Ninunue ipi kati ya Bajaj na Gari kwa biashara ya Bolt

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
11,542
12,404
Wakuu nataka kukunua kati ya bajaj au gari ndogo mfano Vitz/IST or the like ili nimweke dereva apige biashara ya Uber au Bolt.

BAJAJ
Kwa upande wa Bajaj ikiwa mpya bei ni 7.35M na kwa sasa walio wengi wananunua na kuingia mkataba na dereva kwa miaka miwili ambapo kwa siku ni 20k bila kujali ni J1, J2 au Sikukuu hivyo kufanya kwa miaka miwili kuwa 20,000× siku 730=14,600,000. hapo gharama za service ni zake na baada ya miaka miwili unamwachia Chombo.

GARI
Kwa upande wa gari kwa kweli sijajua chochote zaidi ya kujua tu kwa 7.5M nitapata gari ndogo itakuwa kwenye hali nzuri lkn bado tatizo kujua mfano kwa siku inaingiza kiasi gani hasa kwa sababu hii itategemea request ya wateja hivyo hapa hasa ndipo ningehitaji msaada ili niweze kufikia maamuzi kwa kipi nikichukue kati ya Bajaj mpya ambayo baada ya miaka miwili nitamwachia dereva au gari ambayo kwa sasa katika kipindi cha miaka miwili sijajua itaniingizia kiasi gani.

Ninaomba mwenye kujua hasa kwa upande wa gari plz lets share exprience.

Naomba kuwasilisha.
 
Kiuchumi Bajaj mpya ikipata Dereva anayejitambua itakurejeshea pesa mapema zaidi. Maana mpaka ianze kusumbua kuhitaji major maintenance inaweza kuwa imesharudisha pesa.

Ila gari ya kununua mkononi kwa Mil 7.5 kuna chances kadhaa ikawa kimeo.
 
Tafuta passo , show room inafika mpaka 6.5 , hapo jan japan namanga , weka kwenye uber , biashara ikiwa ngumu kwa kumpa dereva unafanya mwenyewe , ukishindwa kabisa unauza au inakuwa gari yako binafsi ya misele.
PASSO? MIL 6.5 show room? Na kodi imelipiwa?

Aisee nipo nyuma sana ya dunia kama majibu ya maswali yote hayo hapo yatakua NDIYO.
 
Wakuu nataka kukunua kati ya bajaj au gari ndogo mfano Vitz/IST or the like ili nimweke dereva apige biashara ya Uber au Bolt.

BAJAJ
Kwa upande wa Bajaj ikiwa mpya bei ni 7.35M na kwa sasa walio wengi wananunua na kuingia mkataba na dereva kwa miaka miwili ambapo kwa siku ni 20k bila kujali ni J1, J2 au Sikukuu hivyo kufanya kwa mwaka kuwa 20,000× siku 730=14,600,000. ha
Kamanda mkataba wa Bajaji ni miezi 18 sio miaka miwili hili ninauzoefu nalo

Hiyo miaka miwili ni gari.
 
PASSO? MIL 6.5 show room? Na kodi imelipiwa?

Aisee nipo nyuma sana ya dunia kama majibu ya maswali yote hayo hapo yatakua NDIYO.
Hiyo hapo attachment , huwa wanatoaga hizo ofa mara nyingi tu , ukikuta ofa zimeisha zinakuwa 8.5 , hapo ni kila kitu

Screenshot_20210629-223712_Instagram.jpg
 
Nenda mikoani kanunue bajaji chakavu hata laki 7 aifiki,ilete mjini peleka gereji mburahati huko gharama kuirudisha barabarani haizidi milion 2.

Kwa hiyo ela unapata bajaji 2 na kuziweka barabarani.

Just imagine yourself
Umeongea bonge la point, kweli mkoani bajaji used zipo nyingi ukibahatika ya 3M ni kama mpya
 
Back
Top Bottom