Nini maana ya maneno haya? "Chai ya moto, chai ya tangawizi na chai kavu"

testifier

Member
Apr 21, 2021
47
125
Wakuu, poleni na majukumu. Naomba kuuliza nini maana ya maneno haya kama yanavyotumika hapa JF:

1. Chai ya moto
2. Chai ya tangawizi
3. Chai kavu

Nimeyaona yakitumiwa na wachangiaji wa nyuzi mbalimbali ila mimi sielewi wanamaanisha nini wanapoyatumia. Naomba kujuzwa ili twende pamoja
 
Singo

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,126
2,000
Umewahi husianisha kati ya kinachoitwa chai na kilichoandikwa?
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
165,476
2,000
Wakuu, poleni na majukumu. Naomba kuuliza nini maana ya maneno haya kama yanavyotumika hapa JF:
1. Chai ya moto
2. Chai ya tangawizi
3. Chai kavu
Nimeyaona yakitumiwa na wachangiaji wa nyuzi mbalimbali ila mimi sielewi wanamaanisha nini wanapoyatumia. Naomba kujuzwa ili twende pamoja
Habari ya kutengeneza au kutunga iliyojaa uongo ambao mtoa mada hujitahidi kuifanya ya kweli
 
iam Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
2,418
2,000
Hii nayo mbona kama chai
20210517_215104.jpg
 
kindikinyer leborosier

JF-Expert Member
Jan 6, 2018
257
500
chai ni story za kutunga... sasa watu huongeza vionjo vingine mfano: hii ya leo mbona haina vitafunwa, au chai haina sukari kabisa, au umejaza tangawizi, kulingana na vionjo tuu vya mwandish, shabaha ya kusema chai ni mhusika ametoa hadithi ambayo haina uhalisia..
 
Singo

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,126
2,000
Laa. Nimeachwa kwenye mataa.
Kapitie tena kule thread ya Kula kimasihara, soma pages hata page 3 za mwisho kisha ukiona maelezo ya mtu yameqotiwa kuwa ni chai ,jiulize wewe kwa upande unaonaje ? Kama chai kadhaa za kule hautaelewa kuwa ni chai ,basi unasafari ndefu
 
testifier

Member
Apr 21, 2021
47
125
Kapitie tena kule thread ya Kula kimasihara, soma pages hata page 3 za mwisho kisha ukiona maelezo ya mtu yameqotiwa kuwa ni chai ,jiulize wewe kwa upande unaonaje ? Kama chai kadhaa za kule hautaelewa kuwa ni chai ,basi unasafari ndefu
Nimeishaelewa, mkuu, maana ya chai. Wachangiaji wote wa mwanzo walikuwa wananionjesha chai baridi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom