadi mtoto ana pigwa kila siku hao wako wapi?
 
gfsonwin, kwa upande wangu naona ndugu yangu Asprin na Zion Daughter wameeleza vizuri sana. Mtoto hana hatia yeyote maana ametekeleza kile ambacho mama ulimuelekeza kukifanya. Naamini ulichoka kumepeleka mwanao hosp na kuuguza madonda yake kutokana na kudundwa na wenziwe na sasa ni zamu za wazazi wa hao wengine nao waonje chungu ya kuuguza watoto wao.

Mbali na hayo, kilichonifurahisha ni kuwa mwanao sasa amepata confidence kwamba ana uwezo wa kumdunda mtu kitu ambacho hakuwa nacho hapo mwanzo na nahisi ujasiri huu utamsaidia hata kugombea uongozi kokote huko baadaye na kumpa uwezo wa kujieleza na kujiamini.

Kwa upande wa mtoto usimlaumu sana kwa alichokifanya ila mwambie akichokozwa kuanzia sasa atoa taarifa kwa mwalimu husika uili sheria ifuate mkondo. Kama walivyosema wengine hapo mwanzo, unaweza kumtetea mtoto kuwa alikuwa anajikinga kutoka na rekodi ulizonazo na tayari alishapewa adhabu ya suspension.

Well done gfsonwin and son!
Mzazi gani anafurahia mwanae kudundwa hovyo?!
 
Last edited by a moderator:
Isnt this the new school ameenda recently? Kama ni hiyo usimuhamishe mtoto. Jaribu kuangalia ni vitu gani vinavutia bullies kama blane alivyosema. Usimspoil sana banaa, a kid doesnt need expensive outstanding stufd unajua?
asante mamii...........inaumiza sana, mtoto anapoonewa. natamani mwanangu awe jasiri na si kibonde ila sasa hata shule hii naiona kama hawako makini na wanafunzi hasa kwenye suala la nidhamu.
 
...hahahah gfsonwin kidume hicho kimepambana..........

Ila seriously, kama mtoto anapigwa mara kwa mara, walimu hawachukui hatua (hapa inakua ya kinidhamu zaidi)
Unadhani ni shuke inayomfaa mtoto? Unadhani hali hiyo naitimuathiri mtoto?

Upande wangu naomba zungumza na mtoto kwa lugha ya upole na kwa utaratibu.....ila hebu mtafutie mtoto shule ambayo walimu wapo macho na watoto wote.....inayowafundisha kupendana na disciplin kiasi kuwa watoto wanajua kuwa ni
vibaya kupigana shuleni,itamsaidia mtoto kufurahia maisha yake ya shuleni

ila kwa wakati huu zungumza tu na walimu, na ukizungumza nao usisahau kuwauliza je mtoto aliyemuumiza mwanao last time alipewa adhabu gani? Kusije kukawa na double standards, wape malalamiko yako, waulize toka uwalalamikie kupigwa na kuumizwa kwa mwanao walichukua hatua gani?

asante sana BT, nitajitahidi kumuonyesha upendo zaid na kwamba yeye sio mkosaji.
kwakweli waalimu wa hii shule hasa mwl wa darasa lake sijui kwanini huwa anamwona mwanagu kama mtoto asiyekuwa na mtetezi, mara zote nimekuwa naenda shule naripoti sipewi taarifa kama waliompiga wamepewa suspension ila kwa mwanangu mara ya kwanza kafukuzwa nimeumia sana.
 
Isnt this the new school ameenda recently? Kama ni hiyo usimuhamishe mtoto. Jaribu kuangalia ni vitu gani vinavutia bullies kama blane alivyosema. Usimspoil sana banaa, a kid doesnt need expensive outstanding stufd unajua?

it isn't may dearest, and amesoma hapo since KG na mpaka leo he is in grade 4 amekuwa na senario za kuonewa tu, at first nilipresume ni upepo tu utapita vilipozidi nilifuatilia na ndipo nilipogundua kwamba kuna ushindani wa kitoto tu kwani amekuwa akifanya vzr sana darasani. sasa vijizawadi vile anavyonunuliwa kama motivation vinawafanya wenzie wamuonee. king'asti angekuwa mdogo wake ningesema ni mtundu ila kwa huyu yaani sijui kwann anaonewa manake anapenda wenzie na si msumbufu basi tu hana bahati ya kuthaminiwa na wenzie inaniumiza sana.
 
gfsonwin, kwa upande wangu naona ndugu yangu Asprin na Zion Daughter wameeleza vizuri sana. Mtoto hana hatia yeyote maana ametekeleza kile ambacho mama ulimuelekeza kukifanya. Naamini ulichoka kumepeleka mwanao hosp na kuuguza madonda yake kutokana na kudundwa na wenziwe na sasa ni zamu za wazazi wa hao wengine nao waonje chungu ya kuuguza watoto wao.

Mbali na hayo, kilichonifurahisha ni kuwa mwanao sasa amepata confidence kwamba ana uwezo wa kumdunda mtu kitu ambacho hakuwa nacho hapo mwanzo na nahisi ujasiri huu utamsaidia hata kugombea uongozi kokote huko baadaye na kumpa uwezo wa kujieleza na kujiamini.

Kwa upande wa mtoto usimlaumu sana kwa alichokifanya ila mwambie akichokozwa kuanzia sasa atoa taarifa kwa mwalimu husika uili sheria ifuate mkondo. Kama walivyosema wengine hapo mwanzo, unaweza kumtetea mtoto kuwa alikuwa anajikinga kutoka na rekodi ulizonazo na tayari alishapewa adhabu ya suspension.

Well done gfsonwin and son!
Mzazi gani anafurahia mwanae kudundwa hovyo?!

HP hakuna mtu duniani ambaye anaweza kuvumilia mwanae aonewe, na kamwe hakuna mtu anayetaka mwanae awe mgomvi, ila tu mazingira ya shule zetu ndo hivyo. nitajitahd sana kumuelewesha aelewe na mama mdogo nimesha mwambia aende na aseme atamalizana nae nyumbani.
 
Pole sana gfswonin! Nimefurahi ulivyo jaribu kumjengea ujasiri mtoto wako hasa ukizingatia ni wa kiume!

Mimi binafsi nilisha kutana na mtihani kama huo kuna mdogo wangu alikuwa ana pigwa shuleni akiwa form one na alikuwa akirudi ana niambia kuna watu wanamuonea nikamwambia aseme kwa walimu lakini akarudi anasema bado wanaendelea kumsumbua, nilichomwambia ni kwamba kama yeye ana ona ni vizuri kuendelea kuonewa aendelee na sitaki aje kunishitakia.Tangia hapo kwakweli siku sikia mashitaka.

Kwanza hao walimu ni waajabu kwani kipindi mtoto ana umizwa na wanapewa taarifa walikuwa hawazifanyii kazi?! Mwambie huyo mamdogo wako aende aongee nao walimu na awaeleze kabisa na awaulize kwa nini mwanao anarudi ameumizwa na hakuna wanalo fanya?

Hila kusema ukweli hiyo shule hawajui kuwaangalia watoto na matunzo hawajui, maana hadi mtoto ana pigwa kila siku hao wako wapi?

asnte sana loya wangu. najua kesi ikiwa ngumu nakutafuta lol!
 
pole mwali wangu!
hii huwatokea wazazi wengi!hata mi kuna siku nilimwambia kadada kangu wakiingiia anga zake awape nakozi!
walikuwa wanamwonea balaa!mara wamlie vitu vyake mara arudi kafumuliwa nywele,mara wamemnyang'anya juice!nikaona huu ujinga!nikampa maujanja thanks God sijapata kesi mpaka leo,hapo kalikuwa nursery,sa hivi grade II.sisikii maonevu yoyote na yuko shule nyingne!
ah wakati mwingie watoto wanaonewa sana shuleni jamani!lol
hapa niliweka ualimu pembeni nikawa mama mwingine tu aliyeumia kwa mwanae kudundwa kila siku shuleni!

mwali inauma usipime, ila sijui kwann walimu wa shule za private wako kipesa zaid.
 
wala hujakosea,mwache mtoto auvue upole!!wewe piga kazi,mamdogo ataweka sawa
 
Waswaili walisema kuzaa si kazi, bali kulea. Huyo mtoto wako yupo wapi, analelewa na nani, na shule ya aina gani anayoenda?. Kuna shule zengine zinaaribu watoto pia, kutokana na mazingira. Kama mzazi hilo jua.
Kumfundisha mtoto wako kujiami sio kosa. Kama unaona wanamuonea sana muamishe mpeleke shule ingine. Na hao waalimu ni waonevu, iweje wako akipiga asimamishwe shule na wenzie wakimpiga hawasimamishwi. pole kwa matatizo hayo
 
Pole sana gfsonwin. Kwanza inabidi upate maelezo toka kwa mwanao kama alichokozwa tena au yeye ndiye aliyekuwa mchokozi? je, kama alichokozwa kuna mashahidi (rafiki zake na wanafunzi wengine) wanaoweza kuthibitisha kwamba alichokozwa?. Hilo la kujitetea kila anapochokozwa libaki pale pale. Yeyote anayemchokoza ni lazima arudishe mapigo ila mwambie kwamba kabla ya kuanza kurudisha mapigo atafute mashahidi kwa kufanya yafuatayo. "Fulani na fulani (majina ya marafiki zake au wanafunzi wenzie ambao watakuwa eneo la tukio) mnamuona fulani ananichokoza?" Nikimpiga asije kwenda kushtaki kwa Mwalimu." Hii itakuwa ni njia nzuri ya kuwa na mashahidi wa kuthibitisha kwamba alichokozwa. Kama yeye ni mchokozi basi muonye aache uchokozi madhara yake ameyaona. Kamwe usimruhusu kuonewa na yeyote.
 
Last edited by a moderator:
Asprin ujue niliwaza nikupigie wewe nikuombe unisaidie kwenda huko shule, manake nataka mwanangu nae awe jasiri na sioni kosa manake nimekuwa nikilalamika sana juu ya watoto kuachwa kupigana hovyo, ingawa waalim wao hawako makin katika hili. pia nimewaza kumuhamisha tu shule manake naona mapaka afike grade 7 nitakufa kwa presha.
hiyo ya kumpigia Asprin akakusaidie pia ni wazo zuri, kama mamdogo ni mpole vile anaweza kuchanganya madesa na mwisho mtoto akaadhibiwa.
nakumbuka siku moja nilikutana na kisanga fulani, nilichokumbuka ni kuwaambia wale jamaa ngoja nimwite husband.... nikachukua simu nikampigia friend, moja kwa moja nikaanza husband njoo sehemu fulani kuna watu wananiletea dhahama hapa. jamaa alikuja moto umemuwaka anawagombeza mmemfanya nini wife wangu, kumbe mkwala tu
 
Last edited by a moderator:
Hii Thread imenikumbusha utotoni mpaka nimebaki najicheka mwenyewe.

Nakumbuka nilikuwa naibiwa Kalamu kila siku shuleni, Maza alivyokerwa na maombi yangu ya Kalamu kila siku akaniambia na mimi niwe naiba za wenzangu pia. Basi nilianza kuziiba mpaka nikajaza Droo ya meza Home kwa aina mbali mbali za Peni, mpaka zile za waalimu (nyekundu).

Ilivyogundulika nina Kalamu nyingi sana nikaletewa noma kwa nini naiba Kalamu za watu, nikajitetea kwamba nimeamua kulipiza kisasi. Maza ilibidi awe mpole akanikanya juu ya hiyo tabia, japo nilimsikiliza lakini katabia ka kudokoa Kalamu za wenzangu sikukaacha abadani.

Kisa kingine: Kuna Jamaa mtaani alikuwa anapenda sana kutuonea mimi na mdogo wangu, kila tukimshtaki kwa Mzee, tunajibiwa kwamba ni kwa nini tunakubali kupigwa na mwanaume mwenzetu. Kwa kuwa Jamaa alikuwa ametuzidi Umri na Umbo siku moja tulikusanya mawe ya kutosha tukamvizia njia anayopita, alipotokea tu, tukampiga na mawe ya kutosha na kumjeruhi sana, ikabidi apelekwe Hospitali kwa Gharama za Mzee wetu. Na kwakuwa Mzee aligundua kosa lake wala hakutogombeza, zaidi alituasa tusipende kuwafanyia wenzetu fujo. Ila Mbabe wetu naye alituheshimu milele.

Maneno tunayowaambia watoto yana athari kubwa sana juu ya matendo yao.

But all in all, mwambie mwanao asiwe anaanzisha yeye ugomvi ila asiruhusu mtu yeyote amwonee.
 
TANMO nakushukuru sana kwa ushuhuda wako. nitafanyia kazi mawazo yako
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom