Nini Kumbukumbu Yako Ya Baba Wa Taifa?

Nini Kumbukumbu Yako Ya Baba Wa Taifa?

game theory, nisaidie jambo moja ni nchi gani ya Kiafrika ambayo chini ya viongozi wake imefanya vizuri zaidi katika kipindi cha miaka 23 wakati Mwalimu anatawala Tanzania? Hiyo itatusaidia kuona ni nchi gani zilipiga hatua kuuuuuuuubwa ya maendeleo kuliko Tanzania ya Mwalimu ambayo imerudi nyuma miaka 50!?

BOTSWANA,EGYPT, TUNISIA, SOUTH AFRICA,MOROCCO,MAURITIUS
 
GAME THEORY,
Katika kuendeleza kukubaliana kutokubaliana!...

Nadhani swali uloulizwa lilikuwa nchi gani wamefanya vizuri ktk kipindi cha miaka 23 ya mwalimu. Kwa hiyo nakuomba jaribu kutazama vizuri hali ya nchi hizo ktk miaka hiyo. Mathlan Botswana pamoja na kwamba walikuwa na Utajiri mkubwa wa madini (Almasi) ambaoo ulichangia zaidi ya asilimia 50 ya GDP yao ni asilimia chini ya 10 ya wananchi wake waliajiriwa in the formal sectors. Unemployment rate ya Botswana ktk miaka hiyo ilikuwa kubwa zaidi ya Tanzania pamoja na kwamba idadi yao ilikuwa chini sawa na mkoa mmoja tu wa Tanzania.
Kisha nitarudia kusema kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya nchi TAJIRI na nchi ILIYOENDELEA pamoja na kwamba vitu hivi vinaenda sambamba. Ni vigumu sana kwa nchi maskini kuendelea hata zikiwa chini ya viongozi wazuri lakini sii lazima nchi tajiri ikaweza kuendelea ikiwa chini ya Utawala mbaya!
Botswana ni matajiri tena sana kuliko hata Dubai lakini ktk maendeleo wapo chini ya Tanzania.
Hizo nchi nyinginezo zilikuwa matajiri tayari kabla hata ya mkoloni hajaondoka! hasa Egypt na South Africa.
 
Ilikuwa Mei Mosi 1985, iliyofanyika Kitaifa Mkoani Tanga na kuhudhuriwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya Madola Bw. Sherdath Ramphal (or similar sounding name). Siku ya pili yake mvua kubwa ilinyesha mjini Tanga na kufanya barabara kubwa za lami zisipitike hasa kutokea Old Nguvumali, Kisosora, Chumbageni n.k Ikabidi Mwalimu na msafara wake wapite "Uswahilini". Ndipo nilipopata kuona Mwalimu alivyokuwa mtu wa watu... mimi na ndugu zangu tukawa tumejipanga kwenye geti la nyumbani (tulikuwa na kakibanda kakuuza machungwa toka Muheza) basi jua likiwa limeanza kupiga, na akiwa amechelewa kwenda uwanja wa ndege, msafara wake ulipita taratibu katika barabara hiyo ya mashimo (kwani haikuandaliwa kwa ajili ya msafara!) basi tu yeye kageuka upande mmoja tu anapungua watu, ndipo binamu yangu wa kike alipopiga kelele "Na huku!" Mwalimu akitabasamu akageuka na kutupungia... Ilikuwa ni siku ya furaha kwamba na sisi "tumesikiwa"... Since then, I have made it my mission... to be heard by our leaders!!
MM kumbe ulikuwa bebari mkubwa enzi hizo. Kuwa na biashara ya machungwa katikati ya siasa ya ujamaa si jambo dogo hata kidogo......hahahahah; just joking anyway!
 
Hebu ccm tuambieni mnamuezije mwalimu? mmekuwa kinyume cha kile alichokiamini; ulaji rushwa, wizi, majungu, fitna, udhalimu, uongo na ukandamizaji.
 
Baadhi wa wachangiaji wa hii mada wamepotea kabisa.

Natamani siku warudi tukumbuke ya zamani....
 
Back
Top Bottom