Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 90,871
- 106,148
Katika kumkumbuka Baba wa taifa, naomba mchangie kumbukumbu zenu binafsi au zinginezo mlizonazo za hayati Mwalimu.
Nianze mwenyewe: wakati niko mtoto mdogo mwanzoni mwa miaka ya themanini baba yangu mpendwa siku moja alinipeleka kwenda kusali kwenye kanisa la Mtakatifu Peter pale Oysterbay. Siku hiyo tulikwenda kusali hapo kwa makusudi kabisa. Makusudi yenyewe yalikuwa ni kumwona kwa macho Raisi Nyerere na ikiwezekana kumsalimia na kushikana naye mkono. Wakati misa inaendelea mimi mawazo, akili, na macho yangu yalikuwa yameelekezwa kwa Raisi Nyerere. Nakumbuka alikuwa anapenda kukaa pale mbele mbele karibu na altare. Siku hiyo mimi na baba yangu mpendwa tuliwahi na kuapata nafasi ya kukaa kwenye moja ya viti (mabenchi) ya mbele ambapo tuliweza kumwona vizuri Raisi Nyerere. Macho yangu hayakubanduka kwake. Nashindwa hata kusimulia jinsi nilivyokuwa najisikia asubuhi ile. Kwa vile Raisi Nyerere alikuwa na mazoea ya kusalimiana na watu pale nje kwenye ngazi baada ya misa kuisha, mimi na baba yangu mpendwa tuliwahi kutoka na tukajipanga kwenye mwanzo wa zile ngazi za kushukia chini ili tuweze kusalimiana naye na kumwona ka karibu. Ndoto yangu ilitimia pale alipotoka na kuanza kusalimiana na watu. Alipofika tulipokuwa tumesimama sisi akanishika kichwa halafu akanyoosha mkono wake na mimi nikanyoosha wa kwangu na tukasalimiana. Siku hiyo nilikuwa ni mtoto mwenye furaha isiyo na kifani. We fikiria, nimeshikana mkono na Raisi Nyerere...nakwambia nilirudi nyumbani na kuanza kuwatambia marafiki zangu, ndugu zangu, na kila mtu niliyekutana naye. Kamwe sitaweza kuisahau siku hiyo kwani nami nilijipatia sekunde zangu kumi na tano za umaarufu.
Haya washirika wenzangu tuendelee.....