BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,283
Tutaongea mengi sana kuhusu mwalimu,lakini ukweli unabaki palepale,itapita miaka mingi kwa Tanzania kuja kupata kichwa kama kile,hivi utamlinganisha Nyerere na manyang'au wa siku hizi?
Hatukatai Nyerere alikua na mapungufu kama binadamu mwingine yeyote yule,hata mwenyewe aliwahi kukiri kuwa kuna makosa alifanya kama kiongozi kwani hakua malaika,.Ila kaleta mengi sana,ukilinganisha na mapungufu,najua huwezi kupendwa na wote,pia huwezi kukubalika na wote,kwani hata Yesu mwana wa Mungu alipingwa na kusulubiwa sembuse Nyerere.
Mie nakuulizeni hapo ulipo umeifanyia nini Tanzania?Au kulaumu tu,Nyerere kaleta umaskini,maendeleo hayaletwi na mtu mmoja,kama jamii nzima tulikua tunategemea Nyerere ndiye atuletee maendeleo basi mmepotea njia.Alitupa elimu bure ili tuelimike tuje kujikomboa wenyewe,ila cha ajabu elimu aliyotupa ya bure,badala ya kutusaidia,imekuwa mbadala,sasa tunaitumia kuuza nchi,mikataba fake,kutelekeza watanzania Ukraine,ebwana mna mambo ya mzaha,yaani ukisema Nyerere ndo katuletea umaskini,mie sitakutofautisha na Ze Comedy,naona kama vile unaigiza tu.Watanzania tupo milioni 40,je niambie ni nani na kaifanyia nini Tanzania,unaweza kujitolea mfano mwenyewe?Wote ubinafsi umetujaa tu,acheni mzee wa watu apumzike,Mungu asije kutulaani bure,kweli nabii hakubaliki kwao.
Hawa kweli sasa wanakuwa manyang'au, walioweka mbele maslahi yao badala ya nchi, wanaojilimbizia mali kwa kasi kubwa mno kwa kutumia njia za haramu bila woga wowote, kwa kifupi wamewatekeleza Watanzania.