Misemo maarufu ya hekima ya hayati baba wa taifa Mwl J.K nyerere

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,510
14,373
#CHAKUSHANGAZA

Hayati Baba wa taifa amekuwa akiishi katika karne zote kutokana na kauli zake ama misemo yake ambayo imekuwa ikiishi mpaka Leo.

Misemo ya Baba wa taifa imekuwa ikitumika kwa namna mbalimbali kama vile kuonya, kukosoa, kukemea uovu, kuasa jamii juu ya uasi, rushwa, ukuwadi, siasa na mambo mengine mengi misemo ya Baba wa taifa imekuwa ikitumika sana.

Ifuatayo ni baadhi tuu ya misemo ambayo hayati Baba wa taifa alikuwa akipenda kutumia
“Inawezekana tatizo la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni"- Mwl. J. K. Nyerere

“inawezekana, timiza wajibu wako” Mwl JK Nyerere.

“Ikulu ni mahali patakatifu, anaye kimbilia ikulu niwa kuogopwa kama ukoma” Mwl JK Nyerere.

“Ccm sio mama yangu” Mwl JK Nyerere.

“Niliamua waziri achapwe viboko kwa rushwa akitoka amsimlie mkewe”. Mwl JK Nyerere.

“Mtanzania wa leo hawezi kununua watu kabla ya yeye hajanunuliwa!!!”. Mwl JK Nyerere.

“Habari ni habari utasikia fulani kampiga mkewe hiyo si habari, lakini Nyerere kampiga mkewe hiyo ni habari itaandikwa kwelikweli”- Mwl JK Nyerere.

“Kiongozi atakayepokea rushwa, tukimkamata tutamfunga miaka miwili na atapigwa viboko 24; 12 akiingia na kumi nambili akitoka, aende akamwonyeshe mkewe." Mwl JK Nyerere.

“Katika nchi kama yetu, ambayo Waafrika ni maskini na wageni ni matajiri, kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwafrika akiruhusiwa kuiuza ardhi, katika miaka themanini au miaka ijayo, ardhi yote ya Tanganyika itamilikiwa na matajiri wageni, na wenyeji watakuwa watwana. Lakini hata kama wageni wasingekuwa matajiri, litaibuka tabaka la Watanganyika matajiri wajanja. Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu, katika muda mchache, kutakuwa na kundi dogo la Waafrika wakiwa na ardhi na walio wengi watakuwa watwana.”* MWL NYERERE, 1958

“Watanzania wanataka mabadiliko; wakiyakosa ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM” Dodoma, 1995. . Mwl JK Nyerere.

“Mimi nang’atuka, lakini bado nasisitiza kuwa, bila CCM imara nchi yetu itayumba”-1990s. . Mwl JK Nyerere.

“Serikali ikitawaliwa na rushwa haiwezi kukusanya kodi, itabakia kukimbizana na watu wadogo wadogo tu”. Mwl JK Nyerere.

“Serikali ya Tanzania haina Dini”. Mwl JK Nyerere.

“Dhambi ya ubaguzi itawarudi tu naomba Mungu anisamehe lakini na iwarudie”. Mwl JK Nyerere.

“Mimi nimekaa Ikulu miaka 21, kuna biashara gani pale Ikulu?." Mwl JK Nyerere.

“Mara hii tu mmetajirika kiasi hicho? Kama mmeweza kutajirika kiasi hicho katika muda mfupi, fanyeni basi wote tutajirike, kwa nini mtajirike peke yenu?!”. Mwl JK Nyerere.

“Kwa mtu mwaminifu kabisa, Ikulu ni mzigo, si mahali pa kukimbilia hata kidogo”. Mwl JK Nyerere.

“Kaburu ni kaburu tu sio lazima awe na ngozi nyeupe”. Mwl JK Nyerere.

Hakika hayati Baba wa taifa ni taa ing'aayo na isiyoisha nuru milele, kama vijana tuna kila sababu ya kuyaishi maneno matakatifu ya baba wa taifa katika kuhakikisha tunamuenzi kwa vitendo.

Viongozi wa sasa mna kila sababu ya kuyaishi maneno ya Baba wa taifa sio kubaki kuyatumia jukwaani bila utekelezaji wake kwa vitendo, kwa kufanya hivyo tunamdhihaki Baba wa taifa huku aliko.

Baba wa taifa enzi za uhai wake alikuwa akipinga nguvu zake zote ukabila, udini, ubaguzi, ubepari, ujinga, maradhi, ukuwadi, ufisadi na rushwa, pamoja na mambo mengi ambayo alikuwa akikemea waziwazi bila kuogopa.

Kiongozi ni mtu aliyejitoa muhanga kwa ajili ya kulisaidia taifa lake, kwa MWL hakuogopa kuzuiliwa misaada, kuwekewa vikwazo alipambana na wakoloni kweli kweli. Tuungane na viongozi wenye nia ya dhati ya kulifikisha taifa letu kwenye nchi ya ahadi.

KUMBUKA
“Hautakumbukwa kwa ukubwa wa cheo chako, bali utakumbukwa kwa kazi zako nzuri unanizozifanya na kuacha alama"
 
Ubarikiwe sana mkuu kwa kumbukumbu mujarabu ya Mwalimu!!
 
Safi sana. Pia kuna tamko alisema kuna dhambi fulani ukifanya hapa duniani Mwenyezi Mungu hangoji ufike Ahera, Anakuadhibu hapa hapa duniani! Alisema akiwa kachukia lakini inatokea. Hata mahakama ikimwachia aliyetenda kosa haishi kwa amani na kadhalika!
 
Back
Top Bottom