BOB, kitu kikubwa ambacho nadhani walio wengi tunashindwa kuelewa ni kwamba Nyerere alikuwa binadamu kama wengine. Au kwamba ukiwa kiongozi unakuwa tofauti na wengine. Nchi yetu TZ hatuongozwi na wala hatutegemei kupata viongozi walio tofauti na sisi kutoka sayari nyingine (BOB, you once said..leadership ni reflection ya sisi wenyewe wananchi). kwa hiyo kama na sisi tulivyo na ubinafsi, kujipendelea na familia zetu, kuwa wanafiki nk, na viongozi wetu wako hivyo hivyo! Jiulize kwa nini wewe uliondoka TZ? ni kwa sababu ya kutafuta maisha kwingine kwa ajili yako na familia yako! kwa hiyo hata hawa viongozi wetu wanamatamanio hayo hayo ya kuwapeleka watoto wao huko ughaibuni, kuendesha magari mazuri nk.
Now, can you get a leader ambaye hayataki mambo wewe unayoyataka ya anasa? hapana! hata sisi kama wananchi tunajua fika kwamba viongozi wetu ni kama sisi, kwa hiyo tunachotaka kutoka kwao ni kuwa na zile minimum standards kusudi wananchi nao wajiletee maendeleo. ni dhahiri kwamba hata huko ulaya na USA viongozi wanaiba, lakini tofauti na sisi wanaiba harafu wanainvest ndani humo humo huku wakizalisha ajira, na wanaiba huku wakiwafikiria watu wao watafaidika vipi, sisi viongozi wetu wanaiba huku wakikimbilia nje, as a result sisi na wao wenyewe hatufaidiki, ila wanafaidika wengine.
Nyerere alikuwa ni bin adam just like you and me, ila sema alikuwa na kipaji cha pekee hakujiweka mbele kuliko wengine na alijaribu KWA NIA NJEMA kujenga mazingira ya wote kufanikiwa (kwa kutoa huduma za muhimu sawa na bure kama elimu, afya nk). Leo hatutegemei JK awe Nyerere, lakini tunategemea hulka ya ubinadam aliyonayo kama wengine ajitahidi atumie zile raslimali tulizonazo kusudi na sisi tujikomboe. So far ameshindwa.
Kama alivyosema BOB, bila ubepari dunia haiwezi kuwa dunia unayoiona na unayoifaidi. Wanaosema kwamba another world is possible, nachelea kukubaliana nayo, hiyo alternative world inawezekana tuu endapo viongozi wataweka mikakati sahihi na kuwaempower wananchi kufaidi raslimali zao, hatuwezi kuendelea kulaumu globalization. I have always said and I will say it again, African Problems emanate from Africans! wazungu wana nafasi ndogo saana katika haya masaibu yayotukuta. Yaani mi nafikiriaaaa mpaka naona kwamba Africa sijui tusaidiwe au tujisaidie vipi!!ahahahah...