Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,252
- 113,645
Watanzania bwana, mnaongelea ya kumkumbuka mwalimu tu, ongeleeni mmefanya nini kumuenzi mwalimu? Sisi wote kwa kisi kikubwa ni wasaliti wa yale aliyotufundisha Mwalimu.
Sioni hata sababu ya kufurahia siku ya kifo chake, mimi huwa
ni siku ambayo ninaona aibu kwamba siwezi kuyatimiza yale yote niliyokuwa naimba nikiwa kijana, nikiwa chipukizi wa Nyerere, na badala yake naona wote sasa tumejaa ubinafsi tu.
Labda leo mtamkumbuka vizuri Mwalimu kwa kutoa sehemu ya ulicho nacho na kuwasaidia Watanzania wenzetu, ndugu zetu na majirani zetu ambao ni hoi kuliko sisi.
Nakaeribisha mashambulizi.
Anzisha thread yako mwenyewe itakayokuwa mahsusi kwa kumuenzi......
Swali kubwa kwetu sisi ni hili, mwalimu kama kiongozi alituachia umoja wa kitaifa, lugha ya kitaifa, amani na mshikamano kama taifa, baada ya hapo sisi tumefanya nini? Mwinyi atakumbukwa kwa lipi? Mkapa atakumbukwa kwa lipi, JK atakumbukwa kwa lipi? Jiulize mpaka leo, CCM inashinda kwa kutumia mafanikio ya mwalimu personally maana kama yangekuwa na chama basi tungeyaona hata mengine maana chama ni kile kile, lakini wapi.
Anyway................tuzidi kudai mabadiliko, tutafika.
Nyani,
Kumbe kila mtu anaanzisha thread yake mwenyewe?
Nilifikiri kila thread inayoanzishwa kila mtu yuko free kuchangia?
As much as Mwalimu alikuwa mchapakazi mzuri na pan Africanist nilikuwa sikubaliani na sera zake za kiuchumi ambazo ziliturudisha nyuma miaka 50, Vita na Uganda havikustahili damu ya Mtanzania yoyote yule,alitakiwa awaunganishe watu wa dini zote lakini mwishowe alikufa huku nchi ilikiwa iko divided kidini kuliko wakati mwingine wowote ule, japo alikuwa nawangangania wenzake wahamie Dodoma lakini yeye hakuhamia huko, Kodi zetu zilitumika kumjengea nyumba kwenye jiwe huko kijijini kwake lakini baada ya miezi michache aliamua kurudi Msasani.
Mwisho naweza kusema kitu pekee ambacho kilichonitia kuhusu Mwalimu, hakuwa MWIZI kama watawala waliomfuata lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa alikuwa ni DIVISIVE figure na haswa baada ya kuwa kumbatia wadini ambao walimpotosha sana
Masanja,
Hizi ni mbegu zilizopandikizwa na baadhi viongozi alokuwa akiwazungumzia ktk mahojiano yake na Ikaweba Bunting. Kwa kiasi kidogo sana wamefanikiwa na kamwe wasingeweza kuyasema haya akiwa hai.
Game Theory,
Mjomba kusema Nyerere aliturudishja nyuma miaka 50 hizi ni habari za Uongo. Tanzania kama yalivyokuwa mataifa mengine tulikuwa mbele miaka 10 kutokana na ujenzi wa miundombinu mipya. Wengine wote waliyakuta mengi yamewekwa na Mkoloni, sema Ujamaa ulikuwa mrengo ambao hauwezi kufanikiwa ktk mazingira ya kibiadamu.
Mimi husema Ubepari ni sawa na Ngono. Pamoja na hatari zake zote za HIV, kisonono, kaswende na kadhalika kamwe hatuwezi kuepuka. Ni wajibu wetu hata ktk dini. Bila Ubepari hakuna biashara, hakuna biashara hakuna Uchumi, mawasiliano mazuri kati ya jamii na kadhalika.
Ni maisha ambayo kila mmoja wetu ni wajibu wake kutafuta riziki zake kupitia hatua hii isipokuwa Mwl. Nyerere ambaye alikuwa Mkatoliki aliamini kuwa kila mtu anaweza kuwa Padre.. Ngono ni haramu hadi pale utakapo fikia umri fulani.
Na huo Umri ktk uchumi wetu alidhani Tanzania inakuja fikia umri wa kujitosheleza wenyewe (KUJITEGEMEA) hivyo kutakuwepo na level ground ya Ubepari baina yetu na nchi tajiri. This was Impossible!...
Mwisho kuna jamaa mmoja toka kwa michuzi ameweza kuandika mengi mazito ya kumbumbuka mwl. JKN hasa ktk ELIMU. Ni vitu ambavyo wengi wetu hatukuviona kama ni big deal lakini duh! Yes mchonga alikuwa KIONGOZI.
Mungu amzidishie pepo!
Ilikuwa Mei Mosi 1985, iliyofanyika Kitaifa Mkoani Tanga na kuhudhuriwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya Madola Bw. Sherdath Ramphal (or similar sounding name). Siku ya pili yake mvua kubwa ilinyesha mjini Tanga na kufanya barabara kubwa za lami zisipitike hasa kutokea Old Nguvumali, Kisosora, Chumbageni n.k Ikabidi Mwalimu na msafara wake wapite "Uswahilini". Ndipo nilipopata kuona Mwalimu alivyokuwa mtu wa watu... mimi na ndugu zangu tukawa tumejipanga kwenye geti la nyumbani (tulikuwa na kakibanda kakuuza machungwa toka Muheza) basi jua likiwa limeanza kupiga, na akiwa amechelewa kwenda uwanja wa ndege, msafara wake ulipita taratibu katika barabara hiyo ya mashimo (kwani haikuandaliwa kwa ajili ya msafara!) basi tu yeye kageuka upande mmoja tu anapungua watu, ndipo binamu yangu wa kike alipopiga kelele "Na huku!" Mwalimu akitabasamu akageuka na kutupungia... Ilikuwa ni siku ya furaha kwamba na sisi "tumesikiwa"... Since then, I have made it my mission... to be heard by our leaders!!