Naomba maana halisi ya haya Maneno kwa Kiswahili

jkipaji

JF-Expert Member
Sep 22, 2019
5,705
7,583
High Court Judgement

"I hereby quash the entire proceedings and judgment of the lower tribunal for being nulity, Everything in ownership of the disuputed plot remains as if there was no case filed before, The house or plot No 409 Block Z Usagara East within Tanga City will remain the property of late Sylvester Michael Mfumia, as its transfer to the respondent is tented with fraud, liable for distribution to his heirs, Whoever need (sic) distribute to challenge the ownership will have to wait till filing of the inventories in respective court"

Wakuu naomba maana halisi ya haya Maneno kwa Kiswahili!

Asanteni sana naomba kuwasilisha!!
 
Ameshinda rufaa, kwa sababu uuzwaji wa hiyo nyumba/kiwanja ni batili.
Mtu yeyote anayetaka kupinga umiliki asubiri kuorodheshwa kwa mali za marehemu katika mahakama ya mirathi ndiyo apinge umiliki.
 
",,,,,,,,I hereby quash the entire proceedings and judgment of the lower tribunal for being nulity, Everything in ownership of the disuputed plot remains as if there was no case filed before, The house or plot No 409 Block Z Usagara East within Tanga City will remain the property of late Sylvester Michael Mfumia, as its transfer to the respondent is tented with fraud, liable for distribution to his heirs, Whoever need (sic) distribute to challenge the ownership will have to wait till filing of the inventories in respective court,,,,"!!!!! Wakuu naomba maana halisi ya haya Maneno kwa Kiswahili! Asanteni sana naomba kuwakilisha!!

Ninafuta muenendo na hukumu iliyotolewa na baraza, umiliki wa hiyo ardhi utabaki kama ulivyokuwa,kama hakuna kesi iliyowahi kufunguliwa(yaani umiliki unabaki ule wa awali kabla ya kesi ambayo maamuzi yake yametenguliwa hapo). Umiliki wa Nyumba plot no 409 Block Z usagara mashariki wa jini la Tanga utabaki kwa marehemu Sylivester Michael Mfumia,sababu uhamisho wa umiliki kwenda kwa mdaawa ulijawa na udanganyifu,yeyote atakayetaka kupinga umiliki asubiri mpaka inventories iwe file mahakamani.
 
Ninafuta Hukumu na amri zote zilizotolewa na mahakama za chini (baraza la ardhi) kwa kuwa ni batili. Kila kitu kuhusu umiliki wa eneo lenye mgogoro kinabaki kama ilivyo kana kwamba hakuwahi kuwa na kesi. Kiwanja au nyumba namba 409 kitalu Z Usagara East kinabaki kuwa mali ya marehemu Mfumia, kwa kuwa taratibu za kuhamisha umiliki zilitawaliwa na utapeli. Kiwanja kitagawiwa kwa warithi wa marehemu. Yeyote atayetaka mgao ili kupingaumiliki huo asubiri mpaka orodha za mali za mirathi itakapowasilishwa mahakamani palipoombewa mirathi.
 
Asante sana Mkuu! Je kutokana na maamuzi hayo kuna Jinai hapo!!??
 
Jaji aliposema kuna 'fraud' maana yake utapeli au udanganyifu umethibitika. Inaweza kuwepo hiyo jinai ila haijasemwa ni nani aliyefanya udanganyifu ili sasa ndio achukuliwe hatua za kisheria.
 
Asante sana Mkuu! Haya ndiyo Maneno ya Jaji baada ya kusema kuna fraud! ",,,,,,, " The fake administrator (Sadiq Mfumia) has to be arrested and tell the authorities how he secure that Form No IV which assisted the respondent to commit such evils (May God punish them all) mwisho wa kunukuu!!
 
Ninafuta Hukumu na amri zote zilizotolewa na mahakama za chini (baraza la ardhi) kwa kuwa ni batili. Kila kitu kuhusu umiliki wa eneo lenye mgogoro kinabaki kama ilivyo kana kwamba hakuwahi kuwa na kesi. Kiwanja au nyumba namba 409 kitalu Z Usagara East kinabaki kuwa mali ya marehemu Mfumia, kwa kuwa taratibu za kuhamisha umiliki zilitawaliwa na utapeli. Kiwanja kitagawiwa kwa warithi wa marehemu. Yeyote atayetaka mgao ili kupingaumiliki huo asubiri mpaka orodha za mali za mirathi itakapowasilishwa mahakamani palipoombewa mirathi.
Mkuu hii Hukumu umeitafsiri vizuri sana kama vile wwe ndiyo Judge mwenyewe uliyo toa hiyo hukumu!!!! Asante sana!!
 
Asante sana Mkuu! Haya ndiyo Maneno ya Jaji baada ya kusema kuna fraud! ",,,,,,, " The fake administrator (Sadiq Mfumia) has to be arrested and tell the authorities how he secure that Form No IV which assisted the respondent to commit such evils (May God punish them all) mwisho wa kunukuu!!
Ikitolewa hukumu ya Mahakama Kuu,haiwezekani,kufungua kesi,kupinga hii hukumu ya Mahakama Kuu?
 
Ameshinda rufaa, kwa sababu uuzwaji wa hiyo nyumba/kiwanja ni batili.
Mtu yeyote anayetaka kupinga umiliki asubiri kuorodheshwa kwa mali za marehemu katika mahakama ya mirathi ndiyo apinge umiliki.
Hakushinda, ameshindwa kwa sababu alitaka kutapeli kwenye ununuzi wa hiyo nyumba kwenye kiwanja husika.
 
Unaweza kuomba review by half bench.
Kama kuna fraud Mahakama ya Rufaa si itaweza kuitupilia mbali hiyo review yenyewe, au wao Mahakama ya Rufaa fraud huwa hawangali sana kwenye civil court!!??
 
Kama Kuna evidence au Sheria imekiukwa katika kuwndesha kesi unaweza kuomba review hata kama ni fraud.
 
Je Kama Sheria imekiukwa kweli, je inaweza ondoa kosa langu la Kugushi Mirathi!?? Naomba ufafanuzi hapo!!
 
Back
Top Bottom