Nini kilikusaidia kupata kazi?

Nini kilikusaidia kupata kazi?

Acha tu mkuu, nilienda kwenye interview moja tena benk, tumefanya round one tulikuwa kama 300 hvi, tukatokea 10 kati ya wale 300, interview ilikuwa ya round w tu ndo mana walikata kutoka 300 mpaka kumi kupunguza idadi ya wanaoenda round ya 2 ambayo ni mwisho

Tulipoenda tulikuwa wanaume 2 na wanawake 8

Interview ikaendelea, ilipofika zamu yangu wakauliza maswali mpaka ya siasa, nkajibu

Mwisho wakaniambia eti nina mwili mdogo sitoiweza nafasi nanayoiomba mana nafasi hiyo chini yake kuna watu wengine wazima na wakubwa sana kimwil hivyo hawataniheshimu

Najuta kuwa na mwil mdogo, nilitaman Mungu aniumbe upya, mpaka leo npo mtaani zaid ya 5 yrs sasa
hahahaaa pole kuna interview niliambiwa nine over qualify
 
Inaonesha jamaa alikuwa intern ila anakula stipend ambayo hata vijana wengine waliopo kwenye mikataba rasmi hawapati.
Sema ela yake nwanzo ilikuwa ngumu, maana ilikuwa lazima kuandika working plan kila after two weeks, then ikipita ndio unapewa 500K, sema baada yakuaminiwa ndio hivo report akiandika zinaenda moja kwa moja anasubir cash yake tu.
 
Once again, please be informed we have advertised the following positions:
Child Rights Governance Specialist – Dar es SalaamFinance Officer – Kibondo, KigomaProcurement Officer (Buying) – Kibondo, KigomaProcurement Coordinator (Sourcing) – Kibondo, Kigoma

Kindly share the link with your network and encourage qualified candidates to apply. https://tanzania.savethechildren.net/careers



Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
Hivi hizi huwa kuna watu wanapata?

nilitamani kabla sijazeeka nitumikie career yangu Ila naona uzee umenipenda zaidi nimeishia kutumika kwenye kazi sijawahi kuzipenda
 
Nimemaliza chuo 2016.

Nimepigika kitaa bila kazi karibia mwaka mzima.

2017 mwezi wa Sita mshikaji wangu akanipigia simu kuna sehemu wanahitaji mtu wa taaluma yako. Nikapeleka CV isiyo na experience [emoji23]

Wakanipa nafasi ya kuanza kazi ila mshahara mdogo kweli. Nimerudi nyumbani bi mkubwa anauliza vipi huko imekuwaje nikamueleza nafasi ipo ila mshahara mdogo[400K] hivyo sitaenda kufanya. Bimkubwa akaniambia usiache hiyo kazi nenda kafanye. Ni rahisi kupata kazi ukiwa kazini kuliko ukiwa nyumbani.

Nikaanza kazi. Kama alivyo niambia bi mkubwa ni rahisi kupata kazi ukiwa na kazi ikawa kweli. Hapo ni kafanya kazi mda si mrefu nikapata sehemu inayolipa vizuri [emoji1488] Ikafikia kipindi hadi kazi nikawa nazikataa [emoji23]

Kuna siku jamaa kanitumia tangazo la kazi kwa vile CV nilikuwa nayo kwenye simu nikatuma ila sikuwa na lengo la kuacha nilipokuwa. Nikaitwa kwenye interview si kwenda.

Saa tano wakati nipo kazini HR wa hiyo kampuni ananipiga simu ananiuliza mbona sijaenda kwenye interview wakati wengine wapo wanaendelea na interview nikamueleza niko kazini. Huwezi akaniuliza wanakulipa shi ngapi wao wakanipa mara mbili nikaanza kazi.

Sasa hivi nipo serikalini shirika moja wapo kubwa la umma nakula maisha tu [emoji23]

Maneno ya mama ya kuwa ukiwa kazini ni rahisi kupata kazi yamekuwa halisi Sana kwenye maisha yangu. [emoji1488]
Ni kweli mkuu, ni rahisi sana mwenye nacho kuongezewa ila mkono mtupu huwa haulambwi kabisa.😂😂😂
"Heshimuni wazazi wenu mpate kuishi maisha mengi"
 
Mku iyo kitu toa akilini ukiendelea kuwaza hayo nakuhakikishia hutapeleka barua hata1. Kwanza private unapeleka mwenyewe tofauti na serikalini hadi mpitie utumishi mnapokuwaga watu zaidi ya elfu kumi
Private wenyewe wameadopt mfumo wa ajira portal. Kazi ku apply hutumi kwa email tu kama zamani. Lazma ujenge CV kwenye portal yao ndio u attach CV yako na ya mambo mengine.
 
Private wenyewe wameadopt mfumo wa ajira portal. Kazi ku apply hutumi kwa email tu kama zamani. Lazma ujenge CV kwenye portal yao ndio u attach CV yako na ya mambo mengine.
Mkuu hali imekuwa ngumu sana, sasa hivi biashara haziendi kabisa.
 
Dah kwa proffession yako mi nisingekubali kuwa mtaani..Binafsi naona hamna proffession rahisi kupata kazi kama uhasibu mkuu hata Diploma tu watu wanamenya.
Basi msaidie mkuu ili aweze kusogeza maisha mbele
 
Back
Top Bottom