Je, ninaishi na mtu asiyeonekana? Vitu kupotea ndani ni dalili ya nini?

Kipenseli

JF-Expert Member
Feb 9, 2020
800
1,050
Habari zenu wana JF?

Nilikua naomba nipate experience kwenu, hivi inaashiria nini vitu vidogo vidogo kupotea ndani na nikiwa nakaa mwenyewe chumbani (nyumba ina wapangaji wengine).

Yaani kitu naweza kukiweka leo kesho au baada ya siku mbili nikitaka kukitumia sikikuti, je ni dalili kua ninaishi na mtu asiyeonekana?

Kwa mara ya kwanza niliweka tangawizi (ginger) mezani na huwa natumia kwenye kuweka kwenye chai, ila siku moja nikastop kupika chai, siku iliyofata meza naikuta nyeupe na ni palepale nilipoweka zile tangawizi, siku iliyofuata nimeweka viungo vya pilau nilitumia kupikia na pakiti zilizobaki nikaziacha hapo mezani, kesho yake nikataka kuzitumia sikuziona.

Leo ndo nimechanganyikiwa kabisa mpaka nimeamua kuja kuuliza humu, nashindwa hata kuelewa, ila masaa machache yaliyopita nilihitaji kupika mwiko hauonekani na wakati nimeuacha hapa ndani kabla sijaenda kununua mazaga mengine kwa ajili ya mboga.

Kwa hii situation mnadhani shida ni nini wakuu? Mpaka muda huu nimeshindwa kulala kwa hii hofu niliyo nayo.

Kila ninapotoka ninafunga mlango na funguo naondoka nayo, je ni nini kinaendelea jamani, inaweza kua ni shida gani?

UPDATES

Wakuu, tatizo la kupotea kwa vitu getoni nimeamua kulihusisha moja kwa moja na maswala ya ulozi japo imani yangu ilikua nzito sana kwenye masuala haya ya kiimani, lakini mwisho wa siku imenibidi tu niamini tu tena kwa moyo mkunjufu.

Sababu za mimi kuamini hivyo ni kwamba kati ha vitu nilivyoorodhesha (vilivyopotea) sikukiona hata kimoja tena baada ha kutoonekana (pamoja na usafi na kuchunguza kila pembe humu ndani)

Mbili, Kuna alama mwilini hua najikuta nazo ila nikifanya uchunguzi zaidi wa hizo alama (kama kovu) baada ya siku moja vinapotea, hii ni zaidi ya mara moja najikuta na alama(kovu) kama ya kuchanjwa na wembe au pini yenye ncha kali lakini sikumbuki wapi na lini niliumia....

2019, Nilipata tatizo la Hearing Loss , Kipindi ambacho nilihitaji kuanza Advance Level, ndugu na jamaa walihusianisha jambo hili na masuala ya ulozi hapa mtaani ninapoishi (Elimu yangu ni ya kuunga unga, nimesoma ukubwani kwenye Centres mbili tofauti), nilibisha sana hili jambo na kwasasa nimeshakua kiziwi na haya matukio jinsi yanavyokwenda nishaaminj kua kuna mambo yalifanyika

attachment nimeweka alama niliyoinotice kwenye eneo paja alaf kikatoweka
View attachment 2769072
 
Back
Top Bottom