Nini kilikusaidia kupata kazi?

Nini kilikusaidia kupata kazi?

Samahani mkuu kukuuliza hivi.

Umesomea descipline ipi mkuu?. Nje ya kada yako unaweza kufanya kazi za kusogeza mabox masaa 9 ulipwe elfu 6 kwa siku?.
Iyo kazi naweza ifanya ila tu hapo ninapofanya iyo kazi wawe wanashughulika na kazi ya kada yangu (mechanical engineering)
ILA MKUU MIMI NILIKUWA NAHITAJI MAWASILIANO NA NDG. SITAYILA
 
Iyo kazi naweza ifanya ila tu hapo ninapofanya iyo kazi wawe wanashughulika na kazi ya kada yangu (mechanical engineering)
ILA MKUU MIMI NILIKUWA NAHITAJI MAWASILIANO NA NDG. SITAYILA
Ok njoo inbox nikupe .
 
Aisee kazi ukitafuta bila pressure ni easy kupata mi nimetoka zangu chuo sina hili wala lile kampuni niliyo fanya nayo field ikaniita nikapige nao mzigo nimefanya kama miezi sita ivi ikatokea mambo ya utumishi yani very fair hakuna connection wala nini nkaitwa kazini kupitia utumishi
 
Mimi niliandika uzi humu wa kutafuta kazi ,nashukuru nilipata responses za kunipa matumaini, nikawatumia watu CVs then nikapata sehemu nikafanya for a year,nikiwa pale nikaona tangazo kwenye group flani la WhatsApp la ajira, nikaapply nikapata kutokana na experience niliyoipata kwa Boss wangu wa humu jf. Much respect to him👏
 
Kuna dada mmoja kasoma Bachelor ya Kiswahili.. Yupo mtaani anatafuta kazi kwenye makampuni.. Nashindwa kumwambia kuwa kwa elimu yake ingekuwa rahisi kwa yeye kupata kazi iwapo angeenda kwenye mashule kutafuta kazi ya kufundisha!
Sasa anaendelea kuibemenda taaluma yake kwa kuendelea kukaa mtaani wakati uwezo wa kufundisha sarufi anao!

Mwambie kuna bandiko Embassy ya Marekani la muda sana, kuna zile program za exchange wenye degree ya Kiswahili ndio wana dit sana
 
Nimemaliza degree ya IT , niliomba ajira kila pahala ila nimeambulia patupu,utumishi ya serikali huko ndio nyumban kwan ilikuwa kila siku lazima nipitie portal yao, ninaitwa sana mpk oral ila sikuwahi kubahatika kupata, inafika pahala wanaweza kuitwa hata watu 3 hapo wanatakiwa 2 ila amini ndugu yangu siwezi kuitwa, nimesali sana na kuomba ila wapi, pale home wakaona ni mzigo kukaa pale kwani nikirudi nasimangwa kwa maneno mfano mbona fulani kapata kazi, ww unafeli wapi nk. Nikaona Isiwe tabu nikahama pale home nakaa gheto kwa sasa, kiufupi sasa hivi nauza matunda katika genge na mshikaji wangu niliesoma nae primary, na jioni nafanya betting maisha yanaenda. Sitakaa niombe tena Ajira yaan, najua kuna siku nitatoboa.
 
Umeamua kufanya maamuzi ya kiume mkuu, safi ajira ngumu kiukweli. Sema tukomae tu huenda mungu akatukunia nazi.
 
Back
Top Bottom